Yatokanayo na Kamati Kuu ya CHADEMA-Tamko Rasmi la Chama

Naomba nikwambie Viongozi wa Chadema wanaakili timamu zenye mawazo makini.Waziri mkuu tulishamwambia amelidanganya bunge na ujumbne umemfikia vizuri.

Ndani ya siku Tisa walizotoa viongozi,Kikwete ametoa matamko kadhaa katika wizara alizotembelea mf:

  1. alipokuwa katika wizara ya fedha alimuagiza waziri wa fedha kupunguza kodi katika bidhaa mbalimbali ili kumpa unafuu wa maisha.
  2. Bei ya Sukari iliyokuwa inakimbilia 2300 serikali imeamuru ibaki 1700
  3. Deni la Dowans kutolipwa na kutafuta njia mbadala.
Sasa ulitaka nini zaidi?huono AMETEKELEZA maagizo.

Lakini bado Viongozi wa chadema walisema ndani ya siku mia moja wazee waafrika mashariki malipo yao yatashughulikiwa,KIKWETE ALIAGIZA ALIP[OKUWA HAZINA KWAMBA SASA IMETOSHA WAZEE HAO WALIPWE.tena ametoa maagizo huku akijua kesi iko mahakamani.

ULIPASWA KUSEMA KAMA AHADI NA MAELEKEZO YA KIKWETE YASIPOFANYIWA KAZI VIONGOZI WA CHADEMA WATACHUKUA HATUA GANI UNGEELEWEKA.

Kuhusu Arusha usiwe na haraka subiri siku 21.Viongozi wa chadema ni watu wenye mipango thabiti na mikakati mizuri.

MISIMAMO HUWA INATOLEWA BAADA YA KUTOA MDA KWA UPANDE WA PILI.KWNI HIYO NI HAKI YA MSINGI KISHERIA.

Mmmh! Hii imetulia.
Hapa JF napakubali. Kilaza yeyote akiomba data anapewa, shida inabaki kwake - kupotezea au kukubali yaishe.
 
Naomba nikwambie Viongozi wa Chadema wanaakili timamu zenye mawazo makini.Waziri mkuu tulishamwambia amelidanganya bunge na ujumbne umemfikia vizuri.

Ndani ya siku Tisa walizotoa viongozi,Kikwete ametoa matamko kadhaa katika wizara alizotembelea mf:

  1. alipokuwa katika wizara ya fedha alimuagiza waziri wa fedha kupunguza kodi katika bidhaa mbalimbali ili kumpa unafuu wa maisha.
  2. Bei ya Sukari iliyokuwa inakimbilia 2300 serikali imeamuru ibaki 1700
  3. Deni la Dowans kutolipwa na kutafuta njia mbadala.
Sasa ulitaka nini zaidi?huono AMETEKELEZA maagizo.

Lakini bado Viongozi wa chadema walisema ndani ya siku mia moja wazee waafrika mashariki malipo yao yatashughulikiwa,KIKWETE ALIAGIZA ALIP[OKUWA HAZINA KWAMBA SASA IMETOSHA WAZEE HAO WALIPWE.tena ametoa maagizo huku akijua kesi iko mahakamani.

ULIPASWA KUSEMA KAMA AHADI NA MAELEKEZO YA KIKWETE YASIPOFANYIWA KAZI VIONGOZI WA CHADEMA WATACHUKUA HATUA GANI UNGEELEWEKA.

Kuhusu Arusha usiwe na haraka subiri siku 21.Viongozi wa chadema ni watu wenye mipango thabiti na mikakati mizuri.

MISIMAMO HUWA INATOLEWA BAADA YA KUTOA MDA KWA UPANDE WA PILI.KWNI HIYO NI HAKI YA MSINGI KISHERIA.

inaelekea mtoa mada haelewi uhalisia wa mambo. Nashukuru umemjibu vyema kabisa GeniusBrain!
 
Hivi huyu Mbowe na viongozi wengine wa CHADEMA wana akili sawa sawa kweli ? Waziri Mkuu , Mh. Pinda aliisha litolea Bungeni ufafanuzi vizuri na ambao uko wazi juu ya msimamo wa serikali kuwa uchaguzi wa umeya wa Arusha ulikuwa huru na halali, sasa kutoa siku 21 kwa serikali kumaliza tatizo la umeya wa arusha kuna maana gani ?. Hapa walicho takiwa kufanya ni kutoa msimamo wa chama na si kutoa kauli za muda, kwani serikali iliisha toa msimamo wake. Na hapa ndipo umakini wa viongozi wa CHADEMA unapotiliwa mashaka wa kutoa kauli badala ya mustakabali. Tuliona Mwanza walitoa siku 9, ziliisha hivi sasa tangu kauli ile zimepita siku zaidi ya 20, sasa kama kauli zisizo kuwa na vitendo ni bora zisitolewe kabisa.

Kwani we ujui kuwa Chadema ni wanafiki ni watu wa kupenda sifa na kujitafutia umaarufu kupitia magazeti.

Watasema watatoa siku lakini meya ni yule yule. hakuna mabadiliko. Full stop
 
Naomba nikwambie Viongozi wa Chadema wanaakili timamu zenye mawazo makini.Waziri mkuu tulishamwambia amelidanganya bunge na ujumbne umemfikia vizuri.

Ndani ya siku Tisa walizotoa viongozi,Kikwete ametoa matamko kadhaa katika wizara alizotembelea mf:

  1. alipokuwa katika wizara ya fedha alimuagiza waziri wa fedha kupunguza kodi katika bidhaa mbalimbali ili kumpa unafuu wa maisha.
  2. Bei ya Sukari iliyokuwa inakimbilia 2300 serikali imeamuru ibaki 1700
  3. Deni la Dowans kutolipwa na kutafuta njia mbadala.
Sasa ulitaka nini zaidi?huono AMETEKELEZA maagizo.

Lakini bado Viongozi wa chadema walisema ndani ya siku mia moja wazee waafrika mashariki malipo yao yatashughulikiwa,KIKWETE ALIAGIZA ALIP[OKUWA HAZINA KWAMBA SASA IMETOSHA WAZEE HAO WALIPWE.tena ametoa maagizo huku akijua kesi iko mahakamani.

ULIPASWA KUSEMA KAMA AHADI NA MAELEKEZO YA KIKWETE YASIPOFANYIWA KAZI VIONGOZI WA CHADEMA WATACHUKUA HATUA GANI UNGEELEWEKA.

Kuhusu Arusha usiwe na haraka subiri siku 21.Viongozi wa chadema ni watu wenye mipango thabiti na mikakati mizuri.

MISIMAMO HUWA INATOLEWA BAADA YA KUTOA MDA KWA UPANDE WA PILI.KWNI HIYO NI HAKI YA MSINGI KISHERIA.

Suluhisho na Arusha ni mahakamani tu , nawashangaa sana CHADEMA, haki inatolewa na nani kama sio mahakama ? ni utamaduni gani ambao wanatujengea wa kutofuata sheria ? na haya ndio yamesababisha vifo vya watu wa arusha
 
Mbona mnapoteza muda kubishana na watu wasio na upeo?, mie kuna watu humu nilishaacha kupoteza muda wangu kujibizana nao. Kweli ni kupoteza muda bure kujaribu kumuonyesha fisadi na ndugu zake ukweli kuhusu Tanzania na maisha ya watanzania.
Marehemu Nyerere aliwafananisha hawa sawa na manyag'au. Mnajua manyang'au ni kitu gani? kiswahili siku hizi kimesogea mbele zaidi. Nani anajua manyang'au ni nini?
 
Naomba nikwambie Viongozi wa Chadema wanaakili timamu zenye mawazo makini.Waziri mkuu tulishamwambia amelidanganya bunge na ujumbne umemfikia vizuri.

Ndani ya siku Tisa walizotoa viongozi,Kikwete ametoa matamko kadhaa katika wizara alizotembelea mf:

  1. alipokuwa katika wizara ya fedha alimuagiza waziri wa fedha kupunguza kodi katika bidhaa mbalimbali ili kumpa unafuu wa maisha.
  2. Bei ya Sukari iliyokuwa inakimbilia 2300 serikali imeamuru ibaki 1700
  3. Deni la Dowans kutolipwa na kutafuta njia mbadala.
Sasa ulitaka nini zaidi?huono AMETEKELEZA maagizo.

Lakini bado Viongozi wa chadema walisema ndani ya siku mia moja wazee waafrika mashariki malipo yao yatashughulikiwa,KIKWETE ALIAGIZA ALIP[OKUWA HAZINA KWAMBA SASA IMETOSHA WAZEE HAO WALIPWE.tena ametoa maagizo huku akijua kesi iko mahakamani.

ULIPASWA KUSEMA KAMA AHADI NA MAELEKEZO YA KIKWETE YASIPOFANYIWA KAZI VIONGOZI WA CHADEMA WATACHUKUA HATUA GANI UNGEELEWEKA.

Kuhusu Arusha usiwe na haraka subiri siku 21.Viongozi wa chadema ni watu wenye mipango thabiti na mikakati mizuri.

MISIMAMO HUWA INATOLEWA BAADA YA KUTOA MDA KWA UPANDE WA PILI.KWNI HIYO NI HAKI YA MSINGI KISHERIA.[/QUOTE]

thanks josephine,

umesema vizuri sana, nimeonyesha misitizo kwenye nyekundu hapo juu kwasababu kwa watu wa sheria kina kitu wanakiita exhaustion of local remedies. wakiimanisha unatumia hatua za awali zinazopatikana kwanza zikishindikana ndo unakwenda mahakamani.
 
Tusiongelee mate na wino upo. Nafikiri Chadema acheni mikwara.

Bi Sofi anawasubiri mahakamani.......... acheni danganya toto

Wewe ndio msemaji wake? au karani wake? au mpo wote kule kwenye umoja wenu wa wanawake wa ccm UWT?
 
kwa kkifupi huyu mama hawez hata kuongoza kijiji, lakin nashangaa anapewa wizara nyeti yenye kuhusiana na masuala ya watoto, atawaharibu tu, hafai kuwa waziri wala mwenyekiti wa kijiji huyu, ni mgomv, mropokaji,mbishi, hana busara, nawashangaa hata waliompa uenyekiti wa UWT-CCM.
 
mwisho wa Sophia Lion ndio umefika huo, this time she's dealing with people who know what are they doing.
byeeeeeee SS
 
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa hakina nia, ajenda wala lengo la kuipindua serikali iliyoko madarakani kwa njia ya
maandamano, bali hofu na woga alionao Rais Jakaya Kikwete na viongozi wengine inatokana na kushindwa kutekeleza ahadi na kuwajibika kwa wananchi.

Kimesema kuwa pamoja na kuenezwa propaganda hiyo ya kupindua serikali, na nyingine kama za kuvuruga amani ya nchi, ukabila, udini na kufadhiliwa, hakitaacha kufanya kazi yake ya siasa ya kuiwajibisha serikali, kwa kusimamia hoja za wananchi juu ya mwenendo wa nchi na viongozi wao.

Kimesema maandamano ya amani yanayotumika kuishinikiza serikali kuwajibika kwa wananchi si kuhatarisha amani ya taifa, "bali kwa viongozi wabovu wa CCM na serikali yake wanaohofia nguvu ya umma ya Watanzania wanaoanza kuamka, kuelimika na kuhoji juu ya mwenendo wa serikali na viongozi wao".

Kimesema pia kuwa kamwe hakitakubaliana na hila za aina yoyote zinazofanyika kulitia taifa aibu ikiwemo kutaka kubadilisha Sheria ya Manunuzi ya Umma (PPRA) ili serikali inunue vifaa chakavu na kuingia biashara ya aina yoyote na kampuni tata ya Dowans.

CHADEMA kimesema kuwa kitaendelea kutumia 'majukwaa' yote mawili, ndani na nje ya bunge, kutetea maslahi ya Watanzania na nchi kwa ujumla, kikisema kuwa hayo ni muhimu zaidi kuliko kitu chochote kile, hasa katika eneo la nishati ya umeme, ambako kimedai kuwa kuna miradi ya kitapeli inaibuliwa kila kukicha kwa faida ya 'wachache wanaotengeneza mabilioni ya bure.'

Hayo yamesemwa jana na Mwenyekiti wa chama hicho, Bw. Freeman Mbowe alipokuwa akitoa tamko la Kamati Kuu ya CHADEMA, ambapo alisema "kauli za Rais Kikwete kwamba maandamano haya yalilenga kuiondoa serikali iliyo madarakani kwa njia zisizo za kidemokrasia ni uzushi na uwongo."

Alisema kuwa amani wanayozungumzia viongozi waandamizi wa serikali akiwemo Rais Kikwete kuwa itavurugwa, wakihofia kazi ya kisiasa inayofanywa na CHADEMA "ni amani ya CCM na viongozi wake ambao kwa miaka yote walizoea kuishi kana kwamba nchi ni mali yao, badala ya kujiona kuwa ni watumishi wa wananchi waliowachagua kuongoza".

Tamko la Kamati Kuu ya CHADEMA lilisomwa na Bw. Mbowe akisaidiana na Katibu Mkuu wake, Dkt. Willibrod Slaa katika kujibu maswali ya waandishiwa habari, lilijikita katika maeneo kadhaa, ambayo ni kuhusu maandamano ya mikoa ya Kanda ya Ziwa, maandalizi ya ziara na maandamano mengine katika mikoa mitano ya Nyanda za Juu Kusini na Uchaguzi wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA).

Maeneo mengine yalikuwa ni kuhusu vitisho vya kuuawa kwa Dkt. Slaa na viongozi wengine wa kisiasa nchini, suala la uchaguzi wa Meya Arusha, tatizo la umeme nchini, suala la mabomu ya Gongolamboto, janga la tsunami huko Japan, uamuzi wa serikali kuandaa mswada wa kubadili Sheria ya Manunuzi ya Serikali;

Pia azma ya serikali kuwekeza katika uchimbaji wa uranium, mikakati ya kukabiliana na janga la njaa linaloikabili nchi kwa sasa na suala la kupanda kwa deni la taifa kwa kiwango cha asilimia 18 ndani ya mwaka mmoja.

"Kamati Kuu imesisitiza kuwa CHADEMA ni chama cha kidemokrasia na kitaendelea kutafuta ridhaa ya wananchi ya kuunda serikali kwa njia ya kidemokrasia na kwa mujibu wa sheria za nchi na wala haina dhamira ya kuiondoa serikali kwa njia zisizo za kidemokrasia.

"Kamati Kuu ilipokea na kujadili kwa umakini tathmini ya maandamano yaliyofanyika kanda ya ziwa, pamoja na matamko yaliyotolewa na viongozi wa serikali na CCM, wakiwemo Rais Kikwete, mawaziri Bernard Membe, Stephen Wasira, Sophia Simba na John Chiligati...Kamati Kuu imesikitishwa na kauli zilizotolewa na viongozi hao wa serikali na CCM.

"...zinaashiria kuwa viongozi wa CCM hawajui maana na kazi za vyama vya upinzani...Kamati Kuu inapenda umma uelewe kuwa maandamano ya CHADEMA Kanda ya Ziwa yalifanyika kwa taratibu zote za nchi na yalikuwa ya amani tele. Kamati Kuu inapongeza Jeshi la Polisi pale ambapo halikuingilia maandamano hayo pasipo lazima. Malengo ya maandamano yaliainishwa waziwazi kabla, wakati na baada.

"Operesheni zote za kisiasa za CHADEMA hugharamiwa kwa njia ya michango ya viongozi na wanachama pamoja na ruzuku ambayo chama hupokea kutoka Serikali Kuu. CHADEMA haijawahi na wala haina mpango wa kupokea fedha kutoka mataifa ya nje kwa ajili ya maandamano...mbinu za kisiasa kama hizi ni chafu na haziwezi kuiponya CCM magonjwa inayougua.

Bw. Mbowe alisema kuwa CCM imechokwa na wananchi na kuondoka kwake madarakani ni suala linalosubiri muda uamue, akisema kuwa Kamati Kuu hiyo imetambua kuwa Rais Kikwete ameanza kutekeleza walau kwa 'maneno' madai ya msingi yaliyotolewa na chama hicho, ikiwemo kuchukua hatua za kushusha bei ya sukari na gharama za umeme.

"Rais Kikwete na serikali yake wasiwe wazito wala wasione aibu kutekeleza yale yote ambayo CHADEMA inawashauri yenye manufaa kwa nchi lakini wayatekeleze kwa ukamilifu na ufanisi badala ya kufanya kiini macho. Watanzania wana haki ya kudai maisha bora kwa kuwa wameahidiwa muda mrefu na serikali.

"Ni wajibu wa serikali kufanya hivyo kwa kuwa inawatoza kodi wananchi. Kodi ni lazima ziendane na huduma inayolingana, na rasilimali za taifa lazima kwanza ziwanufaishe wananchi wenyewe na si vinginevyo," alisema Bw. Mbowe.

Alisema pia kuwa kamati kuu ya chama hicho imepokea kwa tahadhari na maskitiko taarifa za kuwepo njama za mauaji dhidi ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa, pamoja na wanasiasa wengine nchini, zilizotolewa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dkt. Harrison Mwakyembe.

Mbali ya kuitaka serikali kuharakisha kufanya uchunguzi wa taarifa hizo zilizotolewa na kiongozi mwandamizi serikalini, kisha kutoa tamko juu ya hilo, CHADEMA wamelitaka Jeshi la Polisi nchini kuhakikisha usalama wa Dkt. Slaa pamoja na viongozi wengine waliotajwa, kama ambavyo linapaswa kulinda wananchi wote.

"Kamati Kuu imepokea taarifa juu ya uamuzi wa serikali wa kuandaa muswada mpya wa Sheria ya Manunuzi...imezingatia kuwa lengo kuu la muswada huo ni kuiwezesha serikali na taasisi zake kununua bidhaa zilizotumika...hiki kitakuwa kisima cha wizi, hatutaunga mkono mabadiliko ya sheria yanayotaka kukidhi mahitaji ya watu, ikiwemo kununua mitambo chakavu.

"Tunatambua sana kuwa kuna mikataba mingi ya nishati hapa nchini tunataka yote itathminiwe...sasa hivi serikali ina mpango wa kukodi mtambo wa megawati 260 kwa takribani dola milioni 260...huu ni utapeli mkubwa...kwa nini wasinunue mitambo yetu wenyewe...wala hatutaki waingie katika biashara yoyote kinyemela na kampuni ya Dowans.

"Kwa nini mitambo hiyo isitaifishwe kwa maslahi ya umma kwa sababu iliingizwa kwa rushwa, hatuwezi kukubali biashara ya kuingia mkataba na Dowans, itumike sheria kutaifisha mitambo hiyo."

Aliongeza kuwa kwa sasa ni hatari Tanzania kutaka kujikita katika uzalishaji wa uranium, wakati haina hata sera za uvunaji wa madini hayo, akisema 'kama nchi imeshindwa hata kuhimili mitambo ya umeme na milipuko ya mabomu, itakuwaje uranium. Tuwaulize wenzetu huko Japan au Marekani sasa hivi hawalali, si kitu cha kukimbilia.

Kwa upande wake Dkt. Slaa alisema kuwa Rais Kikwete ametoa tamko kinyume na katiba ya nchi kwa kuitaka hazina ipunguze kodi katika baadhi ya maeneo, kwani hiyo ni kazi ya bunge na serikali ilipaswa kupeleka mswada bungeni ili hilo lifanyike.
 
kwa kweli sijui hii calibre ya viongozi sisiemu wanaitoa wapi????!!!!!!.... the new era DO NOT NEED AT ALL THIS TYPE OF LEADERSHIP!
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom