Yatokanayo na Kamati Kuu ya CHADEMA-Tamko Rasmi la Chama

Sehemu kubwa ya tamko "Mnaitaka Serikali..........." hayo maamuzi yanafikaje serikalini ili yatekelezwe wakati CDM siyo inaunda Serikali?

Mh. Regia naomba unijuze.
 
Sehemu kubwa ya tamko "Mnaitaka Serikali..........." hayo maamuzi yanafikaje serikalini ili yatekelezwe wakati CDM siyo inaunda Serikali?

Mh. Regia naomba unijuze.

Ndugu yangu Vincent najua umemwomba Mh. Regia akujibu. Nami naomba nichangie.
Nijuavyo mimi tamko ni kauli ya kimaandishi iliyo wazi kwa wadau mbalimbali wakiwemo serikali, vyombo vya habari, vyama vya siasa, asasi za kiraia nk. Kauli hii huweza kuchapishwa moja kwa moja (kama ilivyo) kwenye magazeti lakini pia hutawanywa kwa wadau wengine. Kwa mantiki hiyo, serikali ni mdau mkubwa wa vyama vya siasa na hivyo, naamini CDM watatumia taratibu husika za mawasiliano na serikali kufikisha tamko hilo.
 
Tuhuma nyingi zimeshatolewa dhidi ya CHADEMA,
kwanini hili linaonekana kuwagusa sana CHADEMA?

Kwa sababu tafsiri ya kauli zao ni kuonyesha mahusiano ya kijasusi kati ya CDM na balozi kutoka nje. Suala lolote linalohusisha ujasusi ni very serious na ndo maana serikali imeamua kupoza makali kwa kutumia kauli ya Membe ambaye hakutaja chama moja kwa moja kwa kusema magazeti na CDM hawakuielewa sawa sawa kauli ya waziri Membe. Hata hivyo wakasema endapo itathibitika wako tayari kuziomba radhi balozi hizo.
 
nilikuwa najaribu kufikiria kwa makini kwa nini umeandika bilioni 11 na milioni 11,000 kwa wakati mmoja nikakosa jibu, hii watalaamu wa lugha wanaita semantics redundancy.

Sijaandika mimi bali ni kutoka katika taarifa ya CHADEMA na si makosa kusema dola milioni 11,000....na hata kaka yako mkulo hutumia ''semantic redundancy'' hiyohiyo....wewe ulipohoji awali ulisema deni lataifa limetamkwa kama dola milioni 11 amabyao ni ndogo...nasikitika kuwa wewe umkososaji mbaya na msahaulifu mkubwa sana
 
nakumbuka kuna threads moja ulikuja ikiwa na kichwa cha habari kuwa 45% ya wanawake na wasichana wamepata kazi kwa kutoa rushwa ya ngono. 45% ni wengi,huenda anahusika ndo maana hajui anafanya kazi gani.
 
Kwa sababu tafsiri ya kauli zao ni kuonyesha mahusiano ya kijasusi kati ya CDM na balozi kutoka nje. Suala lolote linalohusisha ujasusi ni very serious na ndo maana serikali imeamua kupoza makali kwa kutumia kauli ya Membe ambaye hakutaja chama moja kwa moja kwa kusema magazeti na CDM hawakuielewa sawa sawa kauli ya waziri Membe. Hata hivyo wakasema endapo itathibitika wako tayari kuziomba radhi balozi hizo.

Umenena vyema. Kama sijakosea, kwa sheria za Tanzania, baada ya uhaini, kosa la kufanya ujasusi dhidi ya nchi tena kwa kushirikiana na watu wa nje, ndilo kosa la pili kwa ukubwa na adhabu yake ni kifo.

Kwa hiyo hizi kauli za wendawazimu, waropoka hovyo si za kunyamaziwa hivi hivi. Uzushi mwingine wote kama udini, ukabila, n.k. n.k. unaweza kuvumiliwa na/au kupuuzwa lakini sio suala la uhaini au ujasusi.
 
Yaani nawasikitia sana ndugu zangu Watanzania. Kama hatubadilishi chama tawala tutakufa kabisa kiuchumi. Inashangaza kuona Kikwete amethubutu kuongeza DENI LA TAIFA kwa asilimia 18 kwa mwaka mmoja!

Wengi tunasema maisha ni magumu. Lakini kama hawa wa CCM wataendelea kutawala, basi nawahakikishieni ugumu bado! Huu ni mwanzo tu!
 
Tusiongelee mate na wino upo. Nafikiri Chadema acheni mikwara.

Bi Sofi anawasubiri mahakamani.......... acheni danganya toto
 
nakubaliana na comrade moelex23, inshu ya umeya ars na kutoa siku 21 sioni mashiko sana. nguvu ya umma maana yake nn? kwn kama jamaa (ccm) waking'ang'ania hakuna njia nyingine ya kufuata kwa taratibu za kisheria? mi siwaelewi wanaposema nguvu ya umma,what do they mean? otherwise cdm nawakubali sna tu lkn kwa hili napatwa na ukakasi sioni kama limetulia

Unachekesha . Kama hujui peoples power kamuulize Gadafi na wenzake
 
Hivi huyu Mbowe na viongozi wengine wa CHADEMA wana akili sawa sawa kweli ? Waziri Mkuu , Mh. Pinda aliisha litolea Bungeni ufafanuzi vizuri na ambao uko wazi juu ya msimamo wa serikali kuwa uchaguzi wa umeya wa Arusha ulikuwa huru na halali, sasa kutoa siku 21 kwa serikali kumaliza tatizo la umeya wa arusha kuna maana gani ?. Hapa walicho takiwa kufanya ni kutoa msimamo wa chama na si kutoa kauli za muda, kwani serikali iliisha toa msimamo wake. Na hapa ndipo umakini wa viongozi wa CHADEMA unapotiliwa mashaka wa kutoa kauli badala ya mustakabali. Tuliona Mwanza walitoa siku 9, ziliisha hivi sasa tangu kauli ile zimepita siku zaidi ya 20, sasa kama kauli zisizo kuwa na vitendo ni bora zisitolewe kabisa.
 
nakubaliana na comrade moelex23, inshu ya umeya ars na kutoa siku 21 sioni mashiko sana. nguvu ya umma maana yake nn? kwn kama jamaa (ccm) waking'ang'ania hakuna njia nyingine ya kufuata kwa taratibu za kisheria? mi siwaelewi wanaposema nguvu ya umma,what do they mean? otherwise cdm nawakubali sna tu lkn kwa hili napatwa na ukakasi sioni kama limetulia

mm-bangi-nyingi!
 
Geniusbrain,,,subiri siku 21 ziishe yaani tarehe 22april utaelewa,
Kauli hizi zina maana moja tu,kuwa chadema ni chama cha amani na wanapenda amani,ndio maana tunasisitiza hatua zichukuliwe,kuhakikisha amani ya arusha inakuwepo,baada ya hapo tutapambana...
 
CDM inaonyesha hajui hawajui hata mfumo wa uchumi wa soko. Dunia nzima iko kwenye system hiyo. Serikali kushusha bei ya mahindi wakati usafirishaji unategemea mafuta ni ndoto. Biashara sasa ya sasa ni soko hurui. Infact cdm hata wakikataa wao ni wachochezi. Unampa rais siku 9 then what next.
Acheni wananchi wafanye kazi. Kampeni 2015 not now I love Tz.

Jamani tunapoandika tujaribu kufikiri.Tanzania ni Tanzania na wala haifananishwi na nchi yoyote ile kwani inakila sababu ya kutofautishwa.

Tunapoongelea uchumi tusifananishe na nchi yoyote ile duniani,kwani kila kiongozi katika nchi yake anapambana kulingana na upeo wake wa maono na kufikiri ili kuwaletea wananchi wake unafuu.

Mfano:Tanganyika hatuna mafuta,Zanzibar wanamafuta ambayo mpaka leo ni maneno tu ya siasa yanazunguka,lakini Tanganyika tunautajiri wa Gas,nakumbuka TPDF walishatengeneza system ya gari ambayo inauwezo wa kutumia gas na petrol kwa wakati tofauti lakini mpaka leo hakuna kiongozi aliliona hilo ni la msingi,wataalamu tunao hatuwatumii huoni kwa kutumia Gas tunayoivuna wenyewe ingeweza kupunguza unafuu wa maisha?

Leo kwa kuwa hatuna vongozi wenye upeo wanatuambia hata bei ya gas haiwezi kupungua kwa kuwa bei inapangwa na dunia is that the reality your own product from your own source.WanaJF huu si wakati wa kuendekeza kauli za Kisiasa zisizo na muelekeo,njia zakupunguza makali ya maisha ya Mtanzania ni nyingi sana tunamakaa ya mawe mradi unaojadiliwa kisiasa zaidi,Gas tuliyonayo hakuna Mtanzania anafaidika.
 
Tamko ni zuri, la kizarendo, ktk wakati mwafaka. Chadema wanaonesha kuwa na upeo mkubwa wa kuchambua mambo muhimu kwa taifa na wanaonesha kuwa Kamati Kuu ya CHADEMA inafanya maamuzi bora na sahihi zaidi kuliko CCM ya sasa. Hongera sana CDM. Mimi sina wivu, ni mwana CCM huru. Songeni mbele
 
Geniusbrain,,,subiri siku 21 ziishe yaani tarehe 22april utaelewa,
Kauli hizi zina maana moja tu,kuwa chadema ni chama cha amani na wanapenda amani,ndio maana tunasisitiza hatua zichukuliwe,kuhakikisha amani ya arusha inakuwepo,baada ya hapo tutapambana...

Alama moja wapo ya mtu mnafiki ni kusema asiyo yatenda, na hiki ndicho CDM wametuonyesha. Hivi unategemea kauli gani ya serikali zaidi ya aliyotoa waziri mkuu ? na aliisha sema the wayforward kwa CHADEMA ni kwenda mahakamani !
 
Hivi huyu Mbowe na viongozi wengine wa CHADEMA wana akili sawa sawa kweli ? Waziri Mkuu , Mh. Pinda aliisha litolea Bungeni ufafanuzi vizuri na ambao uko wazi juu ya msimamo wa serikali kuwa uchaguzi wa umeya wa Arusha ulikuwa huru na halali, sasa kutoa siku 21 kwa serikali kumaliza tatizo la umeya wa arusha kuna maana gani ?. Hapa walicho takiwa kufanya ni kutoa msimamo wa chama na si kutoa kauli za muda, kwani serikali iliisha toa msimamo wake. Na hapa ndipo umakini wa viongozi wa CHADEMA unapotiliwa mashaka wa kutoa kauli badala ya mustakabali. Tuliona Mwanza walitoa siku 9, ziliisha hivi sasa tangu kauli ile zimepita siku zaidi ya 20, sasa kama kauli zisizo kuwa na vitendo ni bora zisitolewe kabisa.

Geniusbrain,,,subiri siku 21 ziishe yaani tarehe 22april utaelewa,
Kauli hizi zina maana moja tu,kuwa chadema ni chama cha amani na wanapenda amani,ndio maana tunasisitiza hatua zichukuliwe,kuhakikisha amani ya arusha inakuwepo,baada ya hapo tutapambana...

Alama moja wapo ya mtu mnafiki ni kusema asiyo yatenda, na hiki ndicho CDM wametuonyesha. Hivi unategemea kauli gani ya serikali zaidi ya aliyotoa waziri mkuu ? na aliisha sema the wayforward kwa CHADEMA ni kwenda mahakamani !

I believe GeniusBrain has a very good genius brain to the extent that it is half empty. I wish it was at least half full.
Uongo wote wa waziri kule bungeni uliomfanya hata spika kujikanyagakanyaga anauita majibu? Na pia anathubutu kusema unateemea kauli gaini zaidi ya aliyotoa waziri mkuu? Nataka kuamini kwa vile serikali ya JK ni ya vilaza na wachakachuaji basi hatutegemei kauli nyingine zaidi ya hiyo. Hata hivyo CDM wametoa nafasi ya serikali kuithibitisha dhana hiyo.
 
Hivi huyu Mbowe na viongozi wengine wa CHADEMA wana akili sawa sawa kweli ? Waziri Mkuu , Mh. Pinda aliisha litolea Bungeni ufafanuzi vizuri na ambao uko wazi juu ya msimamo wa serikali kuwa uchaguzi wa umeya wa Arusha ulikuwa huru na halali, sasa kutoa siku 21 kwa serikali kumaliza tatizo la umeya wa arusha kuna maana gani ?. Hapa walicho takiwa kufanya ni kutoa msimamo wa chama na si kutoa kauli za muda, kwani serikali iliisha toa msimamo wake. Na hapa ndipo umakini wa viongozi wa CHADEMA unapotiliwa mashaka wa kutoa kauli badala ya mustakabali. Tuliona Mwanza walitoa siku 9, ziliisha hivi sasa tangu kauli ile zimepita siku zaidi ya 20, sasa kama kauli zisizo kuwa na vitendo ni bora zisitolewe kabisa.

Naomba nikwambie Viongozi wa Chadema wanaakili timamu zenye mawazo makini.Waziri mkuu tulishamwambia amelidanganya bunge na ujumbne umemfikia vizuri.

Ndani ya siku Tisa walizotoa viongozi,Kikwete ametoa matamko kadhaa katika wizara alizotembelea mf:

  1. alipokuwa katika wizara ya fedha alimuagiza waziri wa fedha kupunguza kodi katika bidhaa mbalimbali ili kumpa unafuu wa maisha.
  2. Bei ya Sukari iliyokuwa inakimbilia 2300 serikali imeamuru ibaki 1700
  3. Deni la Dowans kutolipwa na kutafuta njia mbadala.
Sasa ulitaka nini zaidi?huono AMETEKELEZA maagizo.

Lakini bado Viongozi wa chadema walisema ndani ya siku mia moja wazee waafrika mashariki malipo yao yatashughulikiwa,KIKWETE ALIAGIZA ALIP[OKUWA HAZINA KWAMBA SASA IMETOSHA WAZEE HAO WALIPWE.tena ametoa maagizo huku akijua kesi iko mahakamani.

ULIPASWA KUSEMA KAMA AHADI NA MAELEKEZO YA KIKWETE YASIPOFANYIWA KAZI VIONGOZI WA CHADEMA WATACHUKUA HATUA GANI UNGEELEWEKA.

Kuhusu Arusha usiwe na haraka subiri siku 21.Viongozi wa chadema ni watu wenye mipango thabiti na mikakati mizuri.

MISIMAMO HUWA INATOLEWA BAADA YA KUTOA MDA KWA UPANDE WA PILI.KWNI HIYO NI HAKI YA MSINGI KISHERIA.
 
Well said Josephine, Serikali miaka ya nyuma walizoea kwenda likizo mara baada ya uchaguzi, walisubiri mwaka mmoja kabla ya kipindi chao kuisha ndiyo wanarudi tena majimboni kwao kuanza kutimiza machache ambayo wananchi watayaona kwa urahisi ili kujipanga kwa uchaguzi unaofuata.

Lakini sasa hivi hilo halipo CHADEMA inawanyima usingiizi kabisa hawa waheshimiwa na ndiyo maana baada tu ya ziara ya kanda ya ziwa Mh Waziri mkuu naye anaenda kutibu majeraha.

Hii ndiyo kazi ya Chama Kikuu cha Upinzani katika nchi yeyote, on the process sisi wananchi tunafaidika, isingekuwa CHADEMA hayo yaliyosemwa na Josephine yasingetokea.

CHADEMA moto ni ule ule - serikali hakuna kwenda likizo, kama mkiamua kuyadharau / kuyapuuza madai ya CHADEMA basi hili ndilo kaburi lenu 2015.
 
CDM wakae vizuri kwani MAandamano Badala ya kuwajenga yatawabomoa Maana maisha ya watu Arusha yalipotea pamoja na lawama kwenda serikalini lakini bado CDM nayo inajukumu la kuhusika na misiba hiyo Kama wakifanya "what if" analysis
Umeya Wa Arusha sio muhimu kiasi cha kuanzisha vurugu tena eeh Mungu tunusuru
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom