Yaliyojiri: Kongamano la Katiba: 15 Januari 2011 Nkrumah UDSM

Nyerere alikiri katiba inamfanya awe "dikteta", Mzee Shivji anamwaga vitu.
 
Katiba zote hazikuwa na uhalali wa kisiasa kwa kuwa wananchi hawakushiriki katika michakato ya katiba hizo.Shivji anasema pamoja na hayo,Uongozi wa Mwalimu ulikuwa halali kutokana na itikadi ya chama na uwezo na umarufu wake binafsi.Mwalimu Nyerere mwenyewe amewahi kusema chini ya katiba hii,angeweza kuwa dikteta.
 
Kweli mkuu mpaka kilaza ZOMBA kamuona ujue huyo ni kichwa kwelikweli!!

For your information, Zomba alikuwepo katika kongamano la katiba la mwaka 1990. Sijui kama ulikuwa umesha zaliwa.
 
huyo kombani akamtafute babu yake aendeleze hule utani aliosema,,miaka stini na nne bado wanaendekeza utaani,sisi tuko serious utani hatutaki,utni utafanya na mkwere kwa muda wenu
 
Mapendekezo ya shivji:majadiliano ya katiba yawe katika stage mbili
1.mijadala midogo
2.bunge au tume
 
For your information, Zomba alikuwepo katika kongamano la katiba la mwaka 1990. Sijui kama ulikuwa umesha zaliwa.
Kuwepo kwenye kongamano si tija ila kuendelea kuwa mtumwa wa fikra za kitumwa ndiyo tija.
 
Shivji anapendekeza kuwa mchakato wa katiba mpya uwe na hatua mbili,hatua ya kisiasa na hatua ya kisheria.Lazima kuwe na mjadala wa wazi kwa kila sehemu kwa kila mtu.Kuwe na Tume yakuratibu mchakato maoni kutoka kwa wananchi.Baada ya hapo kuwe na Mkutano Maalumu na mwisho kuwe na kura ya maoni kutoka kwa wananchi.

Shivji anasema ana wasiwasi na Tume itakayoundwa na rais,hasa katika watu watakaounda tume hiyo,hadidu za rejea na kwamba mapendekezo ya tume hiyo yatapelekwa wapi.
 
wapi SPIDERMAN?? jamaa huyu cjui ana program ya kuandika kama mtu anakuwa anaongea? maana speed yake ni kama machine
 
Shivji anapendekeza kuwa mchakato wa katiba mpya uwe na hatua mbili,hatua ya kisiasa na hatua ya kisheria.Lazima kuwe na mjadala wa wazi kwa kila sehemu kwa kila mtu.Kuwe na Tume yakuratibu mchakato maoni kutoka kwa wananchi.Baada ya hapo kuwe na Mkutano Maalumu na mwisho kuwe na kura ya maoni kutoka kwa wananchi.

Shivji anasema ana wasiwasi na Tume itakayoundwa na rais,hasa katika watu watakaounda tume hiyo,hadidu za rejea na kwamba mapendekezo ya tume hiyo yatapelekwa wapi.

Hapo Prof Kanena
 
jenerali ulimwengu ameanza kwa kumpiga kijembe chenge kwa kuendesha gari lisilo na insurance.anasema katiba yetu misingi yake ni ya uingereza
 
Back
Top Bottom