Yanga Yamchomolea Micho Mechi Ya Kirafiki

Mbonea

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
640
20
MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Yanga wamekataa kucheza mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa Ethiopia, St George iliyopangwa kufanyika Septemba 28 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.</SPAN>

Gazeti moja la kila siku limesema kuwa, hatua hiyo imechukuliwa siku moja baada ya mabingwa hao kutangazwa kuwa watacheza na timu hiyo inayofundishwa na kocha wa zamani wa Yanga, Sredojevic Milutin 'Micho'.

Awali, ilielezwa kuwa timu kongwe ya Uganda, SC Villa pia itacheza mechi za kirafiki nchini.

Afisa Habari wa Yanga, Luis Sendeu alisema jana kuwa timu yao haiwezi kubadili ratiba ya Ligi Kuu na inatarajia kwenda mkoani Kagera Septemba 25 au 26 kwa ajili ya mechi dhidi ya Kagera Sugar.

Alisema kuwa wamepania kufanya vizuri katika mechi hiyo na ndiyo maana wameamua kwenda huko mapema na itakuwa vigumu kwao kuondoka Dar es Salaam Septemba 29 baada ya mechi hiyo dhidi ya Wahabeshi.

"Kiufundi imeonekana haijakaa vizuri kusafiri siku hiyo kwani Dar es Salaam hadi Kagera kupitia Mwanza ni takribani siku mbili au tatu endapo tutasafiri bila matatizo.

"Tumewapa taarifa waandaaji wa mechi hiyo kuhusiana na maamuzi hayo ikiwa pamoja na masharti endapo watataka tucheze," alieleza.

Pamoja na kutotaja masharti hayo, imebainika kuwa Yanga inahitaji shilingi milioni 20 ili icheze mechi hiyo ambazo zitatumika kwa usafiri wa ndege kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza na baadaye kwa meli hadi Bukoba mkoani Kagera.

Yanga ina pointi nane na inashikilia nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi wa timu 12.


</SPAN>
 
Back
Top Bottom