Yanga inacheza DSM na Zamalekh, TBC wanaonyesha Bongfleva!

commonmwananchi

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,377
1,952
wananchi na wana JF kwa ujumla

Kuna mechi muhimu sana inaendelea katika uwanja wa taifa jijini dar es salaam na mpaka sasa yanga iko mbele kwa bao moja bila.hii ni mechi ya kutafuta klabu bingwa afrika.

Cha ajabu kituo chetu cha television ya walipa kodi tanzania,TBC wao wanaonyesha vipindi vya bongofleva, je haya ni matumizi halali ya chombo hiki cha umma?

Wenzao wa KBC wa jirani zetu kenya wao timu ya ulinzi kenya iko uwanjani ikimenyana na karuturi na wanaonyesha LIVE kupitia super sport.

Nina imani ingekuwa ni tukio la ccm basi tungeonyeshwa live.sasa kwa mtindo huu ndoto za taifa hili kusonga mbele kisoka zitatimia?????
 
wameona ni bora kutuburudisha kwa masongi kuliko kutuletea mastress.

Ni kweli italeleta stress mkuu,lakini Clouds Tv wanaonyesha mechi wameshirikiana na Channel ten so unaweza kuiona.Japo hakuna jipya hapo unaweza kujiharibia weekend yako bure!
 
Nimekubali kwamba ni stress kuangalia hii mechi,kutokana na madudu ninayoshuhudia yanga wakiyafanya,na tayari wamisri wameisha sawazisha na wanapelekwa puta sasa.na yanga wameshindwa kutumia nafasi nyingi walizozipata.
 
TBC hakuna kitu toka long tym tu.....timu ya taifa ikicheza hawaonyeshi, ndio itakuwa yanga!
 
Leo saubuhi Marine Hassan alikuwa akiimiza uzalendo.....
Uzalendo upi Watanzania kukosa mechi hii kupitia Chombo chao cha hbr cha taifa?
Ila ingekuwa maadhimisho ya CCM wangekuwepo live
Hii ndio Tanzania ya kulalamika bila kujua mchawi wetu nani.................
 
Ilikuwa tbc enzi za Tido, I wish wangebadili jina waondoe hiyo T ya mwanzo kwani haiendani na utaifa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom