Yanga Bingwa!!

MzalendoHalisi

JF-Expert Member
Jun 24, 2007
4,514
1,360
Yanga leo imepata Ubingwa wa Premier- Tanzania baada ya kuichapa Toto Africa Mwanza 2-1!

Wamefikisha point 46 ikiwa bado mechi 5 mkononi!

Simba Mko Hapo???

Yanga!! Yanga!!! yanga!!!

Wanayanga mpo???
 
Last edited:
Kwa Tanzania hatujambo ila tukikutana na mafarao wa Misri mmmmhhh...Hongera Taifa stairs hongera Yanga
 
Hongereni sana wana Yamga kwa kuchukua ubingwa huu mapema kabla hata ligi haijaisha,hongereni sana
 
Mlinda mlango Kaseja afunga bao la mwaka

Paulina David, Mwanza


BAO la mwaka la kipa Juma Kaseja lilitosha kuweka historia mpya kwa kuipa Yanga ubingwa wa 22 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza huku Azam ikiichapa 6-2 Villa Squad jijini Dar es Salaam.


Yanga iliyokuwa ikihitaji pointi tatu ili kutangazwa mabingwa kwa msimu wa 2008/'09, iliandika bao lake la kwanza katika dakika ya 21 lililofungwa na Kaseja aliyetumia vizuri udhaifu wa mwenzake, Abdallah Msafiri wa Toto Africa na kuachia mkwaju ambao ulidunda na kutinga nyavuni.


Awali, Kaseja alidaka na kupiga mpira mrefu wa juu uliokwenda moja kwa moja wavuni, dakika tisa baadaye Hussein Sued aliisawazishia Toto Afrika kabla ya Mike Baraza kufunga bao la pili na ushindi kwa mabingwa hao.


Katika mchezo huo ulioshuhudia timu hizo zikikosa penalti kila moja, mshambuliaji Mkenya Mike Baraza wa Yanga alikosa penalti dakika ya 18 kipindi cha kwanza, naye Said Dilunga alipoteza nafasi ya pekee ya kuisawazishia Toto wakati mkwaju wake wa penalti ulipoishia mkononi mwa Kaseja, dakika ya 62.


Naye Sweetbert Lukonge anaripoti kutoka Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuwa jahazi la Villa Squad limezidi kuzama baada ya kukubali kipigo cha mabao 6-2 kutoka kwa Azam FC.


Mshambuliaji Nsa Job ndiye aliyekuwa mwiba mkali kwa ngome ya Villa kwa kupachika mabao matano peke yake na kuzawadiwa mpira akimwachia mchezaji wa kimataifa wa Uganda, Danny Wagaluka akihitimisha karamu hiyo ya mabao kwa bao la sita.


Katika mchezo huo uliokuwa na raha ya aina yake, ulishuhudia mabao manne yakifungwa ndani ya dakika nane za mchezo huo, Azam ilipata mabao kupitia kwa Nsa Job, dakika ya 16 na 25 wakati Villa walisawazisha kupitia kwa Juhudi Samwel (19) na Lewede Dayton (24),kipindi cha kwanza na kufanya matokeo kuwa 2-2 hadi mapumziko.


Kipindi cha pili kilikuwa kibaya zaidi kwa Villa baada ya Nsa Job kufunga bao la tatu, nne na sita katika dakika ya 51,74 na 88, huku Mganda Wagaluka akipachika bao la tano (85).


Katika kile kilichoonekana kama kuchanganyikiwa na kipigo, mchezaji wa Villa , Launt Bagia alikosa penalti mwisho mwa mchezo, dakika ya 90 iliyopanguliwa na kipa wa Azam, Vladimir Niyonkuru.


Kutoka Mbeya, Brandy Nelson anaripoti kuwa mvua kubwa iliyokuwa inanyesha mjini humo ilisababisha mwamuzi Dominick Nyamsana kutoka Dodoma kuusimamisha mchezo huo katika dakika ya 28.


Mchezo huo baina ya Prisons na Kagera Sugar ulikuwa ukichezwa kwenye Uwanja wa Sokoine mjini hapa huku zikiwa zimefungana bao 1-1.


Akizungumzia kuahirishwa kwa mechi hiyo mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoani Mbeya, Festo Nkemwa alisema mvua kubwa iliyojaza maji uwanjani ndiyo sababu ya kuahirishwa kwake.


Nkemwa alisema mvua hiyo ilisababisha wachezaji wa timu hizo kuanguka na kuweza kuhatarisha afya zao.


Naye mwamuzi Nyamsana alisema hadi uamuzi huo ulifikiwa kutokana na hali ya uwanja kutofaa tena kwa mchezo huo.


Mabao hayo, Prisons yalifungwa na Shaban Mtupa dakika ya nne, Haruna Hassan wa Kagera akasawazisha, dakika ya 18.
Source: Gazeti la Mwananchi
 
Hongera yanga ila mkivuka mpaka tu..kichapo mpaka lini?basi mjipange klabu bingwamwakani msogee hata robo fainalinaamini hamtaangukia misrim...
 
Haya shangilieni tu maana furaha ya NYANI inakaribia kufika Jangwani...na hapo ndo kilio na machozi kitawafika wanayanga.hongereni kandambili
 
Yeboyebo hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee, mnyama kaliwaaaaaaa mwaka huuuuu, wacha wivu mnyama kwani kazi yako ni kuliwaaaaaaaaaa
 
Safi sana Yanga, kwa kuweka rekodi mpya katika soka la TZ kwa kuwa bingwa mara 22!

Simba na midomo yao mikubwa wamechukua ubingwa wa Tz mara 16 tu!
 
Awali, Kaseja alidaka na kupiga mpira mrefu wa juu uliokwenda moja kwa moja wavuni, dakika tisa baadaye Hussein Sued aliisawazishia Toto Afrika kabla ya Mike Baraza kufunga bao la pili na ushindi kwa mabingwa hao.

Source: Gazeti la Mwananchi

Hongereni Yanga. Ila hili goli ninatia shaka (kama la kifisadi vile), hasa timu ndugu zinapocheza.
 
Last edited:
Wandugu,
Masatu tuko wapi? na mzee mzima PM wafikishieni hizi salaam na waambieni watufikishie salaa m na pole nyingi kwa KAPUYA na DALALI
 
- Yanga oyeee! saafi sana, lakini timu yangu ni Manyema FC, ila Yanga ni watoto wa nyumbani pia, tuko pamoja wapenzi wa Yanga na Liverpool!

Respect!

FMES!
 
Jamani mtupe update za maandalizi ya kuwavaa Wamisri, wengine tunasikia tuu Yanga bingwa, mara Yanga kachapwa tatu, sasa sijui inakuwaje.
 
Jamani mtupe update za maandalizi ya kuwavaa Wamisri, wengine tunasikia tuu Yanga bingwa, mara Yanga kachapwa tatu, sasa sijui inakuwaje.

Kwa wamisri andika maumivu kama nawe ni Yeboyebo, pale mnaondolewa tu, hata Kocha wenu alishajikatia tamaa, sasa morali ya wachezaji itatoka wapi?.
 
Mie natoa hongera nyingi kwa watoto wa Jangwani, timu ya Yanga (taifa Stars) kwa ubingwa huu ...

Hivi kumbe Yanga ndo Taifa stars? Nadhani ndio maana ilitolewa mapema kule Ivory Coast kwenye CHAN !! Duuh, halafu nilishasahau, kumbe Wamisri watakuja tena!! Hawa watavuruga furaha ya ubingwwa, kama vile mnyama alivyovuruga sherehe za ubingwa wa Zamalek katika ligi yao mwaka 2003.
 
Kidume ndani ukitoka nje mdebwedo!Baba ndani ukitoka nje kama mama vile!Any way hongereni Yanga!
 
Kidume ndani ukitoka nje mdebwedo!Baba ndani ukitoka nje kama mama vile!Any way hongereni Yanga!

Mhh, TAMWA wakikusikia wewe...!!! Kwa nini isiwe hivi: Mama ndani ukitoka nje kama baba vile.
 
Goli la Kaseja linanikumbusha Paul Robinson alipokuwa Spurs alimfunga kipa mwenzie Ben Forster
Hongera vijana wa Jangwani,poleni sana watani wetu msipoangalia hata nafasi ya 2 hampati
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom