Yamenikutaaa ndugu zangu

Si afadhali uchomwe kisu ndugu yangu unaweza kuponea chupuchupu. Anaweza akamkata Mr. Kipara huko chini akakuacha huna jinsia.
 
Huyo dada ananipenda kufa wivu umemzidi mkuu mpaka inakera sana

Ndio maana nimekueleza kuwa kitakachofuata ni wewe kukatwa mashine yako ubaki bila jinsia. Tena akikutembelea uwe unalala na jeans kabisaa kujihami.
 
sikiliza instincts zako. kama moyo wao unasita kumuoa, usimwoe kabisa. huenda kuna kitu kikubwa na kibaya kiko mbeleni kati yenu na hizo ni tahadhari. mke wa kumuoa hu-flow naturally na wala hutoona kuwa unatumia nguvu kubwa kupambana na resistance ndani ya nafsi yako kuingia kwenye ndoa.
 
Za sahizi wanajamii. Ni siku nyingi sijajiunga nanyi lakini leo ninahitaji msaada wenu wa mawazo. Nina uhusiano wa mapenzi na msichana mmoja toka 2007. Ni muda mrefu sana lakini kinachonishangaza moyo wangu unajiuliza mara mbili mbili kumuoa najiuliza sana kwanini. Ila tatizo kubwa ana wivu sanaaa umepitiliza kabisa kiasi kwamba vitu vidogo anasema nimemcheat anataka tuachane bila ushaidi. Kuna kipindi flani nilinyimwa unyumba kwa zaidi ya miezi 8 nikamwambia sitakuja kumuomba unyumba daima.

Kiukweli bado nampenda lakini nakereka sana vitu vidogo anasema tuachane imezidi sana. Kutokana na umbali wa ninapoishi nimejikuta na uhusiano na msichana mwingine ambao si wa mapenzi na huyu dada anatambua kuwa nina msichana. Mwezi wa 7 nilikua nimepanga kumvisha pete huyu mpenzi wangu lakini kabla ya muda kufika akaja ghafla mkoa akakuta msg za yule rafiki yangu ikawa balaa akampigia simu yule dada akamwambia sisi ni marafiki tuu.

Hakutaka kuamini akachukua vitu vyake vyote akaondoka zake. Baada ya siku chache akaanza kupigia simu wasichana wote aliokuta msg zao na kuwaambia vitu vya ajabu ajabu kwamba mimi nina wasichana wengi na mambo mengine machafu sana ambayo siwezi ongea.

Naona story inakua ndefu anyway sasahivi tunawasiliana vizuri ila kila siku napigiwa simu usiku wa manane nikiwa nimelala asubuhi nakutana na messege tuachane kweli nimechoka huu wivu wa hatari. Hebu jamani naombeni msaada huyu dada ananifaa au ndo ntaishia kuchomwa kisu maana ni mcha.....

Ukiendelea naye huyo utajuta atakapokuwa ameingia ndani 'rasmi' utajuuuuuuuuuuuuuta kwa nini ulimuoa. Mpige chini mkuu au kama vipi fuatilia familia yake ujue wazazi wake wanaishije, usije ukaoa matatizo ukaishia kufa bure. Wengi wa wanawake wa mtindo huo huwa wanatoka kwenye familia ambayo baba na mama huwa hawana mahusiano mazuri. So inakuwa kama msichana anajihami asije akakutana na matatzo alopitia mama yake. Kama hali ilikuwa hivy kwao, atakupa matatatizo sana na hautaweza furahia maisha ukiwa naye. Whatch out, you are diging up your own grave in which you will be burried alive!!!!!!!!! Ushauri tu!
 
Huyo demu ni mmachame nini? Angalia mkuu unaweza ukawa genderless!
 
"listen to many but decide alone" yaonekana kabisa kuwa huyu dada anakupenda kumbuka kuwa hana IMAN na wewe tena kuringana na hzo text hata angekuwa n mm kukutra text yake ya mapenzi arafu anadai ni rafiki yako 2 wakawaida na vle vtext lazma awe vle cha msingi na hapo ni patamu sana ulishajua tatzo la ugonvi wake nini, jtahid kubadilika na kumuwekea mazngira ya kukuamini, kama vp tokea leo we mpe simu yako tu, i mean awe na huru wakuimilik utakuwa umeua kasi yote.
 
Mapenzi hayako hivo akupendaye atakuamini..... nyuma ya pazia yy ni msaliti na anfikiri ww pia u msaliti take time mchunguze
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom