...Yanadondoka

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,809
Kuna jamaa mmoja ndo ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuja hapa Uingereza. Na kwa bahati amekuja wakati wa msimu wa theruji (winter) na yeye tangia kuzaliwa hajawahi kuona barafu ikishuka. Siku moja wakati yupo matembezi karibu na home kwao, mara barafu ikaanza kushuka kwa kasi na kwa wingi. Jamaa kuona theruji ikishuka akajuwa sasa ndo mwisho wa dunia, akaanza kutimua mbio mpaka kwao na huku akipiga kelele… jamaaniii eeeeeeeh!!! nafaaa hukuuu… mawingu yanadondokaaa…!!! nifungulieni mlangooo… jamaa kufungua mlango na kuanza kumhoji mambo yalikuwa ivi…

Jamaa: vp wewe mbona makelelee mengii?


Mgeni: wewe uwoni nini, nje mawingu yanadondoka hujui kama inawezekana ndo mwisho wa dunia?


Jamaa: uku akicheka… wacha ushamba wewe hiyo ni theruji au barafu huu ni msimu wa winter kaka…!


Mgeni: unataka kunambia huko juu kuna friji ama...?

Mimi kuona ivo na kuzingatia kuwa nilishaaga nikajiondokea zangu, huku nikikata mbavu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom