Yanga watatoka kweli kwa simba....?

Mbonea

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
640
20
Kwa style ya jana wadau Yanga waliioionesha, je watatoka kwa Simba?
 
Kikosi cha Yanga mwaka huu ni kibovu mno, na hili ndiyo tatizo la kung'ang'ania wachezaji kibao wa nje ambao hawana uwezo kuwazidi wazalendo wetu.

Nadhani usajili wa Simba ni bora mwaka huu na Yanga isipokuwa makini inaweza kuvuna Aibu. naomba hilo lisitokee
 
Wana yanga wenzangu msiwe na shaka juu ya timu yetu,ipo mbioni kumnyakua Messi ktk kipindi cha dirisha dogo la usajili ili kuongeza makali,pia chama tawala kimeahidi ku deal na marefa,kama kilivyoanza nao jana ule ni mwanzo tuu,tu tegemee penat nyingi sana msimu huu,Simba wachovu hawana hela!!!!
 
Kaka Mchajikobe umetoa kali sana...eti mtasajili Messi...hahahhaahah..kubali hamna kitu mwaka huu kwenu...Siyo Simba tuu timu zote mtakutana nayo watawatesa tuu...usijifariji kaka kwamba mtapata penalti kila mechi....Hela hakuna mwaka huu..Manji hataki kuwajua kabisa..mnaboa tuu..Nani kakuambia Simba hela hawana...Hela wanayo nyingi tuu ila hawataki kuonyesha..wanafanya mambo kwa ukimya...
 
msijidanganye, yanga ni timu nzuri, Ligi ndio kwanza inaanza ndio kwanza mechi ya nne tu, simba msijidanganye kwa kushinda hivyo vimechi mfululizo ligi bado sana ndugu zangu mpaka mzunguko wa kwanza uishe ndipo unaweza kusema lolote, yanga hiaja badilika sana, wachezaji wakali bado wapo na wazoefu kama ngasa,chuji,tegete,nsajigwa,na wengine kwahiyo yanga bado ni nzuri na wanao uwezo wa kutetea ubingwa, mpira sio simba na yanga tu ila ligi kwa ujumla. simba mnacheza ili kuikamia yanga lakini kombe wanabeba wengine hiyo ni akili au matope. simba ni nguvu ya soda tu, tuone leo kwa kagera sugar kama mtavuna nini.
 
aisee, haya na tusubiri tuone

Wana kocha mzungu na golikipa manyoya mzungu. Nasikia huyu golikipa alikuja mtaalam wa mabomba enzi za DAWASA. Lowasa alipowatimua DAWASA jamaa akaamua ajaribu bahati yake Yanga na jamaa wa kandambili wakamind rangi. Sasa watajuuuuuta kumwacha Tanzania One Kaseja.

Nasisitiza: Simba 4 Yanga 0
 
Ndugu zangu Kanda2 msimu huu ubingwa tushaukosa na kocha anasubiri tufungwe game ya Simba afukuzwe
 
Nimesikia tetesi kuwa MANJI kajiondoa kuifadhili Yanga
 
Nimesikia tetesi kuwa MANJI kajiondoa kuifadhili Yanga

Siyo tetesi mkuu. Hilo liko wazi. Kocha katolewa New Africa sasa anaishi uswazi. Wachezaji wanapiga miayo kwenye mgofu wao Jangwani.... Unafanya mchezo na wafadhili wetu. Wanafadhili timu kwa malengo fulani, wasipoyapata wanaingia mitini. Poleni watani, ndoa yetu itadumishwa tena mwaka huu.

Habari ni hii. Wekundu 4 Kandambili O
 
Technically Simba ni wazuri kuliko Yanga. Na hii ni kutokana na ukweli kwamba Simba wana mwalimu mzuri zaidi ukilinganisha na Yanga. Kuhusu nani atashinda katika mchezo wao ni vigumu kutabiri kwani mechi zinazohusisha timu hizi mbili huwa hazitabiriki. Simba nzuri inaweza kufungwa na Yanga mbovu and vice versa. Mnakumbuka mwaka ule Simba ilipokuwa mbovu kabisa ikikaribia kushuka daraja lakini ikaifunga Yanga na kuikosesha ubingwa. Nina uhakika kikosi hiki cha sasa cha Yanga kingekuwa kinafundishwa na kocha wa sasa wa Simba (Patrick Phiri) kingefanya wonders.
Lakini tatizo lingine kubwa la Yanga ni kukimbilia kusajili wachezaji wengi wa kigeni bila sababu. Safari hii imesajili wachezaji 11 wa kigeni, tena wengine kwenye position ambazo tayari zina wachezaji wazuri wa hapa nyumbani. Kanuni zinaruhusu wachezaji watano tu wa kigeni kupangwa katika mchezo mmoja wa ligi. This means ma-pro sita wanakuwa nje kabisa ya uwanja kila mechi.
Utabiri wangu ni kwamba iwapo Yanga wataendelea kuwa na kocha huyu wa sasa, watakapokutana na Simba watarajie kunywa mabao mengi kwani mpaka kufikia wakati huo Simba watakuwa wameiva zaidi. Ingawa kama nilivyosema hapo juu, mechi za timu hizi mbili huwa hazitabiriki....
 
Hawataki kujifunza ya REAL MADRID. Nyota kibao lakini wanakandamizwa! Yanga = Real Madrid , Simba = Barcelona
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom