Yanga watatoka kweli kwa simba....?

Technically Simba ni wazuri kuliko Yanga. Na hii ni kutokana na ukweli kwamba Simba wana mwalimu mzuri zaidi ukilinganisha na Yanga. Kuhusu nani atashinda katika mchezo wao ni vigumu kutabiri kwani mechi zinazohusisha timu hizi mbili huwa hazitabiriki. Simba nzuri inaweza kufungwa na Yanga mbovu and vice versa. Mnakumbuka mwaka ule Simba ilipokuwa mbovu kabisa ikikaribia kushuka daraja lakini ikaifunga Yanga na kuikosesha ubingwa. Nina uhakika kikosi hiki cha sasa cha Yanga kingekuwa kinafundishwa na kocha wa sasa wa Simba (Patrick Phiri) kingefanya wonders.
Lakini tatizo lingine kubwa la Yanga ni kukimbilia kusajili wachezaji wengi wa kigeni bila sababu. Safari hii imesajili wachezaji 11 wa kigeni, tena wengine kwenye position ambazo tayari zina wachezaji wazuri wa hapa nyumbani. Kanuni zinaruhusu wachezaji watano tu wa kigeni kupangwa katika mchezo mmoja wa ligi. This means ma-pro sita wanakuwa nje kabisa ya uwanja kila mechi.
Utabiri wangu ni kwamba iwapo Yanga wataendelea kuwa na kocha huyu wa sasa, watakapokutana na Simba watarajie kunywa mabao mengi kwani mpaka kufikia wakati huo Simba watakuwa wameiva zaidi. Ingawa kama nilivyosema hapo juu, mechi za timu hizi mbili huwa hazitabiriki....
****************************************************

Ukweli bwana Simba wamejipanga vizuri na wamesajili wachezaji wazuri mwaka huu, na kama alivyosema mdau hapo juu wanayo one of the best coach in Africa in Patrick Phiri..Nilipata bahati kuongea nae baada ya kutolewa Zamia la time kwan kombe la Africa..Ni mtulivu na anajua Soka kweli kweli..Naona ataleta mafanio sana mwaka huu..Aliwesesha Simba Kutwaa ubingwa mara mbili alipokuwa mao miaka nnee zilizopita..Yanaga bwana hawafundishiki na mastaa players kutoka njee hawana kitu..watachapwa tuu na kila timu watayokutana nayo..

Ila kinachotakiwa ni kuangalia kama viongozi hawataingilia na timu,kama tunavyojua soka ya bongo imejaa ubabe,mara leo makomandoo, mara sijui vibopa, mfadhili...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom