Yaliyojiri Diamond Jubelee Tamko la Waislam - Video

Mohamed Shossi,

..kuna mchangiaji alitoa ufafanuzi kuhusu mchakato mzima uliopelekea serikali na mashirika ya Kikristo kusaini MOU.

..mchango wake nimeuweka hapa, na ulikuwa kwenye thread mahsusi iliyohusu MOU hapa jamiiforums.

Katibu wa TEC said:
Nashukuru mwana JF aliyeweka hadharani MOU husika. Ningependa tu kuongezea machache na hasa historia ya jinsi na kwanini MOU hiyo ilizaliwa:-

i) Wote mtakumbuka kuwa huko nyuma Serikali ilitaifisha Shule na nyingi za madhehebu ya Dini. Utaifishaji huo uliendana pia na Ardhi, hasa ikizingatiwa kuwa wakati shule zinajengwa zilijengwa kwenye maeneo ya madhehebu ya dini na papo hapo kukukiwa na kanisa, nyumba za mapadre na kadhalika. Hii ilikuwa hivyo kwa shule nyingi za Middle School( Model Schools, Upper Primary kama mnavyojua majina yalibadilika sana kati ya 1962 hadi 1965 hivi na ndipo pia mtihani au darasa la nane lilipofutwa rasmi).

2) Kwenye miaka ya 1980 madhehebu yakataka warudishiwe ardhi yao, hasa ardhi ambayo ina majengo mengine yasiyohusiana na shule hizo. Mchakato wa mjadala ulishika kasi, mwaka 1986 Baraza la Maaskofu Katoliki TEC, lilipopitisha azimio rasmi,na kumtaka Katibu Mkuu, awasiliane na Serikali, kuanzisha mchakato wa kufanya survey na kutenga ardhi ya shule rasmi kutoka kwenye ardhi inayotumika kwa huduma nyinginezo za madhehebu ya dini. Wakati huo mimi ndiye nilikuwa Katibu Mkuu wa TEC baada ya kupokea rasmi kazi hiyo December, 1985. Wakati huo madhehebu yaliisha kudai yarudishiwe Shule zao kwa kuwa zimegeuka kuwa aibu kwa kukosa ukarabati, na ziko kwenye hali mbaya sana. Serikali ilikuwa imekataa ombi hilo kwa lengo la kuwa Shule hizo zinawahudumia watanzania wote bila ubaguzi, jambo ambalo ndilo lilikuwa lengo kuu la utaifishaji, na sababu ya utaifishaji ilikuwa bado inaendelelea.

3) Wakati mawasiliano yalipoanza na Serikali wakati huo kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Elimu, Serikali iliomba TEC na madhehebu ya Dini kwa ujumla, kama yanaweza kusaidia ukarabati wa shule hizo kwa kuwa ziko kwenye hali mbaya na hali ya uchumi wa nchi haikuwa nzuri na hivyo mapato ya Serikali.

4) Wakati mchakato huo kwa upande wa Elimu umeanza kulikuwa pia na mgogoro kati ya Serikali na TEC baada ya Serikali kuichukua Hospitali ya Bugando almost kwa utaratibu huo huo wa kuitaifisha. Hospitali hiyo ilikuwa kwenye awamu ya Pili ya ujenzi kwa msaada mkubwa wa Shirika la Misereor( Shirika la Maendeleo la Baraza la Maaskofu Katoliki la Ujerumani) toka Ujerumani.

5) Katibu Mkuu wa TEC alipowasiliana na Wahisani walikataa kata kata kujihusisha tena na ujenzi au ukarabati wa Shule au Hospitali ( Hospitali, vituo vya Afya na zahanati) kwa kuhofia kuwa Serikali ya Tanzania imekuwa ikitaifisha huduma hizo bila majadiliano ya aina yeyte, na hawawezi kuwekeza fedha za walipa kodi wao ( ujerumani Madhehebu ya dini yanapata fedha rasmi kutoka kodi ya wananchi) kwa ratio waliyokubaliana kuendana na idadi ya madhehebu ya dini. Lakini walikuwa tayari kuendelea na huduma mbalimbali za kusaidia madawa na elimu kwa shule zilizoko bado chini ya madhehebu kwa kuwa hawawezi kuwaadhibu wananchi na watoto.

6) Kwa kuwa shughuli zote za Bugando zilikuwa zinaelekea kusimama na kulikuwa na mgomo kila siku, kwa madaktari na manesi na watumishi, Serikali ikaomba tujadiliane upya juu ya mambo makubwa mawili a) Utoaji huduma katika sekta za huduma za Jamii, b) Kuwa na chombo cha mawasiliano na majadiliano kati ya Ikulu na madhehebu ya dini, na kwa kuwa madhehebu ni mengi wakaomba chombo hicho kiundwe na viongozi wakuu wa madhehebu yaliyokuwa yanajulikana kwa mujibu wa Sheria, hivyo Bakwata ( Waislamu- sitaki kuingia kwenye mjadala wa kama Bakwata ni chombo kinachowasilisha waislamu au la), Tanzania Episcopal Conference TEC na CCT ( kwa madhehebu zaidi ya 60 yaliyoko chini ya Christian Council of Tanzania) .

Baada ya Mashauriano tuliunda chombo hicho kikiwakilishwa na Mwenyekiti na Katibu wa vyomb o nilivyovitaja hapo juu. Uratibu ulikuwa unabadilika kila mwaka katika ya madhehebu hayo, vivyo hivyo kwa Sekretariat. Kutokana na utaratibu huo tuliweza kupatia ufumbuzi matatizo yaliyokuwa yakijitokeza mara kwa mara na ikawa rahisi kwa Serikali kuwasiliana na chombo hicho badala ya kila dhehebu peke yake, na kwa upande wetu pia chombo hicho kikatupa nguvu ya kujadiliana na serikali (power of negotiation).

7) Kutokana na hali mbaya ya Shule Serikali, ikaomba madhehebu ya dini kusaidia ukarabati wa shule zilizoonekana zitafungwa kutokana na hali mbaya , nasi kwa upande wetu kwa nia njema ya kuisaidia Serikali lakini pia kuwahudumia watanzania tuliwasiliana na Wahisani ambao walikazia msimamo wao kuwa hawako tayari kuingia kwenye shughuli za ujenzi wala ukarabati kwa kukosa msimamo wa wazi na au wa kisheria wa Serikali ya Tanzania kuhusiana na utaifishaji wa huduma hizo.

Serikali ilipojulishwa, ilichukua hatua ya kuanzisha mchakato mzima wa kupata suluhu ya jambo hilo. Ndipo akapewa jukumu hilo, Mhe. Anne Makinda wakati huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, na mkutano wa kwanza ulifanyika Kurasini Conference Centre (TEC) Mikutano ya baadaye ilikuwa ina alternate kati ya TEC na CCT. Hii ni kwa sababu huduma zilizokuwa zinajadiliwa ni za TEC na CCT ( ambao walikuwa wameathirika na utaifishaji huo). Hatimaye, Serikali ilikubali kuwa haitataifisha tena, na kwa kuthibitisha hivyo, ikawa tayari kuwekeana MOU na madhehebu ya Dini.

Ndipo tukaanzisha mchakato wa majadiliano na Wahisani, na wahisani, nao katika umoja wao kati ya dhehebu la kikatoliki Ujerumani na Kilutheri pia la Ujerumani tukaanzisha mchakato wa namna bora ya kutoa huduama za jamii. Daima Serikali ilishirikishwa kama Observer katika michakato hiyo, na kwa upande wa Ujerumani Serikali yao nayo ilishirikishwa katika timu za majadiliano. Hatimaye, makubaliano yalifikiwa, na ndipo ikazaliwa chombo kipya Christian Social Services Commission (CSSC), chenye Secretariat yake ( Katibu Mtendaji wa kwanza akawa Dr. F.Kigadye aliyekuwa Mkurugenzi wa Bugando). Huduma za kilichokuwa Christian Medical Board (ya TEC na CCT ikavunjwa na kuwekwa chini ya CSSC) na idara za Elimu zilizokuwa chini ya TEC na CCT huduma zake zikaunganishwa na kuwekwa chini ya CSSC. Ndiyo MOU iliyosainiwa na Askofu Stanford Shauri wa Diocese ya Ruvuma, Mwenyekiti/Katibu Mkuu wa CCT wakati huo, na Askofu Josephat Lebulu, wakati huo Askofu wa Jimbo Katoliki la Same, na Mwenyekiti wa TEC. Kwa upande wa Serikali kama sikosei aliweka saini Mhe. Edward Lowassa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (au Waziri sikumbuki).

8) TEC na CCT nazo zikawekeana na Wahisani Mkataba MOU yao ya ndani ili kupata misaada ya ujenzi, ukarabati na uendelezaji wa huduma zote za jamii . Huduma hizo zinaendelea hata sasa japo sasa kwa kiwango kidogo baada ya mkataba wa awali kwisha.

Narudia tena, namshukuru sana aliyeweka kwenye JF MOU hiyo. Ninarudia kuwaomba wenzangu, tumetumia muda mrefu sana kujadiliana kwa hisia ya aina mbalimbali.

Watanzania hatukuzoea huko nyuma kuulizana dini zetu, wala kabila wala ukanda. Haya mambo tukiyaendekeza Taifa letu litakuwa hatarini. Tukumbuke kubomoa ni kazi nyepesi sana, sekunde lakini kujenga tena inachukua muda mrefu na ni kaz ngumu, na wakati mwingine hata ukifanikiwa huwezi kujenga kama ilivyokuwa.

Nashauri ili JF ibaki na heshima yake ya Home of Great Thinkers tupende kufanya Research zaidi kabla ya kulaumiana au kuhisiana, kama mtu hana taarifa za kina awaombe wenye taarifa.

Kama mnavyoona mimi nilikuwa nafahamu historia yote, nafahamu MOU, lakini sikuwa nayo. Mtu huwezi kujua kila kitu na au kuwa na kila kitu, we need to complement each other. Tunaweza tukidhamiria, na JF itabaki na hadhi na heshima yake daima.
 
Asante Mkuu JokaKuu kwa kuiweka hii. Lakini sidhani kama itasaidia sana kwa mtu ambae anaweza kudiriki kusema kuwa serikali ilikuwa inazipa makanisa pesa za kujenga shule na hospitali. Mtu ambaye ana victim mentality ni vigumu kuiondoa hata umwambie nini.

Amandla........
 
Fundi Mchundo said:

Fundi Mchundo,

..kuna hospitali za kanisa zina miaka 100 tangu kuanzishwa.

..sasa ni vizuri hawa wenzetu wakafanya utafiti kabla ya kutoa madai yao.

..nadhani wengi siyo wa huku Tanzania bara. yuko mmoja, he was so brainwashed, ilinichukua siku tatu nzima ku-prove kwake kwamba Tanganyika ilikuwa na mwanachama wa UN kabla ya Zanzibar.

..jambo lingine linalonishangaza ni kwamba MOU imesainiwa tangu 1992. sasa tangu wakati huo Waislamu[hili kundi la Shehe Basaleh,Ponda, etc] wamefanya juhudi gani kuboresha elimu na afya ktk "maeneo" yao.

..vilevile matajiri[Bakhresa,Mohamed Enterprise,Hilal,Oil Com,...] wakubwa wa nchi hii ni Waislamu. hivi kweli hawa wameshindwa kujenga walau shule 10 ambazo zitatoa elimu ya uhakika kwa vijana wa Kiislamu??

..nampongeza Mama Salma Kikwete kwa kujenga shule kijijini kwao Nyamisati. kamshinda hata JK ambaye alikuwa mbunge wa Bagamoyo for 15yrs and did not do anything to improve education or health services in his constituency.
 
Mimi naachukia zana mtu mlamikaji, mvivu na anaye taka starehe bila jasho. Nikiwa boss wako aise utanichukia111. napenda mtu mchapakazi, anaye jua kutatua matatizo na siyo kulalamika.

Kuna watu utakuta kila siku wanalalamika eti mwalimu anawaepndelea baadhi ya wanafunzi. Lakini chukua paper yake uone madudu anayo andika. Kama wewe unataka ukubaliwe na mwalimu fanya juhudi, wahi darasani kaa dawati la kwanza, uliza maswali yenye mwelekeo, kesha miguu kwenye maji ya baridi kama matango hayapandi.

Sasa hizi porojo zilizo letwa hapa, sinaweza kuwa za kweli lakini mambo mengi yalianadikwa hapa ni mawazo ya awtu wasio fanya kazi na wanataka vitu vya bwerere. Wanafikiri sikuwatatokea waarabu wawajengee shule utitiri na wataweza kuziendesha.

Angalia chad, waarabu walijenga misikiti kila mtaa, wale wenyeji (wavivu), wakajifanyia ndio ajira, kushinda hapo na kuweka sheria misikitini kila mzazi alete mtoto madrasa, mwisho wakaishia kuwafunga minyororo watoto wote ambao hawakufuata maelezo yao hadi wanaharakati wa kifaransa wakaingilia kati.

Huu ni mfano tuu, lakini ndugu zangu waslam, tusifikilie kusema, na kulalamika hivi ndiyo solution. sasa hivi nawapongeza kwa mwamko mlio uonyesha katika elimu na sector nyingine. Nyie wenyewe ni mashahidi, kuna watu hata elimu dunia hawana wanafikili kuwa endesha watu kwa kushinikiza habari kama hizi ndio jeuri. hakuna anaye tetewa hapa.

Ninngeona mnasema kuna shule, Chuo kikuu kimejengwa na serikali ikakipiga marufuku kwa sababu ni cha waislam basi ningekuwa wa kwanza kupinga hilo kwa nguvu zote. Au ningesikia kuna chuo kinawabagua waslam kweli kabisa ningefanya maandamano kwa ngucvu zote maana hakuna umuhimu wa kugombana wakati wote ni watoto wa baba mmoja, taifa moja ,a nchi moja.

Lakini mtu hajafauru, na analeta porojo ati kuna ubaguzi?? jamani hivi wapi tunakwenda. Tujifunze kwa wanao fanikiwa na sio kulalamika eti wachanga wezi wakati mwenzio kila siku anaamka saa kimi na moja asubuhi kukatia ng'ombe majani, wewe unapiga usingizi??.

Haya mambo yamwaharibu sana ndugu zetu waslam, wamepandikizwa mawazo yakijiona wananyanyasika wakati hakuna kitu kama hicho. Mtu anaomba kazi asipo itwa eti sababu ni muslam. kawni wakristo wangapi hawajaitwa??.

ebu tuamuke ndugu zetu, tufanye kazi, someni kwa nguvu zote vyuo vipo haijalishi ni chuo gani wewe piga shule, usaidie kuondoa fikra potofu kama hizi.

Unajua unaniumiza mtu kuona watiu wanataka kila kitu kiwe cha kislam. haita tokea katka nchi ama tanzania. Ube tushikamane tujenga taifa linalo suasua kama kobe mchonvu.

Sanmahani kama nimewakwaza.
 
kinachonishangaza ni mashekhe kulishupalia kanisa kwa kipindi hiki, sijui maskini wa Mungu limewakosea nini? Mie ninavyoona kukata mzizi wa fitna basi na nyie fungueni hospitali zenu na hizo huduma nyingine za jamii ili mfaidike na hiyo migawo, ila tu mkumbuke wenzenu hata shule wameenda hivyo hata miradi yao inakuwa endelevu haiwezi kufa. Hebu fikiria kusingekuwa na Bugando, KCMC Na nyinginezo nyingi sijui nchi ingekuwaje? Ungeniambia serikali itajenga, nikuulize mbona serikali imeshindwa kujenga ndani ya hii miaka 50 tangu uhuru hizi huduma za jamii?
Kwanza wanaolalamika ni genge la watu wachache tu na wanaoishi Dar, ungetuuliza sie tunaoishi huku mikoani makanisa yanavyotusaidia hasa mahospitali
Serikali imeshindwa kuboresha tu shule za kata za secondari, itakuwa mambo yote itaweza?
hata hivyo nchi inajengwa na watu wote ikiwamo na taasisi binafsi, kwa hiyo mie nawashangaa hawa ndugu zangu kukaa na hizi chuki ambazo hazina msingi. Haf kwenye hizo huduma za jamii wakristo kwa waislam, budha, wapagani wote tunachangia kwa hiyo si kwamba wakristo wanatibiwa bure!
Kwa upande wangu naona madai ya hawa ndugu hayana mshiko kabisa!

Itajenga lini wakati inagawa pesa kwa kanisa kwa siri na wazi? na imekuwa ikifanya hivyo tokea enzi za ukoloni? tunatibiwa wote kwa pesa lakini faida inachukuliwa na kanisa, si serikali wala muislamu anapata! msijifanye mna weza kujibu hoja ambazo hamjui nyie tulieni, uzuri ni kwamba hata waislamu waliokuwa hawajui kitu sasa wanapata kuelewa si issue ya basalehe wala ponda, na ndio mana hata akina Mohamed Idd wanasaidia kuwaelimisha watu, TUTAFIKA TU MNAPOTAKA TUFIKE NCHI NYINGI ZIMESHAFIKA
 
Tunaaibisha ndugu zangu.wenyewe tu waislamu tunapigana ndani ya misikiti,sasa kama tukiwa na nchi yetu peke yetu itakuwaje? Si itakuwa zaidi ya somalia. Chuki zisizo na survey nzuri hazijengi. Mtme alituasi tutafute elimu dunia vilevile.
Masalaam
 
Halafu mkuu kati ya yote uliyoandika hapo sijaona hata mmoja likimtaja kiongozi mkuu wa nchi kwa sasa ambaye ni muislamu.
Mbona membe siyo spika wa bunge kwa hizo tuhuma mlizo mpa?? Mbona wala hajawahi kua waziri wa sheria na katiba wala fedha??
Maamuzi makubwa hua yanafanywa na rais lakini kwenye tamko lenu sijaona mahali ambapo mmeonyesha kukerwa na ufanisi wake wa kazi!!
Mkuu kama wewe unaona mbali mi nakushauri achana na haya mambo pia ukiona mtu yeyote anapandikiza chuki kama hizi kemea milele.

Hivi hujaelewa kwamba yeye ndiye kaandika hilo tamko kwa hiyo anajaribu kulipromote hapa kwa thread mbalimbali? Tatizo hajagungua kwamba watu hapa wanafikiri, hawasikilizi na kuamini!
 
Tunaaibisha ndugu zangu.wenyewe tu waislamu tunapigana ndani ya misikiti,sasa kama tukiwa na nchi yetu peke yetu itakuwaje? Si itakuwa zaidi ya somalia. Chuki zisizo na survey nzuri hazijengi. Mtme alituasi tutafute elimu dunia vilevile.
Masalaam

Muislamu gani asiejua hata salam inavyotamkwa ! sasa masalaam ndio nini tena? ni mbadala wa Salaam alaikum au ulikusudia nini?
 
maneno ya waislam ni ya kweli na hayana mjadala, wakiristo wanazunguruka kwa nyuma kubeba mali za watz
 
maneno ya waislam ni ya kweli na hayana mjadala, wakiristo wanazunguruka kwa nyuma kubeba mali za watz

hivi algeria, tunisia, libya, yemeni, etc kuna wakristo nako wanao iba mali za wenzao????. Tulilete maneno yasiyo na msingi. Umaskini ni wa wote na hakuna anayefaidi. Fanya kazi tukomboe taifa na siyo kukaa eti tunaonewa.
 
itajenga lini wakati inagawa pesa kwa kanisa kwa siri na wazi? Na imekuwa ikifanya hivyo tokea enzi za ukoloni? Tunatibiwa wote kwa pesa lakini faida inachukuliwa na kanisa, si serikali wala muislamu anapata! Msijifanye mna weza kujibu hoja ambazo hamjui nyie tulieni, uzuri ni kwamba hata waislamu waliokuwa hawajui kitu sasa wanapata kuelewa si issue ya basalehe wala ponda, na ndio mana hata akina mohamed idd wanasaidia kuwaelimisha watu, tutafika tu mnapotaka tufike nchi nyingi zimeshafika

jamani tusilete mambo ili tuu kuonyesha ushindani.
 
Mimi naachukia zana mtu mlamikaji, mvivu na anaye taka starehe bila jasho. Nikiwa boss wako aise utanichukia111. napenda mtu mchapakazi, anaye jua kutatua matatizo na siyo kulalamika.

Kuna watu utakuta kila siku wanalalamika eti mwalimu anawaepndelea baadhi ya wanafunzi. Lakini chukua paper yake uone madudu anayo andika. Kama wewe unataka ukubaliwe na mwalimu fanya juhudi, wahi darasani kaa dawati la kwanza, uliza maswali yenye mwelekeo, kesha miguu kwenye maji ya baridi kama matango hayapandi.

Sasa hizi porojo zilizo letwa hapa, sinaweza kuwa za kweli lakini mambo mengi yalianadikwa hapa ni mawazo ya awtu wasio fanya kazi na wanataka vitu vya bwerere. Wanafikiri sikuwatatokea waarabu wawajengee shule utitiri na wataweza kuziendesha.

Angalia chad, waarabu walijenga misikiti kila mtaa, wale wenyeji (wavivu), wakajifanyia ndio ajira, kushinda hapo na kuweka sheria misikitini kila mzazi alete mtoto madrasa, mwisho wakaishia kuwafunga minyororo watoto wote ambao hawakufuata maelezo yao hadi wanaharakati wa kifaransa wakaingilia kati.

Huu ni mfano tuu, lakini ndugu zangu waslam, tusifikilie kusema, na kulalamika hivi ndiyo solution. sasa hivi nawapongeza kwa mwamko mlio uonyesha katika elimu na sector nyingine. Nyie wenyewe ni mashahidi, kuna watu hata elimu dunia hawana wanafikili kuwa endesha watu kwa kushinikiza habari kama hizi ndio jeuri. hakuna anaye tetewa hapa.

Ninngeona mnasema kuna shule, Chuo kikuu kimejengwa na serikali ikakipiga marufuku kwa sababu ni cha waislam basi ningekuwa wa kwanza kupinga hilo kwa nguvu zote. Au ningesikia kuna chuo kinawabagua waslam kweli kabisa ningefanya maandamano kwa ngucvu zote maana hakuna umuhimu wa kugombana wakati wote ni watoto wa baba mmoja, taifa moja ,a nchi moja.

Lakini mtu hajafauru, na analeta porojo ati kuna ubaguzi?? jamani hivi wapi tunakwenda. Tujifunze kwa wanao fanikiwa na sio kulalamika eti wachanga wezi wakati mwenzio kila siku anaamka saa kimi na moja asubuhi kukatia ng'ombe majani, wewe unapiga usingizi??.

Haya mambo yamwaharibu sana ndugu zetu waslam, wamepandikizwa mawazo yakijiona wananyanyasika wakati hakuna kitu kama hicho. Mtu anaomba kazi asipo itwa eti sababu ni muslam. kawni wakristo wangapi hawajaitwa??.

ebu tuamuke ndugu zetu, tufanye kazi, someni kwa nguvu zote vyuo vipo haijalishi ni chuo gani wewe piga shule, usaidie kuondoa fikra potofu kama hizi.

Unajua unaniumiza mtu kuona watiu wanataka kila kitu kiwe cha kislam. haita tokea katka nchi ama tanzania. Ube tushikamane tujenga taifa linalo suasua kama kobe mchonvu.

Sanmahani kama nimewakwaza.

Acha uzushi, hakuna anayetaka kila kitu kiwe cha kiislamu, dhulma mnayofanya dhidi ya raia hao haiwezi kupimwa kwa maneno yako ya kipuuzi, unaweza kuandika sana lakini hutaweza kujibu maswali ya msingi, kwa nini miongozo ya maaskofu inafanyiwa kazi kwa haraka na kila siku ni sahihi wakati kauli za wengine ni za kubezwa ? Kama ni kauli za kijinga wanazo maaskofu ambao walisema eti Kikwete ni Chaguo la mungu-walijuaje? ,kwa nini baada ya miaka 5 amekuwa sio chaguo la Mungu? kikwete kabadilika nini ? waliona nini wakati ule na hawaoni nini leo kwa kikwete? wamefeli kiroho na kiakili maana hata maono hawana!, watulie Tujadili kuondoa mfumo kristo ulioshamiri, tuondoe udini hata kwa mikono yetu, maana wao hawajui kama kuna udini kwa sababu unawanufaisha
 
Hawa Waislamu inaonekana kweli wapo nyuma. Alie hudhuria na kuendelea kufuata Uislamu wa namna hii ni tatizo kichwani...Kuna tofauti kuwa sana kati ya Waislamu waliosoma na wale waliokimbilia madrasa kama solution ya kujenga madaraja na kutoa huduma mahospitalini...failures zao ndizo zinaonekana na kama kuna vijana ambao wapo collage leo na wanasikiliza ujinga kama huu nawatakia kila la heri kwenye uradicals...Kama kuna mtu anashindwa ku-load yaliotokea Diamond hii itasadia:

Last edited by a moderator:
Acha uzushi, hakuna anayetaka kila kitu kiwe cha kiislamu, dhulma mnayofanya dhidi ya raia hao haiwezi kupimwa kwa maneno yako ya kipuuzi, unaweza kuandika sana lakini hutaweza kujibu maswali ya msingi, kwa nini miongozo ya maaskofu inafanyiwa kazi kwa haraka na kila siku ni sahihi wakati kauli za wengine ni za kubezwa ? Kama ni kauli za kijinga wanazo maaskofu ambao walisema eti Kikwete ni Chaguo la mungu-walijuaje? ,kwa nini baada ya miaka 5 amekuwa sio chaguo la Mungu? kikwete kabadilika nini ? waliona nini wakati ule na hawaoni nini leo kwa kikwete? wamefeli kiroho na kiakili maana hata maono hawana!, watulie Tujadili kuondoa mfumo kristo ulioshamiri, tuondoe udini hata kwa mikono yetu, maana wao hawajui kama kuna udini kwa sababu unawanufaisha

Kwani walio penda kikwete awe raisi 2005 walikuwa niwakristo pekee yake?? Na baada ya miaka mitano si kila mtu analalamika kuwa hajatimiza yale aliyo ahidi. Watu hawajaji kikwete ati kwa kuwa ni muislam, hata angekuwa ni mpaganim, au mkiristo bado kama raia tungekuwa na kumkosoa. Hivi huko tunisia waliko mtimua raisi kwa sababu ya masiha magumu ya raia nako kuna wakristo, au algeria wale waislam walio anzisha jihadi ilkuwa ni dhidi ya wakristo??. Tuache kupandikiza vitu ambavyo havita tusaidia. Na kama kuna jambo dai kama mtanzania .
 
Fundi Mchundo,

..kuna hospitali za kanisa zina miaka 100 tangu kuanzishwa.

..sasa ni vizuri hawa wenzetu wakafanya utafiti kabla ya kutoa madai yao.

..nadhani wengi siyo wa huku Tanzania bara. yuko mmoja, he was so brainwashed, ilinichukua siku tatu nzima ku-prove kwake kwamba Tanganyika ilikuwa na mwanachama wa UN kabla ya Zanzibar.

..jambo lingine linalonishangaza ni kwamba MOU imesainiwa tangu 1992. sasa tangu wakati huo Waislamu[hili kundi la Shehe Basaleh,Ponda, etc] wamefanya juhudi gani kuboresha elimu na afya ktk "maeneo" yao.

..vilevile matajiri[Bakhresa,Mohamed Enterprise,Hilal,Oil Com,...] wakubwa wa nchi hii ni Waislamu. hivi kweli hawa wameshindwa kujenga walau shule 10 ambazo zitatoa elimu ya uhakika kwa vijana wa Kiislamu??

..nampongeza Mama Salma Kikwete kwa kujenga shule kijijini kwao Nyamisati. kamshinda hata JK ambaye alikuwa mbunge wa Bagamoyo for 15yrs and did not do anything to improve education or health services in his constituency.

Fedha wanazo nyingi tu, lakini mashariti yake ni magumu sana sana, kwa kitu kinachoitwa maendeleo.
 
Acha uzushi, hakuna anayetaka kila kitu kiwe cha kiislamu, dhulma mnayofanya dhidi ya raia hao haiwezi kupimwa kwa maneno yako ya kipuuzi, unaweza kuandika sana lakini hutaweza kujibu maswali ya msingi, kwa nini miongozo ya maaskofu inafanyiwa kazi kwa haraka na kila siku ni sahihi wakati kauli za wengine ni za kubezwa ? Kama ni kauli za kijinga wanazo maaskofu ambao walisema eti Kikwete ni Chaguo la mungu-walijuaje? ,kwa nini baada ya miaka 5 amekuwa sio chaguo la Mungu? kikwete kabadilika nini ? waliona nini wakati ule na hawaoni nini leo kwa kikwete? wamefeli kiroho na kiakili maana hata maono hawana!, watulie Tujadili kuondoa mfumo kristo ulioshamiri, tuondoe udini hata kwa mikono yetu, maana wao hawajui kama kuna udini kwa sababu unawanufaisha

Kweli Huyu ni Maskini wa mawazo...nipe mafanikio ya serikali na uongozi wa Kikwete? Siku zote baadhi ya waislamu inabaki nyuma kwa kuleta maneno ya ovyo badala kudiscuss matatizo ya Taifa Zima. JK alipochaguliwa wakristo wengi walimpigia kura na leo hamtaki tumpime na failures zake...huu ni ujinga kusikiliza mawazo ya kibaguzi na udini wenu...msituchafulie nchi yetu kwa kutojua jinsi ya kujenga Taifa letu. Maendeleo ya elimu bora, huduma bora mahospitalini, ajira kwa watanzania ni haki ya kila mtanzania sio muislam au mkristo. Hii kweli inadhihirisha jinsi gani waote mliohudhuria Diamond na wote mnaendelea kufuata maneno ya hao mlio wasikiliza ni just another radicals...
 
Ndg zangu mimi nadhani kuna kitu tunakizunguka hapa! Siyo Kanisa wala serikali.Tukinyoosha ni kwamba ni kwa muda mrefu sasa Ndg zetu Waislamu wamekuwa wakilalamikia kuonewa.Mara zote madai yamekuwa ni kubaguliwa,kutotendewa haki,mara wakristo wanapendelewa! hii ni ajabu sana! Nilianza kuhisi kwa sasa wanafikiria na wanaelewa hali ikoje kumbe bado.
Nianze kusema kuwa hamna anayeonewa hapa wala hakuna anyembagua mtu! Membe akitwa anweza kuitwa kama muumini pia! na ieleweke ana haki ya kikatiba ya kukutana na yeyote mradi asivuje sheria. Lakini pia Nani anweza kusimama hadharani akaeleza Membe aliitiwa nini? na kama Membe aliitwa kwa sababu ansuasua katika imani yake je? Siyo vizuri KUHISI KITU.Turaise hoja pale penye data,ukweli na hakika.Itamaanisha tumekuwa na tumeelimika na kustaarabika.
Kumekuwa na madai kama hayo ya kanisa kupendelewa>hebu aje mtu na data kuwa kanisa fulani limepewa fedha na serikali ili lijenge shule fulani. That I'm Sure hakuna anayeweza kufanya! Hata huyo rais feki hatajaribu! Hii ilitokana tu na watu flani kuhisi tu kuwa inawezekana ikawa hivi na bila data wakaanza kuwajaza ujing wenzao ambao nao bila kufikiria wakaaza kupiga kelele kama hizo.Kimsingi huko ni kujidhalilisha. Wakati tutakapoanza kuhoji ni kwa nini hawa wtu hawaonyeshi kukua miaka yote msione tunawatusi. KAMA KUNA MTU ANAJUA KUWA SERIKALI IMEGAWA PESA KANISANI NA ANA USHAHIDI HII INAWEZA KUSIKILIZWA HATA MAHAKAMANI!
Wakati flani nilisikia Waislamu wakidai wanafelishwa makusudi ili wasisome! Hivi ni kweli inawezekanaje hao walim waislam wanaokuwekpo kwenye marking wasiseme? Nina uhakika kama hivi tu hakuna data watu wazima tena wenye nafasi zao wanaropoka vitu vya kitoto wangepewa agizo hilo la kufelisha wangesema mapema mno! But this I'm sure kuwa Waisalam wamekuwa nyuma kielimu kwa sababu msisitizo umewekwa kwenye Elim Akhera kuliko Elim Dunia. Na hii hata wewe kaka Mohamed unajua sielewi ni kwa nini unaweza kujifanya houni! Kimsingi Takwimu mbalimbali zimekuwa zikionyesha kuwa hilo ni tatizo la Waislamu kidunia na ni kubwa zaid Kwenye mataifa ya Kiislam kuliko hata hapa. Kwa watanzania tuanze kwa kuangalia hizi shule zetu tu then eje mtu aseme tena kwa sauti Ikiwezekana Nitapenda Mashekhe watoe tamko kuwa Mpaka huko kwenye seminary zao wanakatazwa kufundisha vizuri!
Na hii ya shule ndiyo inayozaa matatizo yote. Nikasikia Viongozi wa kikristo ni wengi kuliko waislam. Sasa ndugu zangu tuanchagua viongozi kwa kuzingatia mambo mengi ikiwemo elimu,busara na hata uzoefu.Tuliposema tukaanze darasa la kwanza wegine wakakimbilia Madrasa.Walipolazimishwa kwenda shule wakahimizwa kushika Kwa nguvu Elim Akhera! Leo tunataka viongozi angalau wenye kaelimu kadogo,wengie wanategemeaje sijui.Hivi nikweli kuna anyedhani kuna mtu atauliza umesoma mpaka Juzuu ya ngapi? Hivi na hili halionekani jamani? Kulikuwa nahaja ya kulalamikiana na kusingiziana?
Sasa hapa nimepata mpya kwamba "Pengo amemwita Membe amekwenda sisi tumemfuata Membe amesema hana nafasi". Kwani swala ni kumfuata au ni Kuwa na nafasi? Mimi naona jibu lilikuwa wazi tu:Membe hakuwa na nafasi Basi.Hili halikuwa swala la kujikusanya na kuanza kupiga kelele za kuonewa> Ilitakiwa tu Aulizwe PS wa Membe Bosi ana nafasi lini Wapewe appointment wasikilizwe basi. Sasa esho tutafuta viongozi tena kwa kigezo kama hiki cha busara nyie mnaonaje ipo hapo hata harufu ya busara? JUST SEE IT BY YOURSELF! IPO? Aje mtu aseme Membe alikataa kutuona Kwa sababu ni Waislam na ni forever hataki tutakuelewa siyo hiyo ya kukosa nafasi jamani!
Nasikia sasa Serikali imetoa pesa kanisani wajenge shule. Hivi tunaongelea ruzuku au fedha tofauti? Nijuavyo mimi ruzuku wanapata wote wala tusipotose umma hapa. Vinginevyo Hata kama uwe huna aibu kama ilivyo serikali ya CCM bado huwezi kijenge shule au hospital;i kanisa au Msikiti. Sijui nani kawadanganya. Na kwa ninavyojua hakuna uthibitisho licha ya kuwa kwenye serikali hiyohiyo wapo na Waislamu na hawatawasaidia kwa data hizo coz HAZIPO!
BINAFSI naona kuna kinachozungukwa na wenzetu hawa.Siyo Pesa kanisani,siyo elimu wala upendeleo walolote! Just angalieni swala hili limekurupuka msimu upi then mtaona pamoja na mimi hiki ninachokiona sasa.Hili swala limeanza baada ya wizi wa kura Arusha na Mauaji ya Polisi na haswa tatizo ni Maaskofu kushikia kidedea ishu hiyo! Hapo kwenye summery Hujasema Kiini cha malalamiko so wachangiaji wanashindwa kuelewa intesity ya hoja. Ukweli wa hoja yao nikuwa eti kwa nini Maaskofu wajidai wana uchungu sana na mauaji ya Arusha wakati Kule Zanzibar ni serikali hii hii iliyoua ila hawakusema kwa kuwa ilikuwa inaongozwa na Mkristo(Mkapa) Na kuwa mbona mwembe chai hawakusema lolote. Kwamba kimsingi sasa maaskofu wanapiga kelele kwa sababu tu Kiongozi ni Mwislamu!
Jamani tuwe tunafikiria kabala ya kukurupuka na hoja.Ni Vibaya sana ku acuse kwa hoja isiyo na mwelekeo kama hiyo. Tukisemea ya 2001 Zanzibar, hivi kuna mtu anaweza kusema hadharani kwa sauti kwamba waliokufa pale ni waislamu? Au kuwa tu ni Zenj basi tua imani kuwa wote ni waislamu na walionewa na rais mkristo na maaskofu wakafurahia tu. Waulizeni waliotoka Zanzibar,hata kule kuna makanisa jamani. May be mtuaseme waliokuwa targeted ni waislam tu na aje na data Otherwise ni mambo ya kitoto kulazimisha hilo.
Hata ilipokuja ya Mwembechai bado nashukuru kuwa wanaokumbuka watasema kuwa ulikuwa ni mkusanyiko uliokuwa HAUJARUHUSIWA(tofauti na Arusha), Na Mbya ulikuwa wa kidini wa kushinikiza watazania wkubali madai yale yale ninayosema yaliyokosadata namwelekeo,madai ya kunyimwa uhuru wa kuabudu ingawa hakuzuiwa mtu kwenda msikitini,madai ya kupewa haki ya kuvunja mabucha ya Nguruwe bila kujali hii siyo nchi ya kiislam, na bado wanadai Maaskofu wangekuwa wamesemea na hilo!!!!!!!Nashukuru pale Mwembechai alikuwepo ndugu yenu mpendwa Yusuph bin Makamba na Ikulu alikaa Mheshimiwa sasa Alhaj Ally Bin Hassan!Hivi huwa tunaona mazingira yakoje lakini au ni kwa kuwa tumezoea kuongea tu. INA BORE!
Inaposemwa ishu ya OIC ikumbukwe kuwa siyo Waislam wala Wazanzibari wenye haki ya kuamua kujiunga na jumuiya yoyote.Hiyo ilitakiwa iwe hoja ya nchi kuamua kujiunga na ilikataliwa na Watanzania siyo Wakristo.Siyo kwa sababu OIC ni Mbaya ila kwa sababu ile ni Jumuiya ya nchi za Kiislam na nchi yetu siyo ya Kiislam.Bado utashangaa pamoja na kuwa ni swala la wazi kabisa la kikatiba kuwa KATIBA YETU HAINGERUHUSU ZANZIBAR KUJIUNGA NA OIC KWA KUWA HATUNA NCHI YA ZANZIBAR,ukona watu wadai wanaonewa!
I really hate to be talking about beliefs and differeces in faith coz this goes into some dirty ditches and we know it! Ila wakati mwingine nachukia upotoshaji na kudanganyana. Ukiamua kupiga kelele kuwa mkweli tu. Tusilazimishe nchi kuwa ya KIISLAMU! Tuheshimu Imani zingine pia!
I'm sorry I had to say this lakini napenda kuelimisha na kama nimekosea nikosolewe........................No Offence.
 
ndg zangu mimi nadhani kuna kitu tunakizunguka hapa! Siyo kanisa wala serikali.tukinyoosha ni kwamba ni kwa muda mrefu sasa ndg zetu waislamu wamekuwa wakilalamikia kuonewa.mara zote madai yamekuwa ni kubaguliwa,kutotendewa haki,mara wakristo wanapendelewa! Hii ni ajabu sana! Nilianza kuhisi kwa sasa wanafikiria na wanaelewa hali ikoje kumbe bado.
nianze kusema kuwa hamna anayeonewa hapa wala hakuna anyembagua mtu! Membe akitwa anweza kuitwa kama muumini pia! Na ieleweke ana haki ya kikatiba ya kukutana na yeyote mradi asivuje sheria. Lakini pia nani anweza kusimama hadharani akaeleza membe aliitiwa nini? Na kama membe aliitwa kwa sababu ansuasua katika imani yake je? Siyo vizuri kuhisi kitu.turaise hoja pale penye data,ukweli na hakika.itamaanisha tumekuwa na tumeelimika na kustaarabika.
kumekuwa na madai kama hayo ya kanisa kupendelewa>hebu aje mtu na data kuwa kanisa fulani limepewa fedha na serikali ili lijenge shule fulani. That i'm sure hakuna anayeweza kufanya! Hata huyo rais feki hatajaribu! Hii ilitokana tu na watu flani kuhisi tu kuwa inawezekana ikawa hivi na bila data wakaanza kuwajaza ujing wenzao ambao nao bila kufikiria wakaaza kupiga kelele kama hizo.kimsingi huko ni kujidhalilisha. Wakati tutakapoanza kuhoji ni kwa nini hawa wtu hawaonyeshi kukua miaka yote msione tunawatusi. Kama kuna mtu anajua kuwa serikali iegawa pesa kanisani na ana ushahidi hii inaweza kusikilizwa hata mahakamani!
wakati flani nilisikia waislamu wakidai wanafelishwa makusudi ili wasisome! Hivi ni kweli inawezekanaje hao walim waislam wanaokuwekpo kwenye marking wasiseme? Nina uhakika kama hivi tu hakuna data watu wazima tena wenye nafasi zao wanaropoka vitu vya kitoto wangepewa agizo hilo la kufelisha wangesema mapema mno! But this i'm sure kuwa waisalam wamekuwa nyuma kielimu kwa sababu msisitizo umewekwa kwenye elim akhera kuliko elim dunia. Na hii hata wewe kaka mohamed unajua sielewi ni kwa nini unaweza kujifanya houni! Kimsingi takwimu mbalimbali zimekuwa zikionyesha kuwa hilo ni tatizo la waislamu kidunia na ni kubwa zaid kwenye mataifa ya kiislam kuliko hata hapa. Kwa watanzania tuanze kwa kuangalia hizi shule zetu tu then eje mtu aseme tena kwa sauti ikiwezekana nitapenda mashekhe watoe tamko kuwa mpaka huko kwenye seminary zao wanakatazwa kufundisha vizuri!
na hii ya shule ndiyo inayozaa matatizo yote. Nikasikia viongozi wa kikristo ni wengi kuliko waislam. Sasa ndugu zangu tuanchagua viongozi kwa kuzingatia mambo mengi ikiwemo elimu,busara na hata uzoefu.tuliposema tukaanze darasa la kwanza wegine wakakimbilia madrasa.walipolazimishwa kwenda shule wakahimizwa kushika kwa nguvu elim akhera! Leo tunataka viongozi angalau wenye kaelimu kadogo,wengie wanategemeaje sijui.hivi nikweli kuna anyedhani kuna mtu atauliza umesoma mpaka juzuu ya ngapi? Hivi na hili halionekani jamani? Kulikuwa nahaja ya kulalamikiana na kusingiziana?
sasa hapa nimepata mpya kwamba "pengo amemwita membe amekwenda sisi tumemfuata membe amesema hana nafasi". Kwani swala ni kumfuata au ni kuwa na nafasi? Mimi naona jibu lilikuwa wazi tu:membe hakuwa na nafasi basi.hili halikuwa swala la kujikusanya na kuanza kupiga kelele za kuonewa> ilitakiwa tu aulizwe ps wa membe bosi ana nafasi lini wapewe appointment wasikilizwe basi. Sasa esho tutafuta viongozi tena kwa kigezo kama hiki cha busara nyie mnaonaje ipo hapo hata harufu ya busara? Just see it by yourself! Ipo? Aje mtu aseme membe alikataa kutuona kwa sababu ni waislam na ni forever hataki tutakuelewa siyo hiyo ya kukosa nafasi jamani!
nasikia sasa serikali imetoa pesa kanisani wajenge shule. Hivi tunaongelea ruzuku au fedha tofauti? nijuavyo mimi ruzuku wanapata wote wala tusipotose umma hapa. Vinginevyo hata kama uwe huna aibu kama ilivyo serikali ya ccm bado huwezi kijenge shule au hospital;i kanisa au msikiti. Sijui nani kawadanganya. Na kwa ninavyojua hakuna uthibitisho licha ya kuwa kwenye serikali hiyohiyo wapo na waislamu na hawatawasaidia kwa data hizo coz hazipo!
binafsi naona kuna kinachozungukwa na wenzetu hawa.siyo pesa kanisani,siyo elimu wala upendeleo walolote! Just angalieni swala hili limekurupuka msimu upi then mtaona pamoja na mimi hiki ninachokiona sasa.hili swala limeanza baada ya wizi wa kura arusha na mauaji ya polisi na haswa tatizo ni maaskofu kushikia kidedea ishu hiyo! Hapo kwenye summery hujasema kiini cha malalamiko so wachangiaji wanashindwa kuelewa intesity ya hoja. Ukweli wa hoja yao nikuwa eti kwa nini maaskofu wajidai wana uchungu sana na mauaji ya arusha wakati kule zanzibar ni serikali hii hii iliyoua ila hawakusema kwa kuwa ilikuwa inaongozwa na mkristo(mkapa) na kuwa mbona mwembe chai hawakusema lolote.
jamani tuwe tunafikiria kabala ya kukurupuka na hoja.ni vibaya sana ku acuse kwa hoja isiyo na mwelekeo kama hiyo. Tukisemea ya 2001 zanzibar, hivi kuna mtu anaweza kusema hadharani kwa sauti kwamba waliokufa pale ni waislamu? Au kuwa tu ni zenj basi tua imani kuwa wote ni waislamu na walionewa na rais mkristo na maaskofu wakafurahia tu. Waulizeni waliotoka zanzibar,hata kule kuna makanisa jamani. May be mtuaseme waliokuwa targeted ni waislam tu na aje na data otherwise ni mambo ya kitoto kulazimisha hilo.
hata ilipokuja ya mwembechai bado nashukuru kuwa wanaokumbuka watasema kuwa ulikuwa ni mkusanyiko uliokuwa haujaruhusiwa(tofauti na arusha), na mbya ulikuwa wa kidini wa kushinikiza watazania wkubali madai yale yale ninayosema yaliyokosadata namwelekeo,madai ya kunyimwa uhuru wa kuabudu ingawa hakuzuiwa mtu kwenda msikitini,madai ya kupewa haki ya kuvunja mabucha ya nguruwe bila kujali hii siyo nchi ya kiislam, na bado wanadai maaskofu wangekuwa wamesemea na hilo!!!!!!!nashukuru pale mwembechai alikuwepo ndugu yenu mpendwa yusuph bin makamba na ikulu alikaa mheshimiwa sasa alhaj ally bin hassan!hivi huwa tunaona mazingira yakoje lakini au ni kwa kuwa tumezoea kuongea tu. Ina bore!
inaposemwa ishu ya oic ikumbukwe kuwa siyo waislam wala wazanzibari wenye haki ya kuamua kujiunga na jumuiya yoyote.hiyo ilitakiwa iwe hoja ya nchi kuamua kujiunga na ilikataliwa na watanzania siyo wakristo.siyo kwa sababu oic ni mbaya ila kwa sababu ile ni jumuiya ya nchi za kiislam na nchi yetu siyo ya kiislam.bado utashangaa pamoja na kuwa ni swala la wazi kabisa la kikatiba kuwa katiba yetu haingeruhusu zanzibar kujiunga na oic kwa kuwa hatuna nchi ya zanzibar,ukona watu wadai wanaonewa!
i really hate to be talking about beliefs and differeces in faith coz this goes into some dirty ditches and we know it! Ila wakati mwingine nachukia upotoshaji na kudanganyana. Ukiamua kupiga kelele kuwa mkweli tu. Tusilazimishe nchi kuwa ya kiislamu! Tuheshimu imani zingine pia!
i'm sorry i had to say this lakini napenda kuelimisha na kama nimekosea nikosolewe........................no offence.

mvivu hata kufikili hawezi, na siku zote ni mlalamikaji. Wafanye kazi waone kama hawata fanikiwa. Sio kushinda manzese .
 
Itajenga lini wakati inagawa pesa kwa kanisa kwa siri na wazi? na imekuwa ikifanya hivyo tokea enzi za ukoloni? tunatibiwa wote kwa pesa lakini faida inachukuliwa na kanisa, si serikali wala muislamu anapata! msijifanye mna weza kujibu hoja ambazo hamjui nyie tulieni, uzuri ni kwamba hata waislamu waliokuwa hawajui kitu sasa wanapata kuelewa si issue ya basalehe wala ponda, na ndio mana hata akina Mohamed Idd wanasaidia kuwaelimisha watu, TUTAFIKA TU MNAPOTAKA TUFIKE NCHI NYINGI ZIMESHAFIKA

Si nilikuambia, Mkuu JokaKuu? Watu wengine hata uwaambie vipi bado hawatakubali maana kukubali ni kukubali udhaifu wao wenyewe!

Amandla........
 
Back
Top Bottom