Yanga Mdebwedo tena!

Masatu

JF-Expert Member
Jan 29, 2007
3,276
125
Matokeo ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania, ni Yanga ( Al-maaruf Kandambili) wamefungwa 1-0 na Maafande wa polisi Morogoro.

Kandambili ambao wana udhoefu mkubwa wa kufungwa tokea kuanza kwa ligi mwaka huu ambapo hii itakuwa ni mara yao ya 3 kufungwa kwa dose 1-0, kabla ya hapo walifungwa na wauza mitumba wa Ilala Ashanti 1-0 kabla ya kupata dhahma ya wana kimanumanu Coastal Union ya Tanga na kufungwa pia 1-0 na hii gharika iliwaangukia leo kwa polisi moro 1-0.

Tunachukua nafasi hii kuwapa pole kandambili wote wa JF michezo ipo mingi sio lazima soka hata karata pia mchezo jaribuni bahati yenu huko.

Kwa upande mwingine wale wafalme wa kulisakata kabumbu Tanzania Mnyama a.k.a wekundu wa msimbazi Simba Sports Club wametoka sare na Manyema katika mchezo uliotawaliwa na wana wa msimbazi kwa takriban dakika zote 90 lakini bahati haikuwa upande wao.
 
Yaani ulivyo stress hiyo tittle ya Simba utafikiri wameshinda vile. Simba na Yanga wote midebwedo tu. Kufungwa na kutoa sare kote ni kumoja tu....tofauti ni kapoint kamoja tu!

Ushindi wa timu nyingine ni ishara la kukuwa kwa soka letu. Kwa hiyo bila ya shaka tunapiga hatua mbele...
 
Yani unaripoti vizuri tena kwa madoido kama Maulid wa Kitenge :)

You really made my day buddy! Japo ni Simba lakini kufagilia kwa namna hii kungenipiga chenga mkuu...

Raha ya utani wa jadi ni kuwepo wachokozi kama ninyi
 
Yaani ulivyo stress hiyo tittle ya Simba utafikiri wameshinda vile. Simba na Yanga wote midebwedo tu. Kufungwa na kutoa sare kote ni kumoja tu....tofauti ni kapoint kamoja tu!

Ushindi wa timu nyingine ni ishara la kukuwa kwa soka letu. Kwa hiyo bila ya shaka tunapiga hatua mbele...

Something is better than nothing...
 
Masatu,
Naona kuna zimwi la mkosi kwa Simba na haswa Yanga mwaka huu!
Inabidi sijui WanaYanga tukatambike!!!! Au pengine ni mkosi wa mda tu! Au huko nyuma hizi timu zilikuwa zinabebwa sasa ni fair game?
 
Nafikiri wachezaji wa timu nyingine wamepata changamoto ya kutaka kuchezea timu ya Taifa. Hile chupu chupu ya kutaka kufanikiwa kuingia African Nation imewapa mushkeli wachezaji wa timu nyingine. Halafu na ile support kuanzia mshiko mpaka uzalendo lazima itakuwa imezaja morali wachezaji wengi kujituma. Nafikiri kila mchezaji ana moyo wa kuchaguliwa kwenye Taifa Stars sasa hivi. Kwa hiyo tutegemee ligi yenye ushindani mwaka huu.
 
Masatu,
Naona kuna zimwi la mkosi kwa Simba na haswa Yanga mwaka huu!
Inabidi sijui WanaYanga tukatambike!!!! Au pengine ni mkosi wa mda tu! Au huko nyuma hizi timu zilikuwa zinabebwa sasa ni fair game?

Hakuna mkosi wala nini Mzalendo, u-mbumbu wa viogozi hususan wa Yanga ndiko kunakopelekea viwango kushuka kwa timu zetu.

Mimi nadhani wakati umefika Tanzania tukawa na soka kulipwa ( kwa maana ya muswada upitishwe bungeni) na hawa the so called makomando waondolewe ktk vilabu timu ziongozwe ktk mifumo kama ya Ulaya ambapo mwanachama unabaki na kadi yako tu sio kauli ya kuweka na kuondoa viongozi.

By the way chama kubwa kama Simba kuongozwa na Hassan Dalali (Mpiga rythim wa vijana jazz wa zamani) ni disaster waiting to happen....
 
Wale wafalme wa kulisakata "Mdundiko" Tanzania Mnyama a.k.a wekundu wa msimbazi Simba Sports Club wamefunyukwa leo 1-0 na Prisons ya Mbeya

Tunachukua nafasi hii kuwapa pole wanamdundiko wote wa JF. Michezo ipo mingi sio lazima soka hata karata pia mchezo jaribuni bahati yenu huko. Masatu eat your words....

Admin tafadhali badilisha kichwa cha habari kuwa "Simba na Yanga wote midebwedo"
 
Mwaka huu prison inakamua kisawasawa. hongera zao maana tumeshachoka na Simba na yanga kila siku.
 
Back
Top Bottom