Yaliyojiri Uchaguzi wa Ubunge Jimbo la Arusha mjini, Lema atangazwa mshindi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,561
217,865
Wakuu,

Natanguliza salamu , huu ni zaidi ya uchaguzi, ni zaidi ya kuchagua, tupeane taarifa kuanzia maandalizi, ulinzi wa vituo pamoja na mwamko wa wananchi , hatua kwa hatua mpaka matokeo yatakapotangazwa.

Nakala kwa Crashwise na Ephata Nanyaro

====================

Kituo cha kupigia kura cha Faraja - Arusha mwamko si mkubwa kwa tulioko kituoni kwa sasa, tuko kama vijana 50.

Naamini bado watu watakuja, namtakia kila la heri Lema.

UCHAGUZI wa Ubunge kwa majimbo ya Handeni na Arusha Mjini uliopangwa kufanyika Desemba 13, mwaka huu, umefanyika salama baada ya kuahirishwa Oktoba 25, mwaka huu, huku idadi ya wapiga kura ikionekana kuwa ndogo tofauti na chaguzi nyingine.

Wananchi wa majimbo hayo ya Handeni na Arusha walianza kupiga kura asubuhi ya leo Desemba 13, mwaka huu, kuwachagua wabunge hao ambao watawawakilisha katika kipindi cha miaka mitano.

Lema atangazwa Mshindi

Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo la Arusha Mjini, Juma Idd, amemtangaza Mbunge Mteule wa Jimbo hilo kuwa ni Godbless Lema aliyeshinda kwa kura, 68,848 sawa na 65.9%, akifuatiwa kwa mbali na Philemon Mollel (CCM) kwa kura 35,907 sawa na 34.4% kati ya wapiga kura walioandikishwa 317,814 ambapo waliopiga kura walikuwa 105,800 sawa na 32.83% huku kura halali zikiwa 104,353 na kura zilizoharibika ni 1447.


Jimbo la Handeni Mjini

Wakati huo huo, wagombea watano kutoka vyama vya ADC, CCM, CHADEMA, CUF na TLP, wamesimama kugombea nafasi ya ubunge katika Jimbo la Handeni Mjini mkoani Tanga kufuatia kifo cha aliyekuwa mgombea wa Jimbo hilo marehemu Dk. Abdallah Kigoda, kilichotokea siku chache kabla ya uchaguzi Oktoba 25, 2015.

CCM yaibuka mshindi Handeni

Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi huo mdogo katika jimbo hilo, Tweneth Haule, amesema idadi ya wagipga kura ilikuwa ndogo.

Msimamizi huyo wa uchaguzi amemtangaza, Omari Abdallah (CCM) kuwa mshindi wa uchaguzi huo kwa kupata kura 10,315 akifuatiwa kwa mbali na mgombea wa Chadema, Daudi kilo Lusewa, aliyepata kura 648. Idadi ya waliojiandikisha...........


Soma zaidi =>
Kiporo cha Majimbo ya Handeni na Arusha mjini, CCM na CHADEMA wagawana majimbo
 
Chadema itashinda Arusha mjini hapo sielewi kwa nini Mbunge wa Arumeru mashariki kaamua kukaa Kando kwny Josh kampen
 
Kituo cha kupigia kura cha Faraja - Arusha mwamko si mkubwa kwa tulioko kituoni kwa sasa, tuko kama vijana 50.

Naamini bado watu watakuja, namtakia kila la heri Lema.
 
Leo hii wana Arusha tunakwenda kutimiza tu wajibu wa kusimama mistari na kupaka rangi ya kucha kwenye vituo maalum maana tayari kama ni kupiga kura tayari tulisha mchagua mheshimiwa Lema kuwa mbunge wetu.
 
kituo cha sinoni shule ya msingi wapo wapo ila sip kama ule uchaguzi mkuu
 
Hivi mgombea wa ccm anaitwa nani? Alifanya kampeni kweli!!?
 
Kituo cha kupigia kura cha Faraja - Arusha mwamko si mkubwa kwa tulioko kituoni kwa sasa, tuko kama vijana 50.

Naamini bado watu watakuja, namtakia kila la heri Lema.

Hapo kuna heart voters 101 wa CCM wapo njiani wanakuja kufunga hesabu
 
Huyu ndio Mollel Chaguo letu wana A town
Mungu amsaidie sana maana tunaenda kupata mkombozi Kwa vizazi vyetu vijavyo Arusha
 

Attachments

  • 1449980690307.jpg
    1449980690307.jpg
    27.9 KB · Views: 2,359
Back
Top Bottom