You must be kidding me! - 21.9Millions USD?

Kha,tujifunze kuwa na shukrani waTanzania.Nadhani huu ni msaada tu(au ni mkopo?).Kama kiasi hiki kilichotolewa kitatumika vizuri/ipasavyo nadhani zitasaidia.Something is better than nothing!!!Hizo zilizoibiwa if possible we will recover some/all.Ila naona si sahihi pale tunaposaidiwa tukaanza kukebehi msaada huo.Unless if there are demands from him as a result of such an aid.

Umewahi kusikia tangazo moja la kibiashara la kutafuta mpangaji likisema hivi "you pay only one dollar for the first months rent" kwa pango ambalo gharama yake labda ni USD 1200. Wewe changamkia hiyo tenda na ingia kwenye mkataba, uone hiyo dola moja inakutoka puani.

Ukweli ni kuwa huu msaada ni kiduchu kwa viwango vya misaada lakini tusipo kuwa makini tutalipa fadhila hii kwa gharama kubwa. Tunachotakiwa kufanya baada ya kuipokea ni kuwa macho na any hidden agenda ya Wachina au mtu yeyote anayetupa msaada.

China hivi sasa wanatupa ndoana na sisi kama kawaida yetu, tunameza nzima nzima tena kwa mbwembwe. Huu msaada maana yake ni kuwa kila Mchina katupatia Tsh. 10/= na Si ajabu kila Mtanzania akaishia kurudisha Tsh. 100/= au zaidi kwa Mchina - kweli ombaomba hana haya wala akili.
 
aah...mwanakijiji nakubaliana na wewe moja kwa moja...hatuna sababu ya kuwa omba omba hivi! lakini ndo tunawarithisha watoto wetu utamaduni huu....nahisi na sisi tulirithishwa? kama ni hivyo wazazi wetu hawakuweza kabisa kufikiria kuwa huru...na maana yake hatujawahi kuwa huru!
 
Kama walitusaidia hivyo kwa nini bado tuko masikini/ mafukara?

Na kila siku tunapewa misaada....lakini hatuendelei. Why? Tatizo liko wapi? What is lacking? Na hii misaada tutaendelea kupewa hadi lini?

What is lacking ? I believe strategic interests.
 
...pesa zenyewe zinarudi kwao tuu kununua tractor za viwandani kwao na vifaa vya hiyo radio zanzibar na kulipa interest,ndio tujifunze hakuna msaada utakaotuondolea umaskini.....hizi dharau nimechoka!
 
somebody need to explain to me; Inawezekana vipi taifa ambalo limeweza kuruhusu kuibwa kwa dola bilioni moja ndani ya miaka kumi kuwa ni taifa hilo hilo lenye kukinga mikono kupokea misaada ya dola milioni 21?

Je yawezekana misaada hii inaficha pengo la kile kinachoibwa kiasi kwamba hatuwezi kuona kwa sababu wajomba zetu kila tunapoibiwa wanatuletea kitu kingine?
 
somebody need to explain to me; Inawezekana vipi taifa ambalo limeweza kuruhusu kuibwa kwa dola bilioni moja ndani ya miaka kumi kuwa ni taifa hilo hilo lenye kukinga mikono kupokea misaada ya dola milioni 21?

Je yawezekana misaada hii inaficha pengo la kile kinachoibwa kiasi kwamba hatuwezi kuona kwa sababu wajomba zetu kila tunapoibiwa wanatuletea kitu kingine?

...tatizo ni lile chama la CCM!
 
yaani tunajigamba kuwa tuna fedha wakati ni kwenye magazeti tu tena tunataka kuwa masjushaa wa kujiamini kwa kusoma fedha zilizoibiwa ,fedha haipo yamebaki mijinamba tu na waliokula tunapigana nao vikumbo yaani ni kheri hizo fedha za Mchina kuliko hizo tulizonazo ambazo hatunazo just zipo tu kwenye makaburasha.
 
the point is kuna misaada ya kijinga ambayo mtu mwenye akili timamu hastahili kuipokea. Hivi mtu akija nyumbani kwako akupe msaada wa godoro la kulalia na mke wako/mume wako utapokea, ukizingatia kuwa una magodoro yaliyo bora zaidi kwenye hifadhi yako?

Mpenda misaada ataseema "ndiyo nitapokea kwani msaada ni msaada"

Mpenda kujitegemea atasema "tatizo langu siyo magorodo ni paa!" so "help me with the paa ambalo sina uwezo nalo lakini hili la godoro I got it covered".

Sisi tunataka kutengenezewa paa, godoro, na kitanda.. tunachotaka ni kuwa tuwe na mahali pa kulala bila kulipa gharama ya kupapata mahali hapo!

What do you expect from Miafrika?
 
CCM wapi ndugu?????

Kenya na Malawi opposition now wameshika serikali karibu 10 years -ruswa tu mtindo mmoja!

...siku zote familia inapoyumba mara nyingi wazazi ndio tatizo,kampuni inapofell CEO na body yake ndio wa kwanza kulaumiwa na kutimuliwa,sasa hapa CCM kama kiongozi wa nchi sijui tumalaumu nani? au labda kuna some exception na CCM....tatizo letu naamini ni hao wanaotuongoza sio wananchi wala opposition!
 
“Small nations are like indecently dressed women. They tempt the evil-minded.” -J.K NYERERE.
 
...tatizo ni lile chama la CCM!

Hapa umeuwa Nyoka kabisa katika biashara hii wanaofaidika ni hawa wezi wetu CCM wasio jua vibaya wala wasio na haya ,wezi wa wa kila kitu hata ubinadamu wanajiona wao ni zaidi na sie waTz tulio wengi ni manamba tu ,tunawafanyia kazi wao mabwana wakubwa wakipita na magari ya fahari meno inje ,toka tupate uhuru Daresalama ambayo ndio Mji mkuu haujapata maji ya kuaminika wala drainage system hakuna ,au nasema uongo ?

Mji mikubwa Tanzania ilikuwa inahesabika wakati tunapata uhuru na hawakuweza kuipatia huduma bora zaidi ya zile walizozikuta kutoka kwa mkoloni mweupe ambae akitulimisha mkonge ,Pamba na menginetele lakini mambo yalikuwa poa ,je toka achukue CCM mpaka leo ni shida bin matatizo ,hakuna maendeleo ya kupigiwa mfano hata moja ,kila fisadi anaekuja hula akaondoka na kujifungulia mabiashara ,nani alieondoka ambae hana biashara yake kuanzia Mwinyi Mkapa na wengineo ?Wana majumba makubwa makubwa japo mimi siyajui lakini wapo wanayoyajua wakiwemo wao wenyewe, CCM toka iwe madarakani imepokea miasaada kibao mpaka wanaotoa misaada kifedha wakasituka kuwa fedha hazifanyiwi kazi tuliyoitolea misaada ,fedha inaliwa njiani kabla haijawafikia walengwa ,kweli si kweli ?
 
To put it in other words..

Kiasi hicho ambacho tunakishangalia ni chini ya kiasi ambacho JK mwenyewe aliweza kutoa kwa mikoa yote na baadaye kikajulikana kama "mabilioni ya Kikwete"..

La maana soma signature yangu tena...
 
Ni vyema kuwa na shukrani, ni sawa, tunashukuru kwa hicho walichotoa,lakini isiwe sababu ya kudhalilishwa, siku nyingine tunaweza kujifunza kukataa ikibidi. Inawezekana kulikuwa hakuna proposals za kueleweka. Hata hivyo dhana ya kuombaomba isipotutoka tutaendelea kusubiri hisani ya wajomba hivihivi, na kila anayekuja tunasubiria katuachia kiasi gani, matokeo yake tunabakia palepale. Tatizo lingine si ukubwa wa msaada au mkopo,tatizo tunautumiaje kututoa pale tulipo? Hiyo Reli ya Tazara ni afadhali miaka hiyo ya 70 kuliko sasa, urafiki ni afadhali ya zamani kuliko ya sasa, tunaenda mbele au tunarudi nyuma? Tunaweza hata kupewa stimulus package yote ya Obama bado tukabaki hivihivi. Suluhisho letu hapa ni kubadili fikra na tufanye kazi kuendeleza nchi yetu.
 
Umewahi kusikia tangazo moja la kibiashara la kutafuta mpangaji likisema hivi "you pay only one dollar for the first months rent" kwa pango ambalo gharama yake labda ni USD 1200.

China hivi sasa wanatupa ndoana na sisi kama kawaida yetu, tunameza nzima nzima tena kwa mbwembwe. Huu msaada maana yake ni kuwa kila Mchina katupatia Tsh. 10/= na Si ajabu kila Mtanzania akaishia kurudisha Tsh. 100/= au zaidi kwa Mchina - kweli ombaomba hana haya wala akili.


Mag3,
Unataka kusema huo msaada ni kama huu wimbo wa AEROSMITH? Hebu anzia kuangalia hii video kwenye 3:40. Duu, hiyo Sandwich kweli inaonekana tamu ila ........

[ame=http://www.youtube.com/watch?v=TmE3K3yJops]YouTube - Aerosmith- Girls of Summer[/ame]
 
.... and in no time, a single Tanzanian (not such a tycoon) known as Liyumba will finish his bail worth $55mil...
 
Back
Top Bottom