Yanga yabamizwa Bukoba

nilkuwa shahidi uwanja wa kaitaba bukoba, mpira ulitawaliwa na vituko vingi:-.

1. Tbl (kilimanjaro bia) kutandaza mabango ya matangazo kuzunguka uwanja jambo ambalo kagera sugar walipinga kata kata na kudai katika uwanja wao ni vodacom tu anayetambulika kama mdhamini, hivyo mabango hayo kuondolewa kwa nguvu na uongozi wa kagera sugar baada ya tff mkoa kugwaya na kushindwa kutoa uamuzi hasa baada ya mwakalebela (tff hq) kuwatishia kuwachukulia hatua iwapo watayatoa. Je, tbl ni wadhamini wa premier ligi?
2. Kitendo cha watu ambao walionekana baadaye kuwa ni viongozi wa yanga kugombea mapokezi ya refa uwanja wa ndege (bukoba) na wale waliokuja baadaye kuonekana ni watu wa simba (friends of simba) kinatia shaka mwenendo mzima wa kukua kwa soka nchini. Kilikuwa ni kituko cha aina yake kwani upande mmja ulifanikiwa kupokea mizigo na upande wa pili kumshikilia refa ambapo simba walifanikiwa kuondoka naye. (nisijue kama ilisaidia kwenye matokeo)
3.nipasho ya mashabiki wa kagera sugar kwa yanga kabla ya mechi kuwa walizoea kununua magoli na kuonga wachezaji wa timu pinzani jambo ambalo walisema kwamba hapo wamekwama na wategemee kipigo.
4. Kitendo cha kagera sugar kumpeleka nahodha wao michael katende kwenye pre match meeting na ukaguzi wa awali uwanjani na baadaye kutomchezesha kwa kumweka bench kama sub. Kiliwaumiza vichwa yanga (habari za ndani za yanga) kwani kilitibua mikakati ya ushindi wao!!!!!
5. Mashabiki kumzomea juma kaseja aliyekuwa anamuomba kocha kutoka baada ya kufungwa goli la pili na kuimba nyimbo za kumsifu maximo kwa uamuzi wake wa kutomchagua timu ya taifa hasa kutokana na kufungwa goli la kwanza mpira uliopigwa toka mbali na kushindwa kuuokoa kutokana na ufupi.
6. Vitendo vya ubabe vya wachezaji wa yanga (idd - chuji) kupigana na mashabiki jukwaani baada ya mechi.

i wish i were there!!!!!!!!!!!!!!!
 
Halafu wewe inaelekea ni SIMBA!maana the way ulivyoweka heading ya thread yako!mimi nilishtuka nikafikiri Simba wamepeta kumbe yale yale tu!Tuambie basi na mechi ya SIMBA VS Azam ilikuwaje?

First Lady, mimi ukinikata damu itakayotoka si nyekundu bali ya kijani. Sasa niambie je mimi ni simba au Y***a?
 
Back
Top Bottom