Hakuna kitu kama hicho, wewe Bashe naona bado unaendelea na matusi mazito kwa watanzania, Na katika hili unaombwa kutuomba radhi.
Ulichokifanya wewe ni kimbelembele cha kutoa kauli hii ili uonekane muungwana, au una au umebakiwa na hekima kiasi kichwani mwako na ni jitihada za kujivua jinamizi la kushindwa, wewe ulikuwa arumeru ukifanya kampeni, kama wakati wote wa kampeni na kabla ya Kampeni of course,ulikuwa haujui kwamba Watanzania hatuitaki CCM na kama ni kweli matokeo ya Arumeru ndio yamekufumbua macho kwamba CCM haitakiwi nchi hii basi wewe ni mmoja kati ya watu vilaza sana wenye lika kama lako.
Nani kakumbia kwamba watanzania wamekasirishwa na makundi yaliyo ndani ya CCM, nani? Funguka Macho we mgeni, CCM mmeonyesha mshikamano mkubwa sana Arumeru Mashariki, Nape Niyauwe amepnda Jukwaa moja na Manywele, what a solidarity? mbona wanaarumeru hawakudanganyika.
CCM moja au yenye makundi haihitajiki Tanzania, tena umeniudhi sana, na hapa umezidi kunithibitishia kwamba wewe sio Mtanzania, watanzania wanalilia elimu, huduma za afya, unafuu wa bei na upatikanaji wa vyakula wewe unasema wanachukizwa na mkundi.
Kweli akutukanaye akuchagulii tusi, nashukuru kwa kuniharibia furaha yangu ya ushindi.
Nami nikupongeze wewe Bashe kwa kuipongeza Chadema. Unaakili sana na uwezo kisiasa lakini wenzio CCM hawakutaki. TAFAKARI CHUKUA HATUA.
Huyo Bashe alishiriki katika hujuma dhidi ya mtiririko wa haki ya kidemokrasia huko Arumeru. Alitumia gazeti lake la RAI kupenyeza opinion poll za uongo kuonyesha CCM ingeshinda kwa asilimia 68 -- kumbe ilikiwa ni maandalizi kwa CCM+NEC kuiba kura! kulikuwa hakuna waandishi wa RAI waliokwenda kufanya opinion poll kule. Aache unafiki.
Bashe CCM siyo Mungu kwako,siyo mama wala baba yako.Kama unadhamira ya dhati basi jiunge na wapambanaji wa kweli kwa lengo la kulikomboa taifa kutoka kwa mafarao wa CCM!Siyo leo unasema hivi halafu kesho unawaambia wandishi wa magazeti yenu na Tbc yenu kuponda ukweli!yuko wapi Tido Muhando?eti kisa alijitahidi kutoa wigo sawa wa habari wakati wa uchaguzi 2010!Magamba hamfai kabisa!
Hongera sana Bashe,siasa za kistaarabu hivi ndizo zinazotakiwa . Kama utakubalianana itikadi ya chama changu,hamia chadema tufanye kazi.Chama kilichothubutu kusahau kuwasikiliza wananchi (kama ulivyosema) kwa muda wa miaka 5 (2007-2012) hakistahilimandate,kime-cease kuwa chama cha siasa
Kama utasukumwa na uzalendo wa dhati kwa taifa letu na kama umekosa imani kabisa na chama chako(of course hakina tumaini) basi ungana na upande wa harakati,ungana na chama chenye rekodiya kusikiliza wananchi wake.Najua kwa mawazo yako haya,chama chako kitaanza kukuona adui kwani CCM hakitaki tena fikra mpya.Karibu kamanda
work up call au wake up call? Huyu Bashe ni mkurugenzi wa wapi vile?
Bashe amesema kweli ila aangalie tu na yeye asije akapata cheo maarifu cha GAMBA halafu wakajenga hoja ya kumvua ndani ya chama. Kwa ujumla hatutegemei jipya lolote kutoka kwa chama ambacho kinaongozwa na wastaafu (kwa maana ya umri wa miaka 60 au zaidi) toka kwa mwenyekiti (over 60), makamu wa mwenyekiti bara (over 70), Makamu mwenyekiti Zanzibar (over 60), Katibu Mkuu (over 60) n.k. Hawa enzi zao zilishapita na ndio waliotufikisha hapa tulipo kiuchumi, kisiasa na kijamii. Wanachotakiwa kufanya kwa sasa ni kimoja tu kumuenzi muasisi wa CCM kwa KUNG'ATUKA.
Ukiangalia age profile ya kamati kuu ya CCM ndio unaishiwa nguvu kabisa imejaa watu ambao walitakiwa kuwa kwenye HOSPICE wakisubiri mwenyezi afanye maamuzi mepesi ya kuwapumzisha. Hivi unatarajia kampeni inayoongozwa Mkapa, Wassira, Mukama, Lowassa, Ole sendeka, Ole Medeye na akina Mwigulu na Lusinde itawavutia vijana kweli kukipigia kura CCM?
Kwa bahati mbaya zaidi hawa wazee wameathiri mtazamo wa vijana ndani ya chama ambao ukiwasikiliza kwa makini unagundua kuwa ni vijana kwa muonekano wa nyuso na miili yao lakini ni wazee wastaafu kwenye bongo zao. Sikutarajia, kwa mfano, kumsikia NAPE akidai kuwa CCM itatawala milele ikiwa ni majibu kwa baadhi ya wazee wenye nia njema ambao walikuwa wakiitahadharisha CCM kuwa inaoelekea siko.
Kwa ufupi mageuzi yanayotakiwa ndani ya CCM ni makubwa mno sawa na kuanzisha chama kipya ndani ya chama. Wazee wa CCM ambao kimsingi ndio wanaotarajiwa kufanya mageuzi hayo kamwe hawawezi kwa sababu umri wao hauwaruhusu. Akina Bashe, Nape, Makamba, Mwigulu, Lusinde na wengineo ndio wanaotakiwa kuleta mageuzi ikiwa tu watafikiri kama vijana na sio kufuata mawazo yaliyochoka ya wazee wao.