Yondani aanza kujuta Yanga

bemg

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
2,799
642

• Adaiwa kuutaka ‘mzigo’ wa Twite arudi Simba

na Dina Ismail


amka2.gif
UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya Firauni. Katika hali isiyotarajiwa, beki aliyesajiliwa kwa mbwembwe na mabingwa wa Kombe la Kagame, Yanga, Kelvin Yondani ameanza kujutia uamuzi wake huo na kutaka kurejea klabu yake ya zamani, Simba.
Habari za uhakika zilizopatikana jijini Dar es Salaam jana, zinaeleza kuwa, Yondani tayari amebainisha mawazo yake hayo kwa viongozi wake wa zamani wa Simba, ambao ndio watu wa karibu na wanaomsapoti kwa mambo mengi.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa, Yondani amewaambia wadau wake hao wa Simba kuwa, watakaporejeshewa fedha zao dola 30,000 walizompa beki Mbuyi Twite, wampe yeye ili afanikishe kurejea Msimbazi.
Simba ilitangaza kumsajili Twite kwa kitita hicho, kabla kuzidiwa kete na Yanga, huku beki huyo akituma wawakilishi nchini kurejesha fedha alizochukua awali, jambo ambalo lilikataliwa na Wekundu wa Msimbazi, ambao walimtaka mchezaji huyo azirejeshe mwenyewe.
“Unajua Yondani hivi sasa hajisikii vizuri, kwani hata watu wake hao wa karibu wa Simba wamehuzunishwa sana na uamuzi wake wa kuhamia Yanga, hivyo hata ule ukaribu wa awali umepungua, hivyo kawafuata na kuwataka kurejea,” kilisema chanzo hicho.
Imeelezwa kuwa, katika makubaliano ya Yondani kusajiliwa Yanga, alilipwa sh milioni 15 na kiasi kilichobaki atamaliziwa baadaye, hivyo amekubaliana na Simba wampe fedha hizo za Twite, ili arejeshe kiasi alichochukua Jangwani.
Sababu nyingine inayoelezwa Yondani kujuta kusaini Yanga, ni hofu ya kuwepo kwa vita ya namba katika kikosi cha mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati.
Habari hizo zimedokezwa huku suala la usajili wa Yondani likigubikwa na utata mkubwa baada ya Simba na Yanga zote kumsajili kwa ajili ya Ligi Kuu ya Bara.
Tayari sekretarieti ya Shirikisho la Soka Tanzani (TFF), limeagiza Kamati ya Nidhamu, Maadili na Hadhi za Wachezaji, kufanya maamuzi.
Hiyo inatokana na Yondani kujiunga na Yanga kwa kitita cha sh milioni 30 kama mchezaji huru, hoja ambayo inapingwa na Simba, ikisema bado ni wao.
Kwamba, ingawa mkataba wa Yondani ulikuwa ufikie ukomo Mei 31, mwaka huu, lakini Desemba 23, 2011, waliurefusha, ingawa mwaka unasomeka 2012.


Tanzania daima
 
anategeneza mazingira ili TFF ikisema ni mchezaji wa simba tusiwe na kinyongo nae acha asugue benchi huko jangwani na akirudishwa simba ni bechi tu mpaka akome.
 
Kelele za magazeti tu hizo, kama wanafahamiaba na hao watu wa karibu wa Yondani mbina hawakuripoti tetesi za usajili wake Yanga
 
Waongee tu wamalizane arudishe pesa za watu kama hana amani na club sio lazima ati
 
Teh teh SIMBA KAPAKATWA bado mnaweweseka jamani nyie si mnakuza vipaji jamani na makinda yenu yanauwezo eti kuliko TWITE na YONDANI sasa mwalalama nini tena.
 
hayo maneno ya wafa maj (cmba) kwan sa hiv c ndo wanatapatapa kwnye kilind ch bahar ya shida hao
 
simba oyeeeeeeeeee.Yondani kamalizie mpira huko2
 
Arudi??? Aje kucheza namba ya nani??? Pale kati kuna ochieng na kapombe. Pia kuna wale Hassan wawili wa kikosi cha pili. Sioni namba yake pale. Huyo mwehu mwenzake Nyosso atachoma sana mahindi mwaka huu

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Poleni sn mbona ngasa yondani anawauma hivo,. Haya mpigeni risasi basi tumkose wote
 
Waongee tu wamalizane arudishe pesa za watu kama hana amani na club sio lazima ati
Ni kweli, alafu unajua kama ameshatumia pesa aliyopewa kufanyia la maana ni nzuri sana, na ni mbinu nzuri hata akiambiwa kuwa bado ni mali ya Simba hatopaswa kurudisha hizo pesa, la maana atakuwa kazifanyia la maana katika maisha yake, na hata akifungiwa hamna shida, kesha vuta mkwanja tayari, hasara kwa hao wahusika, yeye bado kijana atafanya mazoezi kujiweka fit kwa usajili wa mwakani.
 
Hata mimi naona anajuta,
11.JPG

Yondani na wenzake akijuta huko Kigali, hapa walikuwa Ikulu ya Rwanda wakijiandaa kupata msoc na President Paul Kagame.
 
Yondani is not a big deal; there is no need of entertaining him, we have Keita & Ocheing one of them w'll take the lead.
 
Teh teh SIMBA KAPAKATWA
bado mnaweweseka jamani nyie si mnakuza vipaji jamani na makinda yenu
yanauwezo eti kuliko TWITE na YONDANI sasa mwalalama nini tena.

nani analalama?huyo hana namba tena iwe simba ua yanga!ataweka benchi Twite au Pascal Ochieng' ?elewa hivo!
 
Back
Top Bottom