Yame wakuta

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
5,565
836
Jamaa fulani ana karibia kuoa. Wenzie wanamshawishi akajirushe kwa mara ya mwisho maana baada ya hapo atakua "mfungwa". Kwa hiyo jamaa anatoka usiku na washikaji zake. Mida ya usiku sana imefika anaingia kwenye nyumba inayo uza wasichana/wanawake. Anaingizwa kwenye chumba na "mama mwenye nyumba" ana muahidi kumletea "bidhaa" achagua. Wakaingia wasichana warembo watano. Jamaa kuinua kichwa ana kutana uso kwa uso na Mrs. mtarajiwa(mchumba wake). The story goes on lakini swali langu ni je ingekua wewe ungefanyaje(kama wewe ni huyo mwanaume au huyo binti)? Je hapo ni kusameheana tu kwa ajili wote ni wakosaji au kuvunja mipango ya ndoa? Mkivunja ndoa mtatoa sababu zipi?
 
Mh! Kaka hapo kama ni mimi nitaivunja tu hiyo ndoa manake kwa kawaida mwanamke kufanya mambo kama hayo ikiwa si kwa dhiki basi ni hulka yake na ni vigumu kuibadilisha na kama ni kwa dhiki ina maana ndo shughuli yake na itakuwa vigumu kuiacha kwa sababu kwenye familia mambo yakienda kombo kidogo itamuwia rahisi kufikiria Plan B yake. Kwa upande wetu wanaume hiyo huwa ni tamaa zaidi ndo inatuongoza kufanya hii kitu (Nilisikia utani mahali kuwa wanaume wana vichwa viwili na haviwezi kufanya kazi kwa wakati mmoja)

Kama ni kueleza sababu za mimi kufanya hivyo nitasema tu ukweli kuwa tumefumaniana ila sintopenda kuendelea naye kwa sababu nimepoteza imani naye, yeye pia ana haki ya kusema hivyo hivyo kuhusu mimi na sintommaind kwa kuniunguzia. Ila mazee hii kitu Mungu aepushie mbali manake ni msala wa aina yake huo.
 
unaweza ukafa kwa presha, ila kama inakuwa hivyo da hapo ndio inakuwa mwisho ili kila mtu akajipange upya
 
Itabidi kusamehehana na kuendelea na mipango ya ndoa yawezekana mwanamke nae ameshawishiwa kujirusha vya mwisho mwisho kabla ya kuingia kifungoni, hapo chacha...!!!!!!!!!!!!! baada ya hapo kila mmoja atakuwa mwaminifu kwa mwenzie.
Nawasilisha
 
Mzinifu atamuoa mzinifu mwenzie. Sasa wamfuate nani? Waendelee ili wawewanakutana hukohuko.
 
Birds of the same feathers flock together! Sasa huyo bwana atakuwa anashangaa au kukasirika nini ilhali na yeye yuko na makosa hayohayo?Who is cheating who?
 
Birds of the same feathers flock together! Sasa huyo bwana atakuwa anashangaa au kukasirika nini ilhali na yeye yuko na makosa hayohayo?Who is cheating who?

All of them are cheaters. The only difference is that one sells and the other buys.
 
Mara nyingi utasikia watu wanadai mume na mke wamefanana baada ya ndoa. Mie nadhani huwa wanafana kabla ndio maana hao wamekutana
 
mh! ama kweli siku za mwizi arobaini - wote wako kwenye boat moja - hiyo safari yao ya ndoa sijui itakuwaje??? boat litazama tu njiani - MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI - dawa kuuzima moto ni maji - sasa wote ni moto - basi MOTO HUO MKUBWA - afadhali waachane tu
 
Siku zote,mkubwa hakosei.Kwa utamaduni wetu hapo mwanamme ndo mkubwa.
Km ni ni mimi nitawaita wazee niwambie kuwa nimepata tetesi kuwa mchumba wangu ana tabia mbaya..nimeweka mtego na nimemkamata akiwa dangulo.

Nitakuwa nimejitetea na nimehamisha makosa.Hapo kinachofatia ni kumtema maana sababu iko nje nje.

Usiombe mke kuwa changu...kikwetu mme hawi malaya ila anateleza,halali nje ila anachelewa kurudi....itaendelea kueleweka hivo..
 
Jamaa fulani ana karibia kuoa. Wenzie wanamshawishi akajirushe kwa mara ya mwisho maana baada ya hapo atakua "mfungwa". Kwa hiyo jamaa anatoka usiku na washikaji zake. Mida ya usiku sana imefika anaingia kwenye nyumba inayo uza wasichana/wanawake. Anaingizwa kwenye chumba na "mama mwenye nyumba" ana muahidi kumletea "bidhaa" achagua. Wakaingia wasichana warembo watano. Jamaa kuinua kichwa ana kutana uso kwa uso na Mrs. mtarajiwa(mchumba wake). The story goes on lakini swali langu ni je ingekua wewe ungefanyaje(kama wewe ni huyo mwanaume au huyo binti)? Je hapo ni kusameheana tu kwa ajili wote ni wakosaji au kuvunja mipango ya ndoa? Mkivunja ndoa mtatoa sababu zipi?

Mi nahisi upande wa pili ulikuwa nao unawaza hivi
Dada fulani ana karibia kuolewa. Wenzie wanamshawishi akajirushe kwa mara ya mwisho maana baada ya hapo atakua "mfungwa". Kwa hiyo huyo mdada anatoka usiku na mashosti zake. Mida ya usiku sana imefika anaingia kwenye nyumba ambay wanaume huwa wanakuja kununua wasichana/wanawake!!!!

Kwa sense hiyo hakuna wakumlaumu kwa kuwa kila mmoja alikuwa anaaga uhuru wake wa ubachelor.
 
Both are win win!!! Nataka nijue baada ya kunyanyua kichwa na kumwona mamsapu mtarajiwa alijirusha naye au alivaa suruali akaondoka, au alichukua kabinti kengine kati ya wale walioletwa na mkuu wa danguro?? Na wife mtarajiwa ilikuwaje???Tumeachwa hewani.

Bottom line, hiyo ndoa kama ililazimishwa kufungwa, haitadumu!!! Na bora kila mtu atizame kusini na kaskazin asubiri neema na huruma ya Mungu ili apate mchumba mwingine.
 
Kwa upande wangu ningeachana nae niendelee na ukahaba wa mtaani. Hapo hakuna kusameheana shetani huyo anaendelea mpaka siku mnakufa.suppose wasingekutana mmoja angefanya na mwingine kufanywa.
 
Kwa upande wangu ningeachana nae niendelee na ukahaba wa mtaani. Hapo hakuna kusameheana shetani huyo anaendelea mpaka siku mnakufa.suppose wasingekutana mmoja angefanya na mwingine kufanywa.
Nadhani wengi wanasema hapa si ajabu ndio process walizopitia ila kwa bahati mbaya hawakuonana. Sasa wakiachana waende kwa nani? Hao wakae wenyewe kwa sababu tayari wanajuana vizuri, na watajirekebisha. Hata wakiwa kwenye ndoa mmoja akichelewa wanajua wakatafutiane wapi.
 
Jamaa angemchagua huyo mtarajiwa wake waendelee kujirusha kuanzia hapo mpaka home, then no ndoa tena!
 
Siku zote,mkubwa hakosei.Kwa utamaduni wetu hapo mwanamme ndo mkubwa.
Km ni ni mimi nitawaita wazee niwambie kuwa nimepata tetesi kuwa mchumba wangu ana tabia mbaya..nimeweka mtego na nimemkamata akiwa dangulo.

Nitakuwa nimejitetea na nimehamisha makosa.Hapo kinachofatia ni kumtema maana sababu iko nje nje.

Usiombe mke kuwa changu...kikwetu mme hawi malaya ila anateleza,halali nje ila anachelewa kurudi....itaendelea kueleweka hivo..

Basi you are not a real man if you can't own up to your mistakes. Unajiita mwanaume halafu you hide behind the woman? For a mistake you yourself committed? Man up bana, kama kweli mwanaume ndiyo mkubwa unaogopa nini kusema what you really went to do?
 
Back
Top Bottom