Yanga yamnasa mshambuliaji wa Atletico

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=2][/h]JUMAPILI, JULAI 29, 2012 08:08 NA JENNIFER ULLEMBO

YANGA imefanikiwa kumnasa mshambaliaji wa kimataifa wa timu ya Atletico ya Burundi, Didier Kavumbagu, kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania na michuano ya Kimataifa.

Kavumbagu ni kati ya washambuliaji 10 waliong'ara katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame), iliyofikia tamati jana katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mchezo wa kwanza wa Kundi C, uliozikutanisha Yanga na Atletico, Kavumbagu alipeleka kilio Jangwani, baada ya kufunga mabao 2-0 na kufanya timu yake kuanza vizuri michuano hiyo.

Mabao hayo mawili yalimfanya mchezaji huyo kuonekana nyota wa mchezo huo, uliochezwa Julai 14, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Abdallah Bin Kleb, alithibitisha kuwepo ukweli ndani ya suala hilo.

Bin Kleb, ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya usajili ya klabu hiyo, alisema habari hizo ni za kweli na wanaendelea na mazungumza na mshambuliaji huyo ili waweze kumsajili kuitumikia klabu hiyo ya wana Jangwani.

“Tumeonyesha nia ya kumsajili Kavumbagu, kwa sasa tunaendelea na maongezi na mchezaji huyo, mazungumzo yakikamilika tutaweka hadharani,” alisema Bin Kleb.

Kabla ya kumhitaji Kavumbagu, Yanga ilikuwa na mpango wa kumsajili Medie Kagere wa Polisi ya Rwanda, lakini hadi sasa imekuwa kimya.

Kavumbagu anatarajia kuziba nafasi ya Davis Mwape, ambaye ametemwa katika usajili wa timu hiyo, kutokana na kushuka kwa kiwango.

Yanga ina nafasi mbili za wachezaji wa kimataifa, baada ya kuwatema wachezaji wake Mwape na Kenneth Assamoh, katika usajili wa msimu huu na kubakiwa na wachezaji wa kigeni, Haruna Niyonzima, Yaw Berko na Hamis Kiiza.

 
Hii ndo YANGA! hivi zinaendeleaje zile timu mbili tulizozifunga jana!!
 
Hii ndo YANGA! hivi zinaendeleaje zile timu mbili tulizozifunga jana!!

Wengi wa washabiki wamejifungia ndani, wengine wametoka alfajiri hawajarudi nyumbani.

Washabiki wa Azam waliingia na jeneza uwanjani, nani aliondoka nalo baada ya mechi?
 
Angekua kaka yao ukimpiga (simba) mapema, hua harudi uwanjani, ashakimbia mara2 half time hadi wakaitwa wamebepotea na mpera kwapani.
 
Wengi wa washabiki wamejifungia ndani, wengine wametoka alfajiri hawajarudi nyumbani.

Washabiki wa Azam waliingia na jeneza uwanjani, nani aliondoka nalo baada ya mechi?

Kuna wale wanaokaaga jukwaa lile (....) sijui hata walitoka saa ngapi?,ksbb wakati Azam wakipewa medali zao nilipotupa macho kule viti vyeupeeee!
 
Back
Top Bottom