Yanayojiri Bunge la Katiba Dodoma leo 06/03/2014

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Leo mtoto hatumwi dukani.Leo, asiye na mwana aeleke jiwe.Leo,ukigeuka nyuma unakuwa jiwe la chumvi.Leo,macho mbele kama tochi. Leo,masikio na macho ni marafiki muhimu. Leo, kila kitu kina watu;wale wastaarabu na fyatu.Usisubiri kusimuliwa.Jionee au sikiliza mwenyewe leo.

Kwa nyaraka zilizopo,shughuli hiyo itakuwa jioni.Leo,Bunge la Katiba linafikia vifungu vya 37,38 na 39 vya Rasimu ya Kanuni za Bunge hilo ili kuvipitisha.Vifungu tajwa,pamoja na mambo mengine, vinazungumzia namna ya upigaji kura wa kupitisha Rasimu ya Katiba utakavyokuwa ndani ya Bunge hilo.Wapo wa KURA YA SIRI na KURA YA WAZI/DHAHIRI. Leo watajulikana vyema.

Lazima leo Bunge liamue kupitisha au kuviondosha vipengele hivyo vya Kanuni. Ni leo.Si kesho. Lakini, kupitisha SIRI au DHAHIRI kutafanywa kwa SIRI au DHAHIRI? Mwenyekiti wa muda ataongozwa na Kanuni au Taratibu zipi leo kuamua kuendesha kura za SIRI au DHAHIRI wakati itakapojitokeza haja ya kufanya hivyo? Leo kitaeleweka tu.Zege halilali!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (sasa Dodoma)

--------------

Wadau, nikiwa hapa Bungeni Dodoma, Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum anawatahadharisha wajumbe juu ya hatari ya kunyoosheana vidole kwa itikadi za kisiasa. Ufafanuzi huo umetolewa baada ya Mheshimiwa Ole Sendeka kumshutumu waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar, Abubakar Hamisi Bakari kuwa ana maslahi ya chama chake cha CUF. Sendeka alisema hivyo kutokana na Abubakar ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Kanuni kukataa majedwali ya marekebisho ya Sendeka na Ummy Mwalimu kwa madai kuwa hayakuwasilishwa kwenye kamati.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni Prof Mahalu ameeleza kuwa kulijitokeza makosa kwenye sekretarieti na kwamba aliwaomba wabunge waendelee kujadili vifungu hivyo pamoja na hiyilafu zilizokitokeza.

Binafsi nilikuwa sijawahi kumuona Mh. Pandu Kificho akiongoza mkutano wowote. Kutoka moyoni,hakuna spika mwenye hekima,busara,uvumilivu na upendo niliyewahi kumuona katika umri wangu kama Kificho. Kinachotokea bungeni {utovu wa nidhamu kwa baadhi ya wabunge} ni malezi ya hovyo {sio ovyo} waliyopata wabunge wetu toka kwa walezi wao. Mnaokataa kataeni habari ndiyo hiyo. Tutegemeeni siku 150 wakiwa bungeni kwa sababu tu ya utovu na ukosefu wa hekima. Nimekuwa nasema elimu na hekima ni vitu tofauti kabisa.

Jana bunge liliahirishwa kwakuwa wabunge walidai wamechelewa kupewa nakala ya sheria namba 32 hadi 43. Leo bunge limeahirishwa kwa sababu secretariet imetoa majedwali mawili ambapo jedwali moja halionyeshi majina ya akina Mwalimu na Sendeka.

Kwa vyovyote vile wazembe wanajulikana na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa dhidi yao.

Kama mwendo huu utaendelea kila siku bunge litakuwa linaahirishwa huku posho zetu waamka taabani zikiendelea kuliwa.

Ushauri wa bure kwa kamati ya kanuni, waandae sheria ya mpito kwamba hapo bungeni yeyote atakaeonekana kuanzisha vurugu asilipwe posho. Na kwa njaa walizonazo hao watu utaona kama watafanya tena fujo.

Kuna tabia nyingine imezuka ya watu kupiga tu kelele za kuzomea hata kama jambo linaweza kuzungumzika na majadiliano yakaendelea. Hili mimi naona linasababishwa na baadhi ya wabunge wanaotaka bunge kiahirishwe ili wakafanye starehe zao. Dawa ya hawa watu ni kuwawekea monitor atakaeandika majina ya wapiga kelele ili yanapotokea mazingira ya hivyo, majina yanasomwa then kama kawaida wanakatwa posho.

Haya yasipofanyika, hakuna rasimu wala katiba mpya hapo mjengoni. Tutarudi mwaka 77 kuendelea na zilipendwa. Kikwete alisema 'mkileta utoto hatutapata katiba mpya. Na kwa vile nchi haiwezi kuendeshwa bila katiba tutarudi kwenye katiba ya zamani'

Bungeni: Waandishi wa Habari Makanjanja

Ndivyo mchangiaji aliemaliza punde alivyosema katika Bunge hili la katiba waandishi wa habari ambao ni Makanjanja wasipewe nafasi na wanyimwe vibali vya kutoa taarifa za Bunge kule Dodoma wakati bunge linaendelea.,

Mjumbe mmoja ambaye ni mwakilishi wa Taasi zisizo za kiserikali (NGO) Mustapha ,kawa mbogo kwa madai ya Kua Mwenyekiti wa Bunge la Mabadiliko ya Katiba anapendelea na kuendeshwa na vyama vya siasa na watu maarufu kwa kuwapa nafasi za kutoa hoja huku akiwasahau wajumbe 201 walioteuliwa na Raisi na kujiona hawana wanachokifanya kwnenye Bunge hilo.

Je ni kweli Mwenyekiti anapendelea.

Mnyika kachangia kuhusu mavazi rasmi kachangia vazi la kitenge liongezwe mwenyekiti wa kamati ya kanunii kamkubalia. duuu bi kiroboto kaibuka anachangia anamkrash mnyika kwamba mavazi ya vitenge yasiruhusiwe kachangia pumba infact bi kiroboto yuko shallow.

kuna jamaa kakrash skafu kamtolea mfano. savimbi wa bongo. Mmoja kaibuka na vazi la kimasai nalo vipi liruhusiwe? Bi. sarungi kaja na mambo ya urembo wa asili nazani anamaanisha aruhusiwe kuvaa culture zake. Yaani kuna vituko kidogo.

Nassari kaongelea kwamba unadhifu ni kuvaa kimagharubi vazi la kitenge lisiruhusiwe labda huko kwenye kamati.
 
Ndugu zangu,

Watanzania leo tunavuta pumzi huku tukielekeza macho na masikio yetu katikati kabisa ya nchi yetu tuliyozaliwa na tunayoipenda. Ni Dodoma.

Huko itapatikana leo hatma ya mwelekeo wa mchakato wa kupatikana kwa Katiba Mpya ya Nchi Yetu.

Hata hivyo, kuna ishara mbaya kuwa tuliowatuma Dodoma wako katika hatari ya kukwamisha mchakato mzima kwa kujikita kwenye kupigania kisicho na maslahi ya nchi hii kwa miaka 50 au 100 ijayo.

Watapigania yaliyomo kwenye vifungu vya 36 mpaka 37 za Kanuni za kuendesha Bunge hilo Maalum. Inahusu namna watakavyofikia maamuzi, kuwa iwe ni kwa kura za faragha au dhahiri. Ndio, inahusu kura za siri au kura za wazi. Ni' vifungu vya kifo' maana ndivyo vitakavyoamua, kwa namna moja au nyingine, uhai wa mchakato mzima wa kuitafuta Katiba.

Tuliowatuma Dodoma wamejigawa katika makundi ya ' Sisi' na ' Wao'. Wanatafuta kushindana na kupata mshindi badala ya kutafuta muafaka wa Kitaifa. Na hakika, kama alivyopata kusema Rais wa Nchi, Jakaya Kikwete, kuwa kwenye kushindana huko hakuna atakayeshinda. Tutashindwa Sote. Na huo ndio UKWELI.

Hakika, huu ni mtihani mgumu ulio mbele yao tuliowatuma Dodoma. Wakishindwa mtihani huu, basi, ishara zinazoonekana ni za mkwamo wa jumla wa mchakato mzima. NI AIBU.

Tuliowatuma Dodoma hawajachelewa kuitafuta hekima na busara kutunusuru na aibu kubwa ya taifa iliyo mbele yetu. Tuliowatuma Dodoma wawafikirie pia watoto wa kesho na wa vizazi vijavyo katika nchi yetu tuliyozaliwa na tunayoipenda.

Na ushauri hapa ni heri kukubaliana kutokubaliana, na hivyo, kusitisha kwa muda mchakato huo, kuliko kulazimisha kwenda mbele. Ni ushauri pia, kuwa ni heri kuyatafuta maridhiano kwanza kabla ya kuingia kwenye majadiliano, kuliko kuyatafuta maridhiano baada ya kuingia kwenye mapigano na kujeruhiana. Ni busara basi, tuliowatuma Dodoma wakaunda Kamati Maalum ya kuyatafuta maridhiano wa vifungu hivyo. Na ifahamike, kuwa MARIDHIANO ndio msingi wa UHALALI wa mchakato na hata Katiba yenyewe.

Tusipotanguliza busara, hekima na maslahi ya taifa, yumkini yaweza ikawa kama yale aliyopata kuyasema miaka 60 iliyopita, mwandishi yule mahiri, Mtanzania mwenzetu Shaaban Robert, aliandika; " Wasadikika wana desturi ya kutafuta fimbo baada ya kuumwa na nyoka. Tumekwisha umwa na nyoka wa matendo yetu mabaya ya zamani.

Nyoka mwenyewe amekwishakimbia. Hapatikani kwa kujilipiza kisasi, lakini, sumu yake imebakia katika jeraha tulilolipata. Sasa, shauri lililo jema ni kuzuia sumu hii isienee miilini mwetu ikaleta kifo.

Maovu yana hatari kubwa kukaa kati yetu. Tumedumu nayo kwa muda mrefu. Hayakutuletea faida ila hasara, huzuni na kilio siku zote."- Shaaban Bin Robert.

Ni Neno La Leo.
Maggid Mjengwa,
0754 678 252
MjengwaBlog :: Habari, Picha, Matangazo na Matukio
 
Maccm hayajiamini, yanaogopa kupiga kura kwa kutumia box la kura.
 
Siri kwa ulinzi na usalama wa wajumbe wa baraza la katiba na wazi kwa kuwanyima uhuru na kuwatisha baadhi ya makundi ya wajumbe.
 
Ukiondoa unafiki wa kawaida wa kibinadamu, kila mtanzania angependa aipate hiyo nafasi ya kuwa mjengoni kwa sasa. Kitu ambacho kingetofautisha ni dhamira, nia ya dhati na mchango wa mtu akiwa pale. Hapo ndo ningetofautiana na wengine. Ningehudhuria vikao vyote hata kama ni usiku wa manane, ningesaini fomu yoyote ya posho inayokatiza kwangu, kura yoyote ya siri nisingeshiriki, na mwisho ningekaa kimya vikao vyote huku nikivuta mkwanja tu. Sababu yake ni kwamba hao wote walioko hapo bungeni ni porojo tu, katiba itatoka kama ambavyo 'wenye mamlaka' watataka iwe. Kinachofanyika hapo ni ulaji na kupotezeana mda.
 
christopher mtikila:Haki ya kupiga kura kwa
siri haitofautiani na haki ya mtu
kuwa na miguu miwili na kwamba
itashangaza akitokea mtawala
akaamuru kila mtu awe na mguu
mmoja, halafu watu wakakaa
kujadili.
“Wote tutaonekana tuna matatizo
ya akili,” alisema Mch. Mtikila.
Alisema Bunge Maalumu la Katiba
litaingia katika hatia na aibu kwa
kujadili mambo ya msingi ya
kidemokrasia ambayo pia
yameainishwa katika katiba ya sasa,
likiwamo suala hilo la kura ya siri.
“Mwenyekiti (akimlenga Pandu
Ameir Kificho) tumekuchagua kwa
kura ya siri siyo kwamba tulikuwa
wajinga kuliko wenzetu, hapana! Ni
‘democratic civility’ (ustaarabu wa
kidemokrasia),” alisema.
“Ni aibu waheshimiwa na hii
nasema si jambo la mjadala kuna
vitu vya kujadili, lakini si haki ya
kupiga kura kwa siri. Hii ni haki ya
msingi ya kidemokrasia,” alisema
 
Last edited by a moderator:
Nimesikia mwenyekiti akilalamikia muda, hivi kwa nini bunge halianzi asubuhi, badala yake wanapoteza muda na kuanza kulia lia? Hayo mapumziko wanayotaka kila wakati ni ya nini? wabunge wafanye kazi jumatatu mpaka ijumaa.. Bunge lianze saa 3 mpaka saa 7, saa 11 mpaka saa 2 usiku... WASITULETEE LONGO LONGO HAPA.
 
Sawa mkuu nimekusoma na kukuelewa.

Msaada kidogo, Leo kikao cha bunge la katibaba kinaanza saa ngapi?
 
Nimesikia mwenyekiti akilalamikia muda, hivi kwa nini bunge halianzi asubuhi, badala yake wanapoteza muda na kuanza kulia lia? Hayo mapumziko wanayotaka kila wakati ni ya nini? wabunge wafanye kazi jumatatu mpaka ijumaa.. Bunge lianze saa 3 mpaka saa 7, saa 11 mpaka saa 2 usiku... WASITULETEE LONGO LONGO HAPA.
Kwa hela wanayolipwa hata wakikesha ni sawa.
 
Ndugu zangu,

Watanzania leo tunavuta pumzi huku tukielekeza macho na masikio yetu katikati kabisa ya nchi yetu tuliyozaliwa na tunayoipenda. Ni Dodoma.

Huko itapatikana leo hatma ya mwelekeo wa mchakato wa kupatikana kwa Katiba Mpya ya Nchi Yetu.

Umenena ukweli Rafiki yangu Majid. Hata hivyo ninafikiri bila majibu chimbuko la ushindani wa kura za siri na wazi kwa kupiga kwa siri au uwazi. Wanaotaka za siri huenda ni utaratibu wa kawaida siku zote. Wanazotaka za wazi wana jambo gani!? Ni nani anayependa serikali mbili ni kundi litakalo za siri au za Wazi? Wanaotaka serikali mbili kinyume na maoni ya wariomba wana interest gani hasa? Je? Madhara ya serikali 3 ni yepi? Kwanini mwalimu Nyerere alikataza kabisa kuuwaza, kuufikiria wala kuujadili muungano!? Kwani ili kuwa ni dhambi isiyosameheka kuujadili muungano.

Je? Watanzania wakiwemu wajumbe wa katiba mpya, walikuwa wanajua kuwa mjadala wa katiba si mrahisi kama wanavyofikiri? Tunahitaji muda, tunahitaji uvumilivy, tunahitaji busara. Kinyume na hapo ni AIBU TUPU.
 
Maana wanapiga kelele bungeni na kuzomea ovyo kama watoto wa Kindagaten! Yaani hawana hekima wala busara! Mpaka wanakera! Wao wanadhani ukiishakuwa mpinzani basi ni kupinga tu hata kama huna hoja! Kibaya zaidi wanazomea kama wehu! Hawafai, wanakula hela za walipa kodi bure!
 
Sendeka -------- wewe..nimesikia mjumbe akimtukana sendeka..wito kwa wajumbe nidhamu ni muhimu wajumbe
 
Wadau, nikiwa hapa Bungeni Dodoma, Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum anawatahadharisha wajumbe juu ya hatari ya kunyoosheana vidole kwa itikadi za kisiasa. Ufafanuzi huo umetolewa baada ya Mheshimiwa Ole Sendeka kumshutumu waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar, Abubakar Hamisi Bakari kuwa ana maslahi ya chama chake cha CUF. Sendeka alisema hivyo kutokana na Abubakar ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Kanuni kukataa majedwali ya marekebisho ya Sendeka na Ummy Mwalimu kwa madai kuwa hayakuwasilishwa kwenye kamati.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni Prof Mahalu ameeleza kuwa kulijitokeza makosa kwenye sekretarieti na kwamba aliwaomba wabunge waendelee kujadili vifungu hivyo pamoja na hiyilafu zilizokitokeza.
 
Back
Top Bottom