Yanga vs Mtibwa/Simba vs JKT Ruvu - Sept 19, 2012 (Updates)

Kama namuona doris maliyaga wa mwanaspoti anavyosonya.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
mhhhh i kanti bilivu zis.... Yaani kerere zooote kumbe timu ya wizi wa hela za EPA na ufisadi, ya jamaa ambaye juzi juzi kahonga wabunge HAMUNA KITU...??
Na yule bloga wa kujikomba-komba, OHHH REKODI ZA MTAKATIFU KUIFUNGA TIMU YA ZANAKI, mara ohh mtakatifu sijui nini kumbe kweli kagame mlinunua...!!!! Sasa huyo Mbuyu Twetwe amerudi kwao au ..?? Kudadek soka uwanjani sio ktk magazeti na blogu za waandishi njaa..............!!!!!!!!!!!!!!
Wakati wa Kagame baada ya Mbuyu Twite kusababisha magoli ya utata tulisema hela ya EPA imeingia hadi kwenye jeshi la Rwanda wakatutukana lakini ukweli utabaki Kagame mechi nyingi tu walihonga.
 
Mkuu sawa, lakini tutaongozwa na historia mpaka lini, tunahitaji ushindi na siyo kufuata historia, tambo za viongozi wetu, magazeti nayo yalivyopamba timu yetu na mbwembwe za kocha wetu, sikutegemea tupate kipigo kama hiki, ama wachezaji wetu wamechoka safari ndefu? Inatia uchungu sana, kumbuka tukifungwaga , huwa tunafungwa mfululizo mpaka kuzinduka, naogopa hili, nadhani imefikia wakati tusicheze magazetini, maana inaafanya timu pinzani kujiandaa. Kumbuka ni 3-0 , inatia uchungu sana

yap ni ukweli tatizo la soka la bongo ukiwa bingwa unajiachia na kujiamiamin
 
Ninachoendelea kugundua hawa Jamaa zetu wa mtaa wa 2 kumbe wana mashabiki wengi sana.
 



MANJI AWAKA 3-0 ZA MTIBWA, TIMU KUFIKIA KITI MOTO DAR

5.jpg

Viongozi wa Yanga, kushoto Mussa Katabaro na Seif Ahmad 'Magari' wakiwa taaban Uwanja wa Jamhuri jana

KIPIGO cha mabao 3-0 ambacho Yanga imechapwa na wenyeji Mtibwa Sugar ya Turiani, Morogoro kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini hapa jana, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kimemkasirisha Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Mehboob Manji amefoka mno.
Chanzo chetu cha habari kutoka Yanga leo, kimesema kwamba Manji alipiga simu kuulizia matokeo na kufoka sana baada ya kuambiwa timu imefungwa mabao 3-0. "Manji amekasirika sana, alipiga simu, alipoambiwa timu imefungwa akafoka sana,"kilisema chanzo chetu kutoka Yanga jana.
Viongozi wa Yanga walioambatana na timu hapa mjini hapa, akiwemo Seif Ahmad ‘Magari' na Mussa Katabaro walisikitishwa na hali hiyo na hawakuwa tayari kusema chochote.

Lakini habari za ndani zinasema hali hiyo imeanza kuwashangaza hata makocha na wachezaji, kwa sababu timu yao ilikuwa vizuri na ghafla inaanza kubadilika.
Yanga itarejea Dar es Salaam leo kuanza maandalizi ya mchezo wao ujao, dhidi ya JKT Ruvu Jumamosi, lakini kabla ya hapo kutakuwa na kikao kikali juu ya mwenedo wa timu katika mechi mbili za mwanzo.
Katika mchezo wa kwanza ambao Yanga ililazimishwa sare ya bila kufungana na Prisons mjini Mbeya, kocha Mbelgiji wa klabu hiyo alilalamikia malazi mabovu katika hoteli waliyofikishiwa, lakini jana alisema malazi yalikuwa mazuri na wachezaji walikuwa vizuri kabla ya mechi.
Labda ni Uwanja mbovu, hiyo ni sababu iliyobakia, lakini mechi ijayo Yanga itacheza kwenye Uwanja mzuri wa Taifa, Dar es Salaam waliouzoea dhidi ya JKT ambayo jana ilipigwa 2-0 na Simba pungufu.
Mambo mawili yanatazamwa kwa sasa, moja mfumo wa kucheza kwa kujihami zaidi na pili kujiamini kupita kiasi, labda yanaweza kuwa yanachangia matokeo mabaya. Wachezaji wa Yanga kwa sasa wanaonekana ‘kujisikia' mno baada ya matokeo mazuri ya awali, ikiwemo kutwaa Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame na hawachezi kwa kujituma kama mwanzo.
Kuhusu mfumo, hakuna kilichobadilika sana Yanga, bado ni ule ule wa kutumia mabeki watupu wingi ya kushoto, ambao uliwapa Kombe la Kagame, labda tatizo la ‘kujisikia' kwa wachezaji na kudharau timu pinzani linaweza kuwa la msingi katika suala hili.
Katika mchezo wa jana, Yanga ilizidiwa mno na hadi mapumziko, tayari Mtibwa Sugar walikuwa mbele kwa mabao 2-0, yaliyotiwa kimiani na beki wa kati, Dickson Daudi dakika ya 11 akiunganisha kwa kichwa kona ya beki wa kushoto Malika Ndeule.
Bao hilo lilitokana na uzembe wa mabeki wa Yanga ambao walishindwa kumuweka ulinzi mchezaji mrefu kuliko wote, Daudi.
Yanga walijaribu kutaka kusawazisha, lakini mipango yao haikuwa na tija na kujikuta wakiendelea kushambuliwa na dakika ya 43, Hussein Javu aliwainua tena vitini mashabiki wa Simba waliokuwa wakiwashangilia kwa nguvu leo kwa kufunga bao la pili.
Kwa ujumla kipindi cha kwanza, Yanga walicheza ovyo- pasi zao nyingi zilikuwa hazifiki, walishindwa kuwabana wapinzani wao na zaidi Haruna Niyonzima alishindwa kuiongoza vema timu, jambo ambalo lilifamnya kiungo mkabaji Athumani Iddi ‘Chuji' kupanda mbele zaidi kusaidia, ingawa haikusaidia.
Mabeki wawili wa kati wa Mtibwa, Daudi na Salvatory Ntebe waliwadhibiti vema washambuliaji wawili wa Yanga, Hamisi Kiiza na Saidi Bahamnuzi katika dakika 45 za kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili, Kocha wa Yanga, Mbelgiji Tom Saintfiet alianza kwa mabadiliko akiwatoa Frank Damayo na David Luhende na kuwaingiza Simon Msuva na Stefano na Mwasyika, lakini bado ukuta wa Mtibwa ulikuwa mgumu mbele ya Watoto wa Jangwani.
Katika kuongeza mashambulizi, Mtakatifu Tom alimtoa beki Mbuyu Twite na kumuingiza na mshambuliaji Didier Kavumbangu, lakini bado mambo yaliendelea kuwa magumu kwa Yanga.
Dakika ya 86 Hussein Javu aliifungia Mtibwa bao la tatu kwa shuti la mbali, wakitoka kushambuliwa na kufikia hapo, Yanga ‘walikufa' na mashabiki wao wakaanza kuuacha Uwanja wa Jamhuri.
Huu unakuwa mchezo wa pili kwa Yanga tangu kuanza kwa ligi wakiwasononesha mashabiki wao, baada ya mechi ya kwanza kulazimishwa sare ya bila kufungana na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Waswahili wanasema siku ya kufa nyani, miti yote huteleza, Hamisi Kiiza alipaisha mkwaju wa penalti dakika ya 89, baada ya Daudi kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.

KWA HISANI YA http://bongostaz.blogspot.com/

 
Yebo Yebo safari hii msijidanganye, timu zote Ligi Kuu ni nzuri sana msidhani hizi point mnazopoteza sasa mtakuja kuzi-recover kirahisi. Mna timu dhaifu sana! Nimetoka Jamhuri Stadium sasa hivi. Barthez amepigwa bao la umbali wa mita 40! Huyo Twite hamna kitu kabisa; alikuwa njia ya mkato mpaka kocha akalazimika kumtoa. Msikimbilie kusajili wachezaji kutoka nje na kutumia pesa kibao. Wachezaji wapo hapa hapa Bongo. "Ohh tumewapiga bao Simba kwa kumtwaa Twite." Kiko wapi sasa?
hIVI YANGA WAMECHEZA MECHI NGAPI NA KUFUNGWA NGAPI???

SIMBA WAZURI MECHI ZA NDANI TATIZO LAO LINAKUJA KWENYE MASHINDANO YA KIMATAIFA KAMA KAGAME NA MENGINE YANAWASHINDA SANA
 
hIVI YANGA WAMECHEZA MECHI NGAPI NA KUFUNGWA NGAPI???

SIMBA WAZURI MECHI ZA NDANI TATIZO LAO LINAKUJA KWENYE MASHINDANO YA KIMATAIFA KAMA KAGAME NA MENGINE YANAWASHINDA SANA

Lazima utakuwa mgeni sana. Umekuja mjini lini ndugu yangu? Mwaka 2010 yanga alitolewa round ya kwanza na al ahly, mwaka uliofuata dedebit walipiga pasi za kufa mtu taifa pale ball possession ilikuwa 98 kwa 2. Umesahau? Mwaka jana zamalek kawakalisha mapema. Una la kuongea?? Rekodi za simba wewe tafuta mwenyewe nakupa assignment. Hata kagame nani anaongoza kwa kuchukua mara nyingi east n central africa yote. Siku njema!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
hIVI YANGA WAMECHEZA MECHI NGAPI NA KUFUNGWA NGAPI???

SIMBA WAZURI MECHI ZA NDANI TATIZO LAO LINAKUJA KWENYE MASHINDANO YA KIMATAIFA KAMA KAGAME NA MENGINE YANAWASHINDA SANA

Hilo kombe la Kagame linatofauti gani na kombe la "mbuzi"
 
hIVI YANGA WAMECHEZA MECHI NGAPI NA KUFUNGWA NGAPI???

SIMBA WAZURI MECHI ZA NDANI TATIZO LAO LINAKUJA KWENYE MASHINDANO YA KIMATAIFA KAMA KAGAME NA MENGINE YANAWASHINDA SANA
Mkuu mie ni Yanga, ila naomba nitofautiane nawe katika hili, ujue sisi tambo zetu zipo hapa tu East Africa, nakumbuka tushachukua ubingwa kule Nakivubo tukiwa na wachezaji watatu tuliosajili kutoka watani zetu. Ukiacha kanda hii ya Mashariki, huwa hatufurukuti kwingineko, sisemi kwamba watani zetu wameshachukua ubingwa nje ya kanda ahii lakini wameshafanya makubwa ambayo sisi hata robo yake hatufikii katika mashindano ya Kimataifa. Tatizo letu tunacheza magazetini, haapo juu kuna uchambuzi mzuri sana, lakini kama kujisikia wachezaji kutokana na ubora wa timz na kuwa na miundo mbinu basi AZAM ndiyo ifanye hivyo, sisi wachezaji wetu wajisikie katika lipi? usajili?mishahara? kiwanja cha Kaunda? uongozi? ama kuwa na wazee waa klabu wenye misimamo?Naogopa kipigo kingine kinafuata, fuatilia historia yetu, utaona huwa tunafungwa mfurulizo, kwasasa tujielewe, ligi ndiyo imeanzaa, tuachane na tambo zisizo na tija.
 
Mkuu mie ni Yanga, ila naomba nitofautiane nawe katika hili, ujue sisi tambo zetu zipo hapa tu East Africa, nakumbuka tushachukua ubingwa kule Nakivubo tukiwa na wachezaji watatu tuliosajili kutoka watani zetu. Ukiacha kanda hii ya Mashariki, huwa hatufurukuti kwingineko, sisemi kwamba watani zetu wameshachukua ubingwa nje ya kanda ahii lakini wameshafanya makubwa ambayo sisi hata robo yake hatufikii katika mashindano ya Kimataifa. Tatizo letu tunacheza magazetini, haapo juu kuna uchambuzi mzuri sana, lakini kama kujisikia wachezaji kutokana na ubora wa timz na kuwa na miundo mbinu basi AZAM ndiyo ifanye hivyo, sisi wachezaji wetu wajisikie katika lipi? usajili?mishahara? kiwanja cha Kaunda? uongozi? ama kuwa na wazee waa klabu wenye misimamo?Naogopa kipigo kingine kinafuata, fuatilia historia yetu, utaona huwa tunafungwa mfurulizo, kwasasa tujielewe, ligi ndiyo imeanzaa, tuachane na tambo zisizo na tija.

Ni washabiki wachache sana wanaoweza kuwaeleza wenzao kile wasichopenda kukisikia. Wewe wenye Yanga yao wakikufahamu utalijua jiji. Big up sana

Ni vzr wapinzani wa timu hizi waache ujinga, badala yake wajifunze facts kwamba Yanga ni bingwa wa kihistoria wa Tanzania Bara na Simba ni bingwa wa kihistoria wa Africa Mashariki na Kati, na kwamba Simba dnio timu iliyofanya vizuri zaidi kimataifa so far kuliko timu zote za tanzania na kwamba Yanga ndio timu pekee kuchukua ubingwa wa Africa Mashariki nje ya nchi. Mbona facts ziko wazi tu.
 
Back
Top Bottom