Kwa mara nyingine naomba niwape ufafanuzi kuhusu yaliyomsibu maana mm binafsi jana nilienda kwake,Pole sana mkuu. Muhudumu wa Mochuari alikua anapiga dili gani hasiwepo ofisini kwa masaa 2? Utaratibu wa kuhifadhi mwili ulifuatwa kweli? Kwasababu ilikua ni kazi ya manesi/wahudumu kupeleka mwili mochuari. Kwa mara nyingine pole kwa kumpoteza mtoto wenu kipenzi Mariam
pole sana ,mkuu ila umefika wakati tufanye kitu kwajili ya nchi yetu kwni tunaomia ni watu wa chini mkuu,kama wanJF naomab tufanye jambo jamani....,tukoe wenzetu
....Njowepo hapo kwenye one day yes ndipo panapotuharibia watz....anyway inaniuma sana kuona tuna viongozi walipoteza muelekeo na kubaki kulia lia na kusikitika badala ya kuchukua hatua. Hivi kwa nini watanzania tusifanye kweli kwenye sanduku la kura 2015??? Huu utumbo wa CCM unaoendelea kuzamisha nchi lazima ufike mwisho jamani....Pole kwa yote Spika. This is time for CHANGES!!Pole mkuu!
Personally najipa moyo one day tutapata suluhisho la yote haya!
RIP Mariam
Ndg zangu wana JF nadhani niliwapa taarifa juu ya kifo cha mwanangu mpendwa "MARIAM ALLY"aliyefariki siku ya j,mosi usiku.
Mwanangu alikua na umri wa miezi 9 hv,alianza kuugua malaria siku ya tar 29.02,usiku,tukampeleka dispensary alfajiri ya tar 1.3 na akapata vipimo na kuandikiwa doz ya malaria bcoz alikua na malaria "2".
Aliendelea na doz mpaka siku ya tar 3 asubuhi nilipogundua kama anaupungufu wa maji mwilini,tukamrudisha dispensary ile ile kwa ajiri ya kumcheki tena,baada ya kumcheki dk alisema amepungukiwa maji kwahiyo anatakiwa kupewa drip,alitundikiwa drip kuanzia majira ya saa 5 asubuhi,ilipofika majira ya saa 12 jioni dr akatupa rufaa kwenda muhimbili, nilikodi tax na tukafika muhimbili ndani ya muda muafaka,nilipokelewa na dr1 hv bwana mdogo na alijaribu kunisaidia ili tumuwaishe kwenye oxsijen lakini ilishindikana maana madaktari walikua na kikao cha kupanga mgomo mpya.
So mwanangu akawa amefariki kwenye mikono ya mamake,nilishukuru mungu kwa yote, sasa nikaanza utaratibu wa kutoa maiti kuipeleka mochwari,ilituchukua kama dk 40 hv kupewa kibali cha kuipeleka mochwari,still bado haikua problem sana kwangu.
Sasa kilichonikera na kunisikitisha ni baada ya kufika mochwari sikumkuta muhusika wa mochwari na sasa ikanibidi kuzunguka kumtafuta muhusika huku nikiwa nimeibeba maiti ya mwanangu mikononi,punde alifika ndg yangu mmoja niliyekua nimempigia simu aje kunichukua na gari yake bcoz wife tayari alikua ameshachanganyikiwa,so ilibidi mimi nikae kwenye mrango wa mochwari kwa takribani masaa hv ili kumsubili muhusika na ndg yangu huyo pia akaanza kumtafuta na kumpata baada ya masaa 2 hivi.
Baadae niligundua kwamba madaktari walikua bado wanaendelea na kikao cha mgomo uliopangwa kuanza j5 nchi nzima,
Sasa ni swali kwa wana JF, Jee kama hayo yanatokea muhimbili jee sisi tusio na uwezo wa kwenda INDIA tutapona kweli???
Naombeni comments.
Sidhani kwamba ni busara kulaumu maamuzi yaliyofanywa na mfiwa. Hakuna mzazi anayechelewesha kumpatia mtoto wake tiba..pole sana mzee,kwa ujumla inaonekana ulichelewa muda mwingi pale dispensary,ilitakiwa umuwahishe moja kwa moja muhimbili maana inaonekana alikua katika hali mbaya sana