Yamenikutaaa ndugu zangu

subzero

Member
Jan 15, 2011
86
4
Za sahizi wanajamii. Ni siku nyingi sijajiunga nanyi lakini leo ninahitaji msaada wenu wa mawazo. Nina uhusiano wa mapenzi na msichana mmoja toka 2007. Ni muda mrefu sana lakini kinachonishangaza moyo wangu unajiuliza mara mbili mbili kumuoa najiuliza sana kwanini. Ila tatizo kubwa ana wivu sanaaa umepitiliza kabisa kiasi kwamba vitu vidogo anasema nimemcheat anataka tuachane bila ushaidi. Kuna kipindi flani nilinyimwa unyumba kwa zaidi ya miezi 8 nikamwambia sitakuja kumuomba unyumba daima.

Kiukweli bado nampenda lakini nakereka sana vitu vidogo anasema tuachane imezidi sana. Kutokana na umbali wa ninapoishi nimejikuta na uhusiano na msichana mwingine ambao si wa mapenzi na huyu dada anatambua kuwa nina msichana. Mwezi wa 7 nilikua nimepanga kumvisha pete huyu mpenzi wangu lakini kabla ya muda kufika akaja ghafla mkoa akakuta msg za yule rafiki yangu ikawa balaa akampigia simu yule dada akamwambia sisi ni marafiki tuu.

Hakutaka kuamini akachukua vitu vyake vyote akaondoka zake. Baada ya siku chache akaanza kupigia simu wasichana wote aliokuta msg zao na kuwaambia vitu vya ajabu ajabu kwamba mimi nina wasichana wengi na mambo mengine machafu sana ambayo siwezi ongea.

Naona story inakua ndefu anyway sasahivi tunawasiliana vizuri ila kila siku napigiwa simu usiku wa manane nikiwa nimelala asubuhi nakutana na messege tuachane kweli nimechoka huu wivu wa hatari. Hebu jamani naombeni msaada huyu dada ananifaa au ndo ntaishia kuchomwa kisu maana ni mcha.....
 
Wanawake mbona wapo wengi sana mkuu? Kila kitu hapo kinajieleza...HUPENDWI
 
aibu!! kaka mie nakushauri wewe achana nae.....sasa hapa la msingi ni jinsi utakavyo mueleza kwa nini humechukuwa uamuzi huo.

jambo kuu hapa ni kwamba yeye hana imani kwako na bila trust hamna ndoa hapo. sasa wewe haupo tayari ku-spend maisha yako ya ndoa ukiwa unajaribu kumuonyesha yeye kuwa u cn be trusted. so bora tuachane tuu.

jambo la kizingatia hapa ni kwaba anaweza kukwambia kuwa atabadilika...hapa hamna ukweli. hii tabia itajitokeza tuu mkisha kuwa husband and wife....so kataa.
 
Siku akisema tena muachane basi wewe kaza buti mwanzo mwisho achana nae,ndugu yangu ukioa huyo utakereka hadi utamani kufa
 
Wivu huwa hauna neno tuachane. Jatahidi kumchunguza alipokuwa anaishi ni lazima atakuwa na mpenzi mwingine ila anatafuta kisingizio cha kuachana na ww 2 ili siku ukisikia ana mwingine ujue kwamba ww ndio chanzo.
 
Za sahizi wanajamii. Ni siku nyingi sijajiunga nanyi lakini leo ninahitaji msaada wenu wa mawazo. Nina uhusiano wa mapenzi na msichana mmoja toka 2007. Ni muda mrefu sana lakini kinachonishangaza moyo wangu unajiuliza mara mbili mbili kumuoa najiuliza sana kwanini. Ila tatizo kubwa ana wivu sanaaa umepitiliza kabisa kiasi kwamba vitu vidogo anasema nimemcheat anataka tuachane bila ushaidi. Kuna kipindi flani nilinyimwa unyumba kwa zaidi ya miezi 8 nikamwambia sitakuja kumuomba unyumba daima. Kiukweli bado nampenda lakini nakereka sana vitu vidogo anasema tuachane imezidi sana. Kutokana na umbali wa ninapoishi nimejikuta na uhusiano na msichana mwingine ambao si wa mapenzi na huyu dada anatambua kuwa nina msichana. Mwezi wa 7 nilikua nimepanga kumvisha pete huyu mpenzi wangu lakini kabla ya muda kufika akaja ghafla mkoa akakuta msg za yule rafiki yangu ikawa balaa akampigia simu yule dada akamwambia sisi ni marafiki tuu. Hakutaka kuamini akachukua vitu vyake vyote akaondoka zake. Baada ya siku chache akaanza kupigia simu wasichana wote aliokuta msg zao na kuwaambia vitu vya ajabu ajabu kwamba mimi nina wasichana wengi na mambo mengine machafu sana ambayo siwezi ongea. Naona story inakua ndefu anyway sasahivi tunawasiliana vizuri ila kila siku napigiwa simu usiku wa manane nikiwa nimelala asubuhi nakutana na messege tuachane kweli nimechoka huu wivu wa hatari. Hebu jamani naombeni msaada huyu dada ananifaa au ndo ntaishia kuchomwa kisu maana ni mcha.....[/QUOTE]



hapo redi ni mcha mungu au?
 
Labda kama dunia hii kaumbwa yeye peke yake, basi itakulazimu uendelee kutaabika tu mkuu.
 
Piga chini kabisaaa, huyo anakuibia na kukuweka rehani, anayekupenda hawezi kulitamka kiurahisi neno la kuachana.
Wewe mtegee, akirudia tena kusema muachane shikilia hapohapo, miaka minne tuu, watu wanakaa zaidi ya miaka hata kumi lakini bado wakiona hawaendani wanaachana. Ni mapema sana kwa hiyo take an action, achana naye tafuta mwingine wa kumwoa.
 

Binafsi mimi naamini kuwa binadamu tumetofautiana sana kwa tabia na hii inatokana na makuzi yetu, lakini kitu cha msingi katika mahusiano ya aina yoyote ile ni kukubali udhaifu wa mwingine kitu ambacho wewe umefanikiwa. Kama wivu ni tabia yake basi mchukulie hivyo na fanya vitu ambavyo havitampelekea kupata wivu. Naamini kuwa hata uachane nae leo utampata mwingine agahlabu huyo mwingine anaweza kuwa na tabia ya u-kicheche hapo ndio utaomba ni afadhali yule mwenye wivu ulimwacha.

Jiangalie pia wewe nijuavyo kila binadamu anamapungufu na katika mahusiano kuyatambua na kuyakubali mapungufu hayo ni 90% ya kuimudi hiyo relationship!
Ushauri wangu ni kuwa jaribu taratibu kumshauri juu ya tabia hiyo ambayo wewe hufurahi kama ni wa kukuelewa basi itafika wakati atakuelewa na mtaishi maisha ya upendo na amani. Kuachana na tu udhaifu kuwa umeshindwa kumudu uhusiano ambao kimsingi hupaswi kushindwa kuumudu!

Umepewa ushauri na namna nyingi lakini mwisho ni uamuzi wako maana wewe ndiye unayemjua in and out!
 
Mapenzi ni imani, wewe umeshaamini kuwa anakupenda, ila mtu anayekupenda hafanyi hayo uliyoandika. Pia kumbuka kuwa kuna mstari mwembamba sana unatenganisha kati ya mapenzi ya kweli na uzoba. Kuwa makini.
 
Huu ugomvi wa tuachane ni mbaya sana, hii kitu ni mpaka kwenye ndoa na utashtukia ndoa imekwisha ki-masikhamasikhara kwa sababu ya huu u-tuachane.
Mungu amekusaidia umepata muda mzuri wa kumsoma, sasa kama unaona kabla ya ndoa huwezi kuhandle usijidanganye kwamba utahandle ndani ya ndoa.
Changanya na za kwako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom