Yanayojiri mkutano wa NCCR - Disemba 17, 2011

Status
Not open for further replies.
Mbatia sio mpinzani wa kweli amezoea maisha ya kupatiwa sio kujitafutia. Hivyo kwake hongo ni halali wala hajaanza leo ni kigeugeu sie tunamfahamu tangu shuleni Kilimanjaro boys. Tunayo mengi yanayomhusu, anachangia kuivuruga upinzani kwasababu ya tamaa yake. Akina Mkosamali ilitakiwa watafute chama cha kujiunga nacho tangu mwaka 2009 hata ivyo hawajachelewa wanaweza kuhama hata sasa kwani. Kwa nccr hawataweza kufanya chochote watazidi kuitwa ccm B kwa sababu ya mwenyekiti wao. Na wao wanapendwa kwa sababu ya ubunge (Ruzuku) bila ubunge sudhani kama wangekuwepo nccr. Kafulila kufanya kosa si kosa baya ni kurudia kosa tafuta chama makini hata ikibidi kawaombe ndg zako msamaha. Ili msameane na kuendeleza ndoto zako za kisiasa. Ndani ya nccr mtakuwa na ugomvi kila siku na mwishowe watakuchomekea kitu ambacho utakisahau. Mbatia anahongwa ili avuruge upinzani na hilo linajulikana na hata Mvungi nae yumo kwenye io list. Mjiangalie mko wapi msichelewe bado mapema yani ndio tumemaliza mwka mmoja tu.
 
Siasa ni mchezo mchafu ambao kila nikifikiria naumia sana moyoni kama leo asubuhi tumesikia kwenye vyombo vya habari kuwa kiongozi wa nchi yetu amewateua wale waliokuwa mawaziri ambao walishindwa kwenye ubunge mwaka 2010 kama vile Dk.Batilda Buriani,Philip Marmo,Deodoras Kamala na wengine aliowateua kipindi cha nyuma kidogo kama vile Basil Mramba na wengine akawapa ukuu wa mikoa kama vile Joel Bendera,Mwantumu Mahiza na wengineo,hivi uongozi ni kuwa CCM au ni kuwa na uwezo wa kuongoza?mbona kiongozi wetu anawabeba watu wake kwa sababu tu ni CCM?haoni kama anataka kusababisha maandamano kama yale ya Misri,Libya na nyinginezo?jamani wana Jamii Forum naombeni mnisaidie kwa hili.

Si mwelewi kabisa huyu rais ina maana wengine wamezaliwa kuwa viongozi tu katika maisha yao yani hakuna kuwa labda hateuliwe mwenye uwezo ambaaye hata hajulikani. Kweli hapa utasema vijana watapata ajira Tanzania. Kama viongozi ni wale wale tangu tukiwa vidudu, Kingunge, Msekwa, Makinda, na wengine wengi katika serikali ya Tanzania wazee wamezidi inabidi waachie ngazi yani wawe washauri mnachagua makamu wa rais mwenye umri wa miaka mia, mtafikiri vijana hawapo. Kweli Tanzania ni la wenyewe na ndio maana wako tayari kufa kwa ajili ya kulinda katiba ya sasa kwani wanajua kwa katiba mpya wengi watafungwa. Wezi ni wengi katika ccm na serikali yake. Ni wakati wa vijana nao kupata nafasi katika serikali ili iwe changamoto kwa wanaokuja na hata walio mitaani. Ukiangalia safu nzima ya uongozi kwa ccm na serikali yake wazee ni wengi mno na wako katika kulinda maslai yao na familia zao.
 
Kusema kweli mimi nijuavyo chama hakiwezi kumnyang'anya mtu uanachama kwa sababu hiyo ni imani ya mtu kiitikadi na huwezi kuiondoa kwa kumfukuza uanachama unless mtu huyo amekiuka kabisa hata miiko ya kiitikadi...Ila chama kinaweza kumwondoa mtu ktk madaraka na akabakia mwanachama ambaye anaweza kutokuwa na imani na viongozi lakini bado anaamini itikadi ya chama ndio njia pekee ya kuwaletea wananchi maendeleo. Kafulila kutokuwa na imani na viongozi wake ama viongozi wake kutokuwa na imani naye kiuongozi haiondoi kabisa ukweli kwamba yeye ni muumini wa mrengo wa chama.

Hivyo sijui siasa vizuri lakini sijasikia mtu akifukuzwa uanachama kwa sababu za kiofisi, ila najua watu hufukuzwa uongozi kisha wao ndio huamua kukihama chama kuondokana na itikadi ile kwa sababu aidha -Chama kimepoteza mwelekeo wa kiitikadi ama yeye mwenyewe haamini tena ktk itikadi hiyo. Chama siku zote hakina mwenyewe sii cha Mbatia, Mbowe, Mrema wala JK na pia sii cha NEC wala Kamati kuu isipokuwa wanaweza kufanya maamuzi yanayowahusu viongozi na wajumbe wake.

Well nipo katika kujifunza maana sidhani kama kuna mtu anawezxa kunyang'anywa imani ya Ukristu au Uislaam wake ila anaweza kuzuiwa kufanya ibada ktk msikiti au kanisa hilo na still mtu huyo akasalia nyumbani kwake...
 
Tatizo vyama vyetu havina itikadi. Kwa mfano itikadi ya chama cha NCCR- Mageuzi ni ipi?
 
hayo yalikuwa mawazo yangu ninavyo ona mkutano huo! ninaweza nikawa sahihi au ninaweza nikawa siko sahihi, lakini all in all huo ndio mtazamo wangu!

Mawazo mazuri. Utabiri wako haujawa mbali sana na yaliyojiri kwenye mkutano wa NCCR-Mageuzi. Mi nadhani wengine wote waliofukuzwa kama wanataka wanaweza kukaribishwa CHADEMA lkn nachelea kusema kuwa huyu Kafulila pengine si mtu wa kurudi CHADEMA maana ameacha mdomo wazi sana.

Kama CDM itaamua kumsamehe na kumrejesha basi huo mdomo wake ununuliwe chupi maana ni mtu anajiona yeye ni bora sana.
 
Tatizo vyama vyetu havina itikadi. Kwa mfano itikadi ya chama cha NCCR- Mageuzi ni ipi?
Mkuu wangu zamani nilipoingia ktk siasa za Bongo nilikuta kitu kama hiki lakini sijui kama bado iko hivyo ila najua CDM wamehama mrengo..

1. CCM - Left - wing authoritarian
2. Chadema - Conservative
3. CUF - Liberal
4.NCCR -MAGEUZI - Centrist
5.UDP - Liberal Center -Left
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom