Yohana Mwatebela is no more

Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Dec 6, 2006
3,020
576
Yohana Mwatebela mwenye makazi yake mjini mbeya ni jina linalofahamika na wengi. Ameaga dunia usiku wa juzi kuamkia jana kwa shinikizo la damu kwa kadiri ya vyanzo muhimu vya habari. Alizaliwa Kijiji kinachoitwa Mbigili kule Rungwe Mashariki ndani ya Tarafa ya Busokelo, akasoma shule ya Msingi ya Mwakaleli enzi zile, kisha akaenda Kigulu ikiwa wilayani Njombe enzi zile. Akachaguliwa kwenda sekondari Njombe 1976 na kisha alijiunga na CBG Tosamaganga 1980 na baadaye alisomea mambo ya Benki IFM ya DSM na kufanyia kazi NMB Mbalizi branch Mbeya. Kukatokea matatizo yaliyosababisha wafanyakazi wengi kuondolewa kazini, kesi ikiendelea akaonekana hahusiki lakini yeye aligoma kurudi kazini , akaendelea na shughuli zake kumfanya aishi hadi umauti wake.

Kwa taarifa hii fupi, naamini wapo wengi wanaoweza kumkumbuka kwa namna moja au nyingine. Hakuwa muongeaji sana lakini alikuwa mwepesi kushirikiana na mtu yeyote. Bila hata ya kueleza mengi, Mungu aiweke roho yake Yohana Mwatebela mahali pema peponi, Amen.
 
ndo namsikia leo. naskitika sitamuona maishani mwangu. rip yohana mwatebela.
 
RIP marehemu, ni ukweli usioepukika kuwa familia yako na marafiki watakukosa, lakini liko tumaini moja kuu-Yesu Kristo!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom