Yasiyotekelezeka katika katiba mpya

jikis

Member
Aug 8, 2009
18
2
Ndugu zetu majirani wa Kenya waliamua kuandika KATIBA yao upya, na kuweka vipengele vipya, lengo lake kubwa likiwa ni kupanua DEMOKRASIA nchini mwao. Katika kufanikisha hilo waliamua kupunguza mamlaka na madaraka ya viongozi wao wakubwa kwa kuunda tume mbali mbali zitakazoshughulika na uajili wa viongozi katika idara mhimu za serikali.

Duku duku langu hapa ni mwenendo mzima wa uendeshaji na uwajibikaji wa hawa wanaofaulu interview za kuwaweka hapo. Kama mpaka IGP na Judge Mkuu wanachaguliwa katika mfumo huo, je wataweza kulinda na kutetea serikali iliyoko madarakani? Mfano IGP haivi na Raisi, je atatekeleza kwa dhati kile akisemacho raisi wake? Pili endapo huyo aliyechaguliwa (vetted) anamlengo tofauti wa kisiasa na uongozi wa juu, je hatatumia mwanya huo kujiandalia mazingira yakeya baadaye kwa kudhorotesha juhudi za serikali iliyoko madarakani?


Tatu, changamoto na vikwazo walivyonavyo wenzetu (Kenya) katika kutekeleza maadhimio ya katiba mpya si ishara ya kukurupuka katika uandikaji kwa kuweka vipengele visivyotekelezeka katika kipindi kifupi?

Je, Tanzania iko tayari kwa mabadiliko ya aina hiyo, na hawa walioko katika madaraka sasa wana utashi wa dhati wa kisiasa katika kutekeleza kile ambacho wananchi wake wanahitaji kwa sasa?

Je wote tuna muono wa pamoja katika kutekeleza maadhimio ya Ushirikiano wa Africa Mashariki, kwani katika katiba ya KENYA jambo hilo (EAST AFRICA COMMUNITY) halikupewa kipaumbele.

Naombeni maoni yenu wakuu.
 
Back
Top Bottom