Leo ni siku ambayo mh. Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete anatarajia kulihutubia bunge maalumu la katiba. Hotuba yake inakuja baada ya kutanguliwa na hotuba mbili zilizotolewa na; Jaji mstaafu Warioba ambae alitoa hotuba ya maoni ya wananchi juu ya rasimu ya katiba mpya akiwa kama mwenyekiti wa tume hiyo na Amosi Wako ambae ni seneta kule nchini kenya msomi aliyebobea kwenye sheria aliyepata mafunzo hayo chuo kikuu cha dar es salaam (UDSM) kuanzia miaka ya 1969 na pia ni mwanasheria mstaafu wa serikali ya kenya kama alivyo Andrew Chenge wa Tanzania. Alitoa presentation iliyohusu katiba ya kenya namna ilivyopatikana na changamoto walizokumbana nazo. Pia wajumbe 16 wa bunge maalumu la katiba waliweza kumwuliza jumla ya maswali 48, akiwepo mzee Kingunge ambae swali lake lilivuta hisia za wajumbe wengi, na maswali yote yalijibiwa. Je leo ni nini kitajiri? Usikose kufuatilia hapo jioni saa kumi kupitia media mbalimbali nchini tanzania kama tv,radio na mitandao ya kijamii kama hii.
=====
Fuatilia hapa live
https://www.jamiiforums.com/katiba-...-hotuba-ya-rais-uzinduzi-wa-bunge-maalum.html
=====
Fuatilia hapa live
https://www.jamiiforums.com/katiba-...-hotuba-ya-rais-uzinduzi-wa-bunge-maalum.html