Yona na Mramba: Mashtaka na yatokanayo

Yani am anxious to know about this PLEASE can anyone confirm it from sources za Kisutu?
Hii ni habari njema sana kwa taifa hili.
How about Mgonja?IT WILL MARK OUR STRUGGLE AGAINST FISADIZ
 
Wakuu,

Popcorns zaidi! Nimekunja mguu wangu, sinema linazidi kunoga, hatoki mtu hapa leo.

Nani huyo? Mramba na Mgonja? Hata bila kujua title ya picha yenyewe lakini kwa actors wa five stars kama hao, naamini sinema litanoga tu.
 
Hii habari niliandika wiki iliyopita wakati walipotakiwa kupelekwa mahakamani lakini ikaahirishwa sababu ya Send off ya mtoto wa Mramba.... yote yatatimia.
mhmm! yaaani anaruhusiwa kuhudhuria send off kwanza! kweli sheria ina heshima.
 
Hii habari ni ya kweli,nimepata taarifa kutoka kwa mtu ambaye yupo mahakamani kisutu sasa hivi
 
Siku nikiwa na kosa, polisi wakija kunikamata nitawaambia ngojeni nimalizie weekend inayokuja kwanza, wakilazimisha nawauliza mbona Mramba mlingoja amalizie send off ya mtoto wake?. Patakuwa hapatoshi kweli kweli wakilazimisha!

I love Bongo.
 
Serikali inaonekana kuwa serious.Watuhumiwa wa EPA awali nilikuwa nikidhani hawaguswi na sasa haooo....leo hii nasikia tena kina Mramba na yona wamefikishwa mahakamani ! I love this!
 
Kazi ya Pinda kijana wa Mwalimu mnaiona sasa?.... Sio kila mchapakazi lazima anunue waandishi weeengi wa kumjenga magazetini kila siku.

Nina hakika haya yasingewezekana asilani kama EL angebaki madarakani mpaka leo.

Maana kwa EL majizi yote ndio yalikua yanapata kinga, kuanzia Nyari, Lukaza, Manji etc...
 
Mama Mdogo mbona unanipa presha mwenzio???

Ndugu yangu, imenibidi niahirishe mihanjohanjo ya maisha ili nirudi Kisutu. Nimehakikishiwa ni kweli wako ndani ya mahakama na sheria inachukua mkondo wake. Kusherehekea mwanso wa anguko la mafisadi, naenda hapo Subway kupata mlo wa kushangilia ushindi. Karibu tupate chochote kama uko Dar tumpongeze DPP kwa uamuzi mzito.
 
Bado haijsemwa bibie.......tulia kidogo nadhani hapa itajulikana tu


tusubiri tuwe na uhakika wa mashtaka yanayowakabili kati ya mengi yanayosemwa

Anyebisha asikilize redio ... clouds 88.4 ndio wanatangaza sasa
 
Ndugu yangu, imenibidi niahirishe mihanjohanjo ya maisha ili nirudi Kisutu. Nimehakikishiwa ni kweli wako ndani ya mahakama na sheria inachukua mkondo wake. Kusherehekea mwanso wa anguko la mafisadi, naenda hapo Subway kupata mlo wa kushangilia ushindi. Karibu tupate chochote kama uko Dar tumpongeze DPP kwa uamuzi mzito.

Mwenzangu mwenzio nasherekea kwa kula majani kama Pesambili alivyotutaka kipindi kile kwamba tupende tusipende ikiwezekana hata majani tutakula mradi ndege ya Rais inunuliwe. Leo sili.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom