Yanayotokea Kenya Leo, Tanzania Kesho

kinetiq01

Member
Aug 25, 2006
49
0
Mahatma Ghandi, yule mwana falsafa hodari wa India, aliwahi kusema maneno haya; "The earth has enough for man’s need but not for man’s greed".Walioko madarakani katika nchi yetu nzuri, wanasukumwa na tamaa na ulafi unaowafanya wajikaange kwa mafuta yao.

Kama mlivyo wana JF wengi, ninafuatilia kwa karibu sana yanayotokea katika nchi jirani ya Kenya.Hili si jambo la kupuuza eti kwasababu siyo katika ardhi ya Tanzania.The point is, we should not take peace and stability that we currently assume to have for granted, nor should our leaders take our compliance and obedience for granted.

I'm not trying to be an alarmist, but what's happening in Kenya, has been swept under the carpet since after Independence, but now it's up in the open for the world to see.Kusiwe na kundi moja linafaidi kupita kiasi, na kundi la pili linapata shida kupita maelezo.

Mahitaji yetu yanapuuzwa

Haiwezekani jiji la kibiashara kama Dar Es Salaam kukosa huduma ya maji ya bomba mwaka 2008, wakati mjinga mmoja anaidhinisha wizi wa mabilioni ya fedha kwa kisingizio cha kuhakikisha CCM inasinda uchaguzi mkuu.Benjamin William Mkapa atakumbukwa kuwa rais fisadi kuliko wote waliowahi kuiongoza Tanzania.


Hivi kweli mnaamini kwamba pamoja na kashfa za IPTL, SONGAS, NET SOLUTIONS, RICHMOND na TANPOWER RESOURCES, Tanzania bado haijitoshelezi kwa zaidi ya asilimia 10 [kumi] ya mahitaji yake ya umeme?

It's no secret that many Tanzanians are suffering internally, and have been suffering for quite a considerable amount time; we don't know for how long they'll keep their heads down.Lakini one thing is for sure, they'll one day revolt and the oppressors will have to duck for cover - I'm no Prophet, but that day is getting closer.


Machafuko
Mwaka 1994 ilikuwa Rwanda, Somalia imekuwa vitani tangu mwaka 1991.Ukiangalia Uganda na Burundi, pia wamekuwa wakipigana.Na katika siku za karibuni kumekuwa na mapigano Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kama unajua ramani ya Afrika Mashariki na Kati, maelezo yangu hapo juu yatakupa ishara kwamba ni Tanzania pekee ambayo imeweza kusalimika machafuko ya ndani ya nchi - yawe ya kikabila au kisiasa.

Baada ya picha hiyo, jiulize kwa mwendo huu tunaokwenda nao, wa CCM na walafi wachache, itachukua muda gani kabla na sisi Tanzania hatujaingia machafukoni?Kuna baadhi ya wenzetu ukisema hivyo, watakwambia wewe ni mchochezi.Lakini ukweli wa mambo ni kwamba, tunaelekea kubaya.

Hii serikali ya chama kimoja, ambayo tangu mwaka 1977, ukiweka kando miaka ya TANU - inatumia vibaya fursa iliyonayo [Monopoly abuse].Kuna puppets wachache ambao wakialikwa kula pilau wanaridhika na kusaliti wenzao ambao hata maji ya kunywa hawapati, siku ikifika msilaumu mtu.

Hivi Kikwete na wajuba wenzake wanategemea tutaendelea kuwa na utulivu walioukuta kwa ukandamizaji wanaoutekeleza kwa dharau na kiburi cha hali ya juu?

Tamaa na ulafi

Hebu angalieni, wizi wa kishetani wa mali ya wananchi unavyowarudisha nyuma watanzania.Mabilioni ya shilingi yanachotwa na watu ambao hawastahili kuiba.

Miradi ya kifirauni inaletwa kila siku kuchezea fedha ya Tanzania, orodhesha miradi ya kifisadi, kisha ongeza ile ambayo CCM inalazimisha itekelezwe, utagundua kwamba hatuna viongozi, si KIKWETE wala wabunge wetu ambao kila wanachoambiwa wanakubali.

Kwa jinsi viongozi walivyo na tamaa ya utajiri usiokuwa na maana, naamini kabisa, kwamba baadhi yao wanaweza kuuza hata wake zao, ili mradi waahidiwe dola.Na mwelekeo upo wazi kwamba wakishauza wake zao, hata wao wenyewe wanaweza kuvua suruali zao, ili mradi watalipwa chochote waendeshe magari ya kifahari na kuishi kwenye makasri.

TAMAA, ULAFI NA UBINAFSI vinasababishwa na katiba mbovu.Jambo ambalo serikali inapinga lisifanyiwe marekebisho, lakini siku mkong'oto ukianza ndiyo watakumbuka yanayosemwa sasa.

Kwa maelfu ya miaka, kuliwahi kuwa na watawala hodari sana wa Uigiriki, Urumi, Misri na kwingineko, hawapo sasa.Ukijua ni kwanini hawapo, basi CCM standby, GRAVITATIONAL FORCE OF THE WILL OF TANZANIANS WILL CONDEMN YOU TO THE BINS OF POLITICS.

If these people at JF are venting their anger through keyboards, one day they'll do it in real life, real time.Mafisadi you got plenty of time to change the situation, do some good things for your people they'll help you to lead better.
 
Tatizo letu watanzania inapokuja kupigwa risasi wote tunajisweka ndani, kwa hiyo tutafanana na wakenya kwa kuibiana kura lakini sio kwa kupigana risasi, nani atoke nje, mbongo, thubutu yako!
 
Hamna Kitu Kama Hicho Kwa Tanzania Hata Muende Kwa Waganga Hamna. Tanzania Ni Amani Tuuu. Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki Jf.
 
..yaliyotokea kenya hayawezi tokea tanzania,at least tanganyika,labda zanzibar.

..hata hivyo jamii ya watanzania haijagawanyika kama ya wakenya,at least kikabila!

..sasa,labda kama tunapenda kufikiria kwamba yatatokea huku. haitokuwa hivyo,at least for sometime.
 
..yaliyotokea kenya hayawezi tokea tanzania,at least tanganyika,labda zanzibar.

..hata hivyo jamii ya watanzania haijagawanyika kama ya wakenya,at least kikabila!

..sasa,labda kama tunapenda kufikiria kwamba yatatokea huku. haitokuwa hivyo,at least for sometime.

Lakini sisi tunawazidi kuiba kura, wao wanaiba hadi wanakamatana, yaani hata kuiba hawajui.
 
Hamna Kitu Kama Hicho Kwa Tanzania Hata Muende Kwa Waganga Hamna. Tanzania Ni Amani Tuuu. Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki Jf.

..kuna watu wanapenda kuona kunatibuka hapa. hivi wamejiuliza kuwa wao watajisitiri wapi? wanajua kwamba watashindwa kuwazika hata wapendwa wao? au washazoea kuwa wakimbizi?
 
..kuna watu wanapenda kuona kunatibuka hapa. hivi wamejiuliza kuwa wao watajisitiri wapi? wanajua kwamba watashindwa kuwazika hata wapendwa wao? au washazoea kuwa wakimbizi?
Hayo unayosema tayari yanatokea.Kwa umasikini uliokithiri, kunaa watu wanakosa hata fedha ya kukomboa miili ya ndugu zao wanapofia hospitalini.

Tanzania hakuna ukabila kama Kenya, lakini kumbuka kwamba kuna mambo mengine yanayotugawa kama dini, umasikini na utajiri - lakini pia katika swala la ukabila kumbuka kwama kuna makabila makubwa kama wasukuma, wahaya, wanyakyusa na wachaga ambao wanaweza kutumika vibaya kuigawa nchi.

Unajua Kenya hawakuanza kubaguana eti kwa sababu wajaluo hawatahiriwi, kilichosababisha ni mgao mbaya wa rasilimali kama ardhi - kwa kasi hii ya CCM na Kikwete baada ya muda si mrefu tutakuwa kama Kenya.Wachaga wamechukua ardhi ya wagogo au waluguru.....subiri uone moto wake.
 
Back
Top Bottom