Yanayojiri Bunge la Katiba leo tarehe 5 Machi, 2014

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,353
Habari wanaJF,

Kama tunavyojua kuwa leo tarehe 5/03/2014 kikao cha Bunge la Katiba kinaendelea,itakuwa ni vyema tukiwa tunajulishana hapa jamvini ili kuweza kusaidia wadau wengine ambao hawana uwezo wa kuangalia moja kwa moja kwenye tv wajue kinachoendelea katika bunge la katiba.

Karibuni cha michango yenu.
 
Kikao cha bunge ni hadi mida ya saa 10 jioni. Asubuhi kamati ya kanuni inapitia kanuni ya 31 hadi ya 35 ili kufanya marekebisho.
 
Daata mkuu sina access na tv wala redio ndiyo maana nikakimbilia huku, kama unajua kinachojiri tupe updates mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Lissu ni mjumbe wa kamati iliyoandaa kanuni za uendeshaji wa Bunge maalumu chini ya Profesa Mahalu. Nimekuwa nikifuatilia mijadala ya semina imayoendelea sasa na nimevutiwa sana na uwezo wake Mhe Lissu katika kutoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali.
mwenyekiti wa kamati hiyo Pro. Mahalu amekuwa mara nyingi akimtumia Lissu kutoa ufafanuzi juu ya hoja nyingi za wajumbe na Lissu amekuwa akijibu bila bila jaziba,uchama,wala hasira. Tena kwa ufafanuzi wa kina.
Nimejiuliza kama hata mawaziri wetu wangekuwa nao wanatumia style hiyo katika Bunge letu jee kungekuwa na migongano? Hii imeonyesha kuwa kumbe hawa tunaoita wapinzani wanao uwezo mkubwa sana wa kuendesha shughuli za serikali tofauti na wengi wanavyodhani.
 
Lissu amejewa na uzalendo na shule yake haina mashaka . Anasema mawazo yake na anacho kiamini wengine wanasema wanayo tumwa na kusema kwa maslahi fulani ndiyo tofauti ya Lissu hiyo .
 
Wakili Msomi sana Tundu A.M.Lissu ana uelewa mkubwa sana. Ni mtu makini na mwerevu. Ni tunu ya Taifa. Huisaidia Serikali kwa namna moja au nyingine anapohitajika.Hata sisi wa CCM tunajua hilo

Mzee Tupatupa
 
Lissu ni msomi aliyeelimika zamani nilifikiri ni madaktari tuu hutumia elimu yao vizuri kumbe hata sheria inawezekana
 
Tundu ni jembe sana.Tuombee tu yale "mashetani" ya Ufipa yasituharibie jembe letu maana wameshaanza!!
 
Lissu amejewa na uzalendo na shule yake haina mashaka . Anasema mawazo yake na anacho kiamini wengine wanasema wanayo tumwa na kusema kwa maslahi fulani ndiyo tofauti ya Lissu hiyo .
Mkuu Lunyungu,kwa hakika AG Werema angekuwa walao anatenda hata nusu tuu ya anayoyafanya Lissu sasa hivi kwa kweli ndani ya Bunge letu kungekuwa na maelewano na Bunge lingeonekana lina heshima na sura ya kitaifa. Bahati mbaya yeye kama ulivyosema ananena kwa maslahi ya aliyemtuma sio kwa weledi wa kazi yake.
 
Last edited by a moderator:
Lissu ni mjumbe wa kamati iliyoandaa kanuni za uendeshaji wa Bunge maalumu chini ya Profesa Mahalu. Nimekuwa nikifuatilia mijadala ya semina imayoendelea sasa na nimevutiwa sana na uwezo wake Mhe Lissu katika kutoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali.
mwenyekiti wa kamati hiyo Pro. Mahalu amekuwa mara nyingi akimtumia Lissu kutoa ufafanuzi juu ya hoja nyingi za wajumbe na Lissu amekuwa akijibu bila bila jaziba,uchama,wala hasira. Tena kwa ufafanuzi wa kina.
Nimejiuliza kama hata mawaziri wetu wangekuwa nao wanatumia style hiyo katika Bunge letu jee kungekuwa na migongano? Hii imeonyesha kuwa kumbe hawa tunaoita wapinzani wanao uwezo mkubwa sana wa kuendesha shughuli za serikali tofauti na wengi wanavyodhani.

Kichwa cha Lisu Kiko vizuri sana. Anastahili kushika Nafasi ya Werema.
 
Hapa utawadanganya misukule wenzio, So far, sijaona uwezo wala uzalendo wa Lissu, yule ni mropokaji tu kama CHADEMA wengine.
 
Ktk bunge hili kuna majembe ya uhakika kuliko hata Lissu, sema lisu kwa kuwa amepata fursa ya kuomgea mara kwa mara. Lkn ktk bunge hili kuna wajuzi na weledi walio bobea sana subiri vikao vya kujadili rasimu ya katiba kiianze
 
Tumekuzoea wewe! Hoja huna ila una huba iliyopitiliza kwa CCM. Hufatilii hata hayo majadiliano huko Bungeni maana usingesema hivyo. Wenzako walioko huko wametamka kuwa wanakubaliana naye katika fafanuzi nyingi anazotoa ila wewe kwa vile unalipwa ili upinge basi hata ukiambiwa pinga wewe sio MSALANI basi utapinga tuu. Pole
 
Last edited by a moderator:
Huh? Leo ni jembe na kichwa lakini majuzi tu hapa mlimponda baada ya hakimu kuamua kwa upande wa Zitto....

Wabongo bana!
 
Ktk bunge hili kuna majembe ya uhakika kuliko hata Lissu, sema lisu kwa kuwa amepata fursa ya kuomgea mara kwa mara. Lkn ktk bunge hili kuna wajuzi na weledi walio bobea sana subiri vikao vya kujadili rasimu ya katiba kiianze

Wivu wa kike!
 
Lissu ni mjumbe wa kamati iliyoandaa kanuni za uendeshaji wa Bunge maalumu chini ya Profesa Mahalu. Nimekuwa nikifuatilia mijadala ya semina imayoendelea sasa na nimevutiwa sana na uwezo wake Mhe Lissu katika kutoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali.
mwenyekiti wa kamati hiyo Pro. Mahalu amekuwa mara nyingi akimtumia Lissu kutoa ufafanuzi juu ya hoja nyingi za wajumbe na Lissu amekuwa akijibu bila bila jaziba,uchama,wala hasira. Tena kwa ufafanuzi wa kina.
Nimejiuliza kama hata mawaziri wetu wangekuwa nao wanatumia style hiyo katika Bunge letu jee kungekuwa na migongano? Hii imeonyesha kuwa kumbe hawa tunaoita wapinzani wanao uwezo mkubwa sana wa kuendesha shughuli za serikali tofauti na wengi wanavyodhani.

Lisu is intelligent! He knows the subject matter of what he is talking. Usomi wake hauna mashaka.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom