Yanga kumtuza atakayebuni ramani Kaunda

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
na Juma Kasesa

UONGOZI wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga, umeandaa tuzo maalumu kwa wasanifu majengo wazawa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kitengo cha ardhi ambaye atafanikiwa kuchora ramani nzuri ya uwanja wao wa Kaunda na jengo la kitega uchumi la Mafia ambako atakabidhiwa na Rais Jakaya Kikwete.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mjumbe wa Kamati ya Uendelezaji Rasilimali za Yanga, Seif Mohamed, alisema wanatarajia kutangaza shindano hilo kwa wasanifu majengo wa chuo hicho, ili kutoa changamoto ya kupata ramani ya kisasa ya vitega uchumi hivyo ambapo mshindi huyo atakadhiwa tuzo siku ya Harambee ya kuchangia ujenzi wa majengo hayo Julai 7 mwaka huu katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es Salaam na Rais Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Alisema, wanaamini kupitia ushindani huo, wasanifu hao wataweza kushindana kwa kila mmoja kuonyesha kipaji chake ambapo kutakuwa na jopo maalumu la wachambuzi wa ramani hizo ili kumteua mshindi.
Aidha, Mohamed alisema katika kujindaa na harambee hiyo, kamati yake juzi iliendesha semina kwa makatibu na wenyeviti wa matawi wa Yanga, ili kuwapa mwongozo wanachama na wapenzi wa klabu hiyo namna watakavyoweza kushiriki kuchangia ujenzi huo.
Alisema, kila mwanachama na mpenzi wa Yanga, atapewa akaunti maalumu ambayo ataweza kuingiza kiasi cha fedha anachomudu ili kufanikisha harambee hiyo ambayo itaongozwa na Rais Kikwete. “Huwezi kusubiri kuchangiwa ikiwa wewe mwenyewe hujajiandaa, ni vyema tukawapa semina wanachama wetu ili nao kama wadau wakubwa wakaweza kushiriki bila kupata usumbufu,” alisema Mohamed.
 
Safi sana! washirikishe hata wasanifu majengo walionje ya nchi

Yanga Imara
 
na Juma Kasesa

UONGOZI wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga, umeandaa tuzo maalumu kwa wasanifu majengo wazawa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kitengo cha ardhi ambaye atafanikiwa kuchora ramani nzuri ya uwanja wao wa Kaunda na jengo la kitega uchumi la Mafia ambako atakabidhiwa na Rais Jakaya Kikwete.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mjumbe wa Kamati ya Uendelezaji Rasilimali za Yanga, Seif Mohamed, alisema wanatarajia kutangaza shindano hilo kwa wasanifu majengo wa chuo hicho, ili kutoa changamoto ya kupata ramani ya kisasa ya vitega uchumi hivyo ambapo mshindi huyo atakadhiwa tuzo siku ya Harambee ya kuchangia ujenzi wa majengo hayo Julai 7 mwaka huu katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es Salaam na Rais Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Alisema, wanaamini kupitia ushindani huo, wasanifu hao wataweza kushindana kwa kila mmoja kuonyesha kipaji chake ambapo kutakuwa na jopo maalumu la wachambuzi wa ramani hizo ili kumteua mshindi.
Aidha, Mohamed alisema katika kujindaa na harambee hiyo, kamati yake juzi iliendesha semina kwa makatibu na wenyeviti wa matawi wa Yanga, ili kuwapa mwongozo wanachama na wapenzi wa klabu hiyo namna watakavyoweza kushiriki kuchangia ujenzi huo.
Alisema, kila mwanachama na mpenzi wa Yanga, atapewa akaunti maalumu ambayo ataweza kuingiza kiasi cha fedha anachomudu ili kufanikisha harambee hiyo ambayo itaongozwa na Rais Kikwete. "Huwezi kusubiri kuchangiwa ikiwa wewe mwenyewe hujajiandaa, ni vyema tukawapa semina wanachama wetu ili nao kama wadau wakubwa wakaweza kushiriki bila kupata usumbufu," alisema Mohamed.

hapo kwenye red umekosea...... chuo kikuu cha dar es salaaam hikitoi wasanifu majengo hao watu wanapatikana ardhi university
 
Back
Top Bottom