Yanga yalizwa na Kagera sukari

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Jun 22, 2011
4,225
869
MABINGWA wa Afrika Mashariki na kati Dar Young Afrika jana kwa mara pili tena walionja joto katika michuano ya ligi kuu ya VodacomTanzania Bara,baada ya kufungwa na Kagera Sugar ya Mkoani Hapa bao 1-0 katikamchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Kaitaba.

Hata hivyo mchezo huo ulikosa ladha kutokana na timu zotekucheza chini ya kiwango kinyume na matarajio ya mashabiki aliokuwa wamefurikakenye uwanja huo,huku wacheaji wa pandezote mbili wakionekana kukamia zaidi na hivyo kujikuta wakichezeana rafu mbaya kila wakati.

Yanga ndio waliokuwa wa kwanza kulisakama lango la Kagerasugar kupitia kwa washambuliaji wake Said Bahanuz na Kavumbagu,lakini hatahivyo mashuti yao katika ya pili na tano yalitoka nje ya lango.

Kagera walijibu mashambulizi hayo katika dakika ya 7 na 8 kupitia kwa wachezaji wake Enyina Darlinghton na Daud Jumanne, hata hivyo nao mashambulizi yao hayakulenga lango vizuri.

Kagera waliendelea kulishmbulia lango la Yanga kwa takribanidakika 20,hayta hivyo washambuliaji wake hawakuwa makinin katika kulilenga lanola Yanga lililokuwa likilindwa na kipa wa Yanga Yaw Berko ambapo ama mashutiyao yalitoka nje ya lango ama kudakwa na kipa wa Yanga.

Yanga ilipata pigo katika dakika ya 21 kipindi cha kwanzabada ya mshambuliaji wake Tegemeo Said Bahanuz kuumia na kutolewa nje na nafasiyake kuchukuliwa na Jerson Tegete, Bahanuz aliumia baada ya kugongana na Mchezaji wa wa kagera Sugar Amandus Nesta.
Hata hivyo Yanga ambayo ilionekana kama vile kuisoma kageraSugar katika dakika zipatazo 35 za kipindi cha kwanza ilizinduka katika dakika ya 37 na kufanyashambulizi kali langoni mwa Kagera,ambapo mchezaji Tegete akiwa yeye na KipaAndre Ntale alipiga kichwa na kupaa juu ya lango.

Dakika ya 44 Tegete tena akiwa anamtazama kipa wa KageraSugar alijikuta akipiga shuti kali na kupaa juu ya lango na kushindwa kuiandikia timu yake bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza,Tegete alipenyezewa pasi afi na Kavumbagu.

Hat hivyo nafasi ambayo Yanga walijilaumu ni ile aliyoipatafrank Domayo katika dakika ya 45 ambapo akiwa nje kidogo ya eneo la hatrialijikuta akipiga mpira na kutoka nje kidogo ya lango la kagera huku kipa waKagera Sugar akiwa ameanguka baada ya kuokoa mpira uliopigwa na Kavumbagu.

Kwa ujumla kipindi cha kwanza chote timu zote mbilihikuonyesha mchezo mzuri ambapo si yanga wala kagera Sugar ambao walionekanakucheza mpira mzuri.

Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ambapo Yangailimtoa nizar Khalfan na nafasi yake kuchukuliwa na Shamte Ally,wakti ambapoKagera Sugar walimtoa Enyinnah Darlinghton na nafasi yake kuchukuliwa na Temi Felex.

Mabadiliko hayo yalionekana kuleta uhai kwa timu zote mbiliambapo zilianza kucheza mpira wa kuonana zaidi,hata hivyo Kagera ndiowalionekan kunufaika zaidi baada ya kujipatia bao katika dakika 67 mfungajiakiwa ni Temi Felex ambaye alikuwa na dakika 10 tu tngu kuingia uwanjanikuchukua nafasi ya Enyinnah.

Felex alifunga bao hilo kwa shuti kali akiwa nje ya 18 baadaya makosa yaliyofanywa na kipa wa yanga Berko ambaye aliudk mpira na kuutemakatika eneo la hatari kabla ya kuokolewa na Mwasika na kisha kutua kwenye mguuwa mfungaji ambaye alifumua shuti kali na kutinga ndani ya nyavu na kuihesabiatimu yake bao hilo.

Baada ya mchezo huo Kagera Sugar walishindwa kucheza mpiraambapo wachezaji wake ama walikuwa wakipiga mipira nje kwa ajili ya kupotezamuda ama kujiangusha chini ndani ya uwanja, ambapo hadi mwisho wa mchezo huo Kagera waliibuka na ushindi wa bao hilo moja.

Katika mchezo wa jana timu zote mbili hazikuweza kucheza. mchezo mzuri na hasa kwa upande wa Yanga ambao muda mwingi walionekana kushambuliwa zaidi na kuonesha kama vile wachezaji walikuwa wamechoka, ingawa hata Kagera sugar nao hawakuonyesha mchezo mzuri.

Baada ya mchezo huo kocha wa kagera Sugar Mlage Kabange alisema pamoja na ushindi huo lakini wachezaji wake hawakuonyesha mchezo mzuri alioutarajia, lakini akawapongea wachezaji wake kwa kubakiza pointi zote tatu muhimu.

Kabange aliwatetea wachezaji wake kwamba huenda walikumbwa na kihoro kutokana na kila upande kumkamia mwenzake, hali iliyowafanya wachezaji wake kuchukua muda mrefu kuuzoea mchezo.

Katika hatua nyingine watu wanaodaiwa kuwa ni mashabiki wayanga jana walisikika wakiwatukana na kuwalaumu wachezaji wa Yanga baada ya kufungwa mchezo huo, huku wengine wakiporomosha matusi makali kwa washambuliaji Kavumbagu, Tegete pamoja na mabeki Canavaro na Twite kwa kuonyesha mchezo mbovu.
 
hii ni breaking news kabisa. Ngoja niongee na Invisible abadilishe title pale juu
 
Last edited by a moderator:
Sukari tamu kuliko mahindi ya msaada hahahah yale ya njano

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
lakini mleta mada mbona kafungwa leo au siku kikwenu huwa inaisha saa moja..yote kwayote iliyofungwa ni yanga Bile yanga kubwa ya akina twite, kelvin, Canavaro,kavumbagu,niyonzima,kiiza haiwezi kufungwa na kagera, ikumbukwe ina ukuta wa chuma..hahahahaha
 
lakini mleta mada mbona kafungwa leo au siku kikwenu huwa inaisha saa moja..yote kwayote iliyofungwa ni yanga Bile yanga kubwa ya akina twite, kelvin, Canavaro,kavumbagu,niyonzima,kiiza haiwezi kufungwa na kagera, ikumbukwe ina ukuta wa chuma..hahahahaha
si unajua sisi wasabato jua likizama tunaanza siku mpya!!!
 
Bojo!. Yanga katai na magezi. Juzi wameokolewa na kosa la beki oooh Yanga... Inaukuta wa chuma... Haha haha ukuta wa mabua
 
Aibu kwa ITV, Gamba aliaga kuwa mwisho wa habari za michezo bila ya kutangaza matokeo hadi Gondwe alipochomekea vipi huko Bukoba? Kwa taabu Gamba akasema mzee kashughulikiwa kapigwa moja kisha akaaga bila kueleza nani ametufurahisha, ilikuwa dakika ya ngapi na katika mazingira yapi.

ITV inakwenda kubaya sijui kwanini.
 
Yanga vs Mtibwa SUKARI. Yanga vs Kagera SUKARI. Je Yanga vs LAMBALAMBA? Kama rahisi kubashiri vile mana vitamu huwalevya...?
 
Back
Top Bottom