Yametimia!, CCM Imechokwa!, CHADEMA Njia Nyeupe 2015!-Jipangeni!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,179
Wanabodi,
CCM sasa ni "sikio la kufa..." na kama ni tunda, basi ni "lakuvunda..."
CCM imechokwa, Wananchi wameamka na sio watu wa kuswagwa na kupelekwa pelekwa tuu kama ling'ombe!.

Chadema mkiamua, mnaweza!, njia kuelekea 2015, yaani njia ni nyeupe!, kilichobakia ni kujipanga kwa kupanga mipango mkakati na kuunda kikosi kazi kitakachokabidhiwa malengo na kujadili utekelezaji with time frame, 2015, Ikulu ya Magogoni ni yenu!.

Watanzania ni wale wale na CCM ni ile ile, na kuwa sio inachaguliwa kwa kupendwa, bali imekuwa ikichaguliwa kwa mazoea, maadam sasa imechokwa, hakuna namna ya kuiokoa, safari ya kuelekea kaburini imewadia, kilichobakia ni kusubiria tuu itakufa kifo gani!.
Chadema ijipangeje?.
CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!
Kuelekea 2015: CHADEMA Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!
Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni .....!

Namalizia kwa kuipongeza sana Chadema, ushindi ni ushindi tuu, ni mtamu!, always sweet victory, "the winner takes it all, the looser standing small!".
Hongereni sana Chadema.

Pasco.
 
Pasco, naona umesahau (again) kuwa ulitabiri nini kuhusu huu uchaguzi wa Arumeru Mashariki. Infact sio tu ulitabiri you were certain about the outcome. Sasa umeguaka! lost for words!
 
..CCM mbona ilishakufa zamani??

..hivi kwa akili zako inawezekana CCM, chama cha kijamaa, kikaongozwa na mwenyekiti anayemiliki mgodi wa makaa ya mawe[kiwira]??

..hivi kweli CCM, chama cha ukombozi wa Afrika, kinaweza kuongozwa na mwenyekiti[baada ya mmiliki wa kiwira kustaafu] anayehongwa suti na mfanyabiashara Mwarabu?

..tena mwenyekiti mwenyewe ni waziri katika serikali, na kwa nafasi yake hiyo serikali ilikuwa ikimnunulia suti kwa miaka 10.
 
kama ni kijana nakupa pole kushabikia magamba...ukiamua songa mbele...ukiwa double standard lazima ugeuke jiwe la chumvi.
 
Wewe ndo pasco naekufahamu?? Nakufahamu kama mkereketwa na muhumini mzuri tu wa ccm magamba asa unavyotukataga ngebe tukiipinga ccm, any way labda sikukujua vizuri,, but good comments
 
mimi sina cham hata kazi yangu hainiruhusu kuwa na chama ila
moyoni mwangu napenda mageuzi napenda chadema wana sera nzuri
siwezi kujivunia CCM kwa vile serikali yao inanipa mkate lkn wananchi wakifa na njaa wachache wakifaidi
kwa kweli CCM imechoka,wananchi wameamka na nina Imani kaburi lao litawekwa zege 2015.
viva chadema viva watanzania amkeni kumekucha.
Pasco naamini moyoni mwako uko na chadema na umekuwa mwazi
 
Pasco unahitaji kuangalia movie inayomzungumzia Frédéric Bourdin (le caméléon) inayoitwa The Chameleon!!!
 
Hivi Pasco ili CDM ionekane imejipanga unataka ifanye nini? Ina maana Mwanza, Songea na Kiwira CDM kimeshinda kwa sababu ya kuchokwa kwa CCM tu?
 
Pasco ana pwenti, ila ni mnafiki mno!!!
powe.jpg
 
Mkuu Pasco anapaswa kujiita Pasco the comedian yaani sijataka kusema ile tafsiri yake hasa.

Watu hawajaichoka CCM bali wanataka mabadiliko. Wanaweza kuwa bado wana mapenzi na CCM lakini ni vizuri kwa wakti huu na hata kufikia 2015 Chadema kikawa chama tawala.

Halafu Pasco anasema amemfahamu Siyoi na alikuwa MC kwenye harusi yake.

Lakini Pasco asisahau pia kuwa kuna watu kama akina sisi ambao tunamfahamu Siyoi tangu akitumia jina la Siyoi Solomon na alipoambiwa atoe jina hilo na aweke la Sumari ili kupalilia nafasi yake kwenye siasa.

Siyoi alikwishapewa ushauri na watu ambao wanamfahamu kwa karibu kwamba aachane na haya mambo ya siasa na atafute tu kujiimarisha kwenye fani yake ya sheria na hakuweza kusikia labda kwa shinikizo la baba mkwe wake.

Afadhali kaka yake Kisali aliamua mapema kutojihusisha na mambo haya ya kuvaa magamba ambayo hawafahamu chanzo chake.
 
Pasco Pasco au Pascola au Scola wewe tena ama kweli Jaquar wa Kenya kaimba na nukuu kidogo tu kwa mbali Huyu pasco kigeugeu......huyu si ndo yule alitalia CHADEMA kuanguka sasa katoka wapi tena duuh ama kweli Makamanda wako sawa njaa mbaya na njaa hii inasababisha now day hata wanaume wanaolewa pole sana Pascola kwa kuangukia pua wewe na Magamba wenzako plus Sioi na sasa ataolewa,Yu wapi Lusinde mgonjwa wa akili hatumlaumu sana kwani huenda ugonjwa wa akili ndio unamfuatilia ati huyu Lusinde na Kudadadeki zake.Kwa ushauri tu nawaomba wale wote wanaongozwa na huyu somebody so called Lusinderela wamsindikize milembe kabla mambo hayajakuwa mambo.
Ati pia ni mtunga sheria Lusinde naomba kama utasoma hapa acha ujumbe tu na nitakujibu safi sana Kudadadeki subiri kupanda kizimbani kwa matusi yako uliyowatukana viongozi wa ukweli.
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom