Yaliyojiri: BUNGE Maalum la Katiba - TBC LIVE - Feb 18, 2014

Cybercrime

JF-Expert Member
Feb 14, 2014
3,246
1,113
Fuatilia live hivi sasa kutoka Dodoma, limeanza rasmi saa tisa kamili.

=== Updates====

Waliomba nafasi ya mwenyekiti Bunge la Katiba ni wajumbe watano. Kificho, Magdalena, Sadifa Juma Khamis, David Mbatia, Profesa Mahalu.

Kati ya hao, wanne wametimiza vigezo. Ambao ni Kificho, Sadif Khamis, Magdalena na Mahalu,

Wagombea wa nafasi ya Uenyekiti wa Muda wa Bunge la Katiba wameanza kujieleza.

Mhe. Pandu A. Kificho anamwaga sera zake sasa
Maswali kwake.
1. Aeleze elimu yake na uzoefu wake katika masuala ya sheria.
Majibu: Elimu yangu ni kidato cha sita, Nina Diploma ya sheria kutoka IDM Mzumbe pamoja na uzoefu wmingine mbalimbali
2. Kigwanganllah anauliza: Kwa mujibu wa kanuni na sheria, mwenyekiti wa Muda hatoruhusiwa kugombea uenyekiti kamili wa bunge

Majibu: nimeamua kugombea nafasi hii na sina makusudio ya kugombea nafasi ya uenyekiti kamili

3. Swali: Mimi Musahani nikikupa kura utafurahi?
Majibu: Nimeomba kura zenu nitafurahi kupata kura
Sadifa Juma Hamis (Donge- Zanzibar) anamwaga sera zake na kuomba kura kwa wajumbe wa Bunge maalum la Katiba nafasi ya Uenyekiti wa Muda. Elimu yake ni Master ya Sheria. Anaomba kura na sasa ameamua kujitoa kugombea na kumwachia Mzee Pandu kuendelea kugombea kwa kumalizia 'Sikio halizidi Kichwa'

Anayefuata ni Magdalena Rebangilla, taaluma yake ni Mwanasheria. Elimu yake ni Shahada ya Uzamili ya Sheria. Uzoefu wake ni uongozi katika asasi nyingi za misaada ya sheria, mashirika ya kitaifa na kimataifa kama mwezeshaji (facilitator). Anaamini kwamba atakuwa mtu wa katikati ambaye hana ajenda ya chama chochote hivyo hatopendelea upande wowote
Anaomba kura kwa nafasi inayogombewa.

Silinde: Kuna utofauti gani wa kuendesha mikutano ya taasisi na mikutano kama hii yenye watu wa kada na nyanja tofauti?
Jibu. Anaelewa kuna tofauti baina ya mikutano ya taasisi na mikutano ya Bunge. Hivyo atakuwa makini na kuendesha kwa tahadhari akielewa utofauti huo ili tuweze kupata Katiba nzuri.

Massoud Chani: Je yupo tayari kusimamia kanuni na kuweka kichwani? Kwa sababu kila alichoongea hapo amekuwa anakisoma kwenye kijikaratasi.
Jibu: Kushika karatasi ni uzoefu wa wanasheria kwani tunaamini ktk jambo lililoandikwa, Pia kwa mwongozo uliopo kwamba utendaji wa mwenyekiti wa muda utaongozwa kwa ushauri wa wataalam waliopo.

Prof Costa Ricki Mahalu anajieleza wasifu wake ili aombe kura.
Anataaluma ya sheria ni profesa wa sheria na amewahi kuwa Mwanadiplomasia. Hivi sasa ni prof. wa sheria SAUT Mwanza, Pia ni Makamu Mkuu wa Chuo kukuu cha Bagamoyo. Ana uwezo wa kutafsiri sheria na kutoa miongozo inapohitajika.

Tundu Lisu: Kazi ya uenyekiti wa Muda ni pamoja na kusimamia, kutengeneza na kupitisha kanuni za Bunge maalumu. Ni misingi ipi mikuu inayohitaji kujenga kanuni hizo?
Majibu: Kwanza ni sheria yenyewe, vilevile umoja wetu wa tuliopo hapa.

Msabaha: Hiyo taaluma yake atawasaidiaje makundi maalumu ambao wamekuja humu? na pia mbona hajaomba kura?
Majibu: Mimi si mwanasiasa nashukuru kwa kukumbushwa kuomba kura, pili mimi ni mwanasheria hivyo nitatumia taratibu zilizopo bila kuwa na upendeleo

Swali: Ana uzoefu gani
Majibu: Shahada nyingi si hoja, bali ni uelewa na hekima ya Mungu. Nimekuwa Mwenyekiti wa mikutano mingi ya kitaifa na kimataifa, ujuzi huo utanisaidia kuongoza endapo nitachaguliwa

UTARATIBU:
Kwa kuwa kura ni ya siri, mbona hakujatengwa eneo la siri kwa shughuli hiyo?

Katibu wa Bunge anafafanua kwamba demokrasia ya Bunge ni kwamba kura yako ni siri yako. Hivyo kura zitapigwa kwa wabunge waliopo ndani ambao ni 548. Hivyo ametoa rai wagombea kuteua wawakilishi wao ktk kuhesabu kura.
Kura zimeanza kupigwa sasa

Magdalena amemteua Leticia Nyerere kusimamia kura zake

Prof. Mahalu amemteua Wenje kusimamia kura zake

Mbatia hakukidhi vigezo

Wabunge waliohesabiwa ni 548 lakini kura zilizopigwa ni 568 hivyo idadi hiyo imekosa maelezo ya ongezeko la idadi hiyo.
Katibu anashauri zoezi la kura lirudiwe.

Mbunge mmoja ameomba mwongozo kwamba Idadi ihesabiwe upya,

pia Mbunge mwingine anasema kuwa kwa kuwa idadi ya kura haijazidi idadi ya wajumbe wote wanaotakiwa kupiga kura.

Hoja nyingine ni wagombea kuulizwa kama wanaridhia idadi ya nyongeza.

Hoja nyingine ni kuzigawanya kura zilizozidi kwa wagombea ili zihesabiwe.

Mbowe amekiomba kiti kurudia uchaguzi.

Mwongozo: Mwenyekiti amekubali mwongozo huo na ushauri wa Katibu hivyo zoezi la kura linarudiwa upya.

Kura zinaanza kupigwa upya
 
Wadau, wajumbe wa bunge la Katiba ndiyo wamewasili bungeni, tbc1 live
 
Wadau, wajumbe wa bunge la Katiba ndiyo wamewasili bungeni, tbc1 live

Nashawishika kusema NI SERIKALI MBILI, angalia akina nani wanaongoza bunge kwa muda. Katibu wa bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania na Katibu wa baraza la Wawakilishi Zanzibar.
 
Katibu amesoma tangazo maalum la rais la kuitishwa bunge la katiba. Sasa unafuata uchaguzi wa m/kiti wa muda wa bunge maalum la katiba.
 
Kupitia TBC1 ,
Naona wajumbe wanagombea nani atakuwa wa kwanza kuweka historia kwa kuomba “MWONGOZO“ wa kwanza.


Kaaaaazi kweli kweliiii
 
Back
Top Bottom