Yaliyojiri Arusha katika mazishi ya waliouliwa na Polisi

FAMILIA ya marehemu Ismail Omari (25) aliyeuawa katika vurugu za kisiasa zilizotokea Januari 5 mwaka huu mkoani hapa, imedai kushinikizwa na Chadema kumpeleka marehemu wao katika uwanja wa NMC kuagwa kinyume na maamrisho ya dini yao.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, baba mzazi wa marehemu huyo Omar Juma,
alisema shinikizo lililowafanya kukubali kitendo hicho lilitolewa juzi usiku baada ya msemaji wa familia yake, Nyerere Kamili, kupokea simu kutoka kwa mmoja wa viongozi wa Chadema; Diwani wa Elerai, John Bayo, kuwa iwapo hawatakubali kupeleka mwili wa ndugu yao kwenye uwanja huo, chama chake kitajitoa kushughulikia mazishi.

Alidai mbali na shinikizo hilo, pia juzi wakiwa chumba cha maiti, katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru, kuchukua mwili huo, walikuta mazingira yasiyo mazuri kwao kugomea kupeleka mwili huo wakihofia kudhuriwa na wafuasi wa Chadema, ambao walikuwa wamefurika eneo hilo wakitaka miili yote ipelekwe uwanjani kuagwa.

Alisema kutokana na sababu hizo, pia alilazimika kuwapigia simu viongozi hao wa Chadema na alikutana nao siku hiyo, wakakubaliana kuupeleka mwili huo uwanjani hapo, ili kupata msaada wa chama hicho wa mazishi kwa kuwa hawana uwezo wa kuendesha mazishi hayo.

“Sasa baada ya sisi kupokea simu hiyo, tulilazimika kuwapigia simu ili kupata msaada, maana vifo vimetokana na mkutano wao, sasa uwezo hatuna na hali ilivyokuwa pale, tungeweza kupigwa hata mawe na wafuasi wao kwa hiyo ilikuwa hivyo,” alisema Omar.

Pia alisema kutokana na shinikizo hilo, liliipa wakati mgumu familia yake baada ya Waislamu kuchukizwa na kitendo hicho hadi kufikia kunyimwa jeneza la kubebea maiti hali iliyowalazimu kuhangaika katika zaidi ya misikiti mitatu bila mafanikio.

Aliongeza kuwa baada ya hali hiyo, alikwenda kuchukua jeneza kwenye msikiti wa hospitali ya Mount Meru akikodi kwa Sh 5,000 ambayo hadi jana walikuwa wakidaiwa kutokana na kushindwa kulipa.

Kwa hali hiyo na kutambua kuukosea Uislamu na Waislamu kwa jumla, aliwaomba viongozi kuisamehe familia yake kwa kuwa haikuwa dhamira yao kufanya hivyo, bali kwa shinikizo la Chadema.

Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Baraza la Wazee wa Chadema wa Mkoa wa Arusha, Haruna Fundikira, alipoulizwa kuhusu suala hilo alikiri na kusema hata yeye aliungana na familia ya marehemu, kuwa suala la kupeleka maiti katika uwanja huo halikuwa sahihi kulingana na maamrisho ya dini.

Alisema walichokubaliana ni kupata japo picha ya marehemu Ismail ili ioneshwe uwanjani hapo, lakini maiti achukuliwe na kupelekwa kwa maziko Usa River, lakini alishangazwa na taarifa kuwa mwili huo ulipelekwa uwanjani hapo.

Alisema siku moja kabla ya maziko, alikwenda kwa familia ya marehemu kupanga mipango ya maziko hayo na walipokubaliana juu ya taratibu hizo, aliahidi kutoa sanda, lakini alilazimika kuahirisha kuitoa, baada ya kuona utaratibu tofauti na aliokubaliana na familia hiyo.

"Mimi jana sikwenda uwanjani hapo, nilikuwa na mgeni nyumbani, lakini nilichosikia ni kwamba walipeleka mwili huo uwanjani tofauti na nilivyokubaliana nao na sikutoa tena sanda, maana walikuwa na uamuzi wao kama familia,” alisema Fundikira.

Aliongeza kuwa, baada ya kuahirisha kutoa sanda, alipokea simu kutoka kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akisema ameshakubaliana na familia kuhusu taratibu zote za maziko na asihangaike kutoa sanda, kwani chama kitatoa.

Shehe wa Msikiti wa Bondeni, Shaaban Juma, alisema familia hiyo haina haja ya kuomba radhi, kwa kuwa alishirikiana nayo kwa hali na mali, lakini akashangazwa alipoambiwa na
mmoja wa wanafamilia, aondoke kwenye chumba cha maiti na angempigia simu baadaye, kwa kuwa suala hilo lilikuwa likiihusu familia pekee.

Alisema kamwe hawezi kuiomba radhi familia hiyo wala kutoa msamaha yeye, kwani familia imemkosea Mwenyezi Mungu na si Waislamu, kwa kukiuka misingi na taratibu za dini hiyo na iwapo iliona inazidiwa nguvu, ilipaswa kukabidhi jukumu hilo kwa viongozi wa kiislamu ili walisimamie.

“Mbali na Qur’an na Hadithi za Mtume kukataza, lakini kitendo cha kumpeleka marehemu wa
kiislamu uwanjani pale, ambao uligubikwa mapambio ni kinyume na maamrisho ya Mwenyezi Mungu na ni moja ya sababu iliyosababisha yeye asihudhurie maziko hayo,” alisema Shehe Shaaban.

Juzi Chadema iliendesha ibada maalumu ya kuaga miili ya marehemu wawili waliopoteza maisha katika mapambano baina ya wafuasi wa Chadema na Polisi kutokana na kufanya maandamano yaliyozuiwa kwa kuhofia uvunjifu wa amani ambapo watu watatu walipoteza maisha.

Katika hatua nyingine mwili wa marehemu Denis Shirima, nao ulihamishwa kutoka sanduku ambalo lilionekana kuwa duni na kuingizwa katika sanduku la kifahari, ambalo lilinunuliwa na Chadema.

Awali marehemu alikuwa kwenye sanduku la kawaida la rangi nyeupe wakati mwili ukiwa hospitalini tayari kupelekwa kwenye uwanja wa NMC kuuagwa, lakini baadaye ukabadilishiwa kwenye sanduku hilo jipya na la zamani haikujulikana lilikopelekwa.

HabariLeo | Chadema kwenye kashfa ya maiti

Ndugu yangu unashangaza saana! unategemea Gazeti la Uhuru liandike "CHADEMA YAIADABISHA CCM"? au unategemea gazeti la RAI liandike "Sitta Mzalendo wa Kweli"?? kama ndo mawazo yako yapo hivo, then you are a day dreamer!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Na mimi nimeweka Avatar jamani kwa mara ya kwanza. nani anaweza kujua hiyo picha ni ya wapi?
 
FAMILIA ya marehemu Ismail Omar (25), aliyeuawa katika vurugu za Januari 5, mwaka huu, mkoani Arusha, imesema ilishinikizwa na CHADEMA kukiuka maamrisho ya dini ya Kiislamu. Imesema kutokana na shinikizo hilo, familia iliamua kuupeleka mwili wa marehemu Ismail katika uwanja wa NMC kwa ajili ya kuagwa. Omar Juma, baba mzazi wa Ismail, akizungumza na mwandishi wa habari wa gazeti hili, alisema Jumanne saa tano usiku, msemaji wa familia hiyo, Nyerere Kamili, alipokea simu kutoka kwa diwani wa kata ya Elerai, John Bayo (CHADEMA), aliyemweleza iwapo hawatakubali kupeleka mwili wa ndugu yao uwanjani, chama hicho kitajiondoa kushughulikia maziko.
Alisema juzi asubuhi wakiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mount Meru ili kuchukua mwili wa Ismail, mazingira hayakuwa mazuri, hivyo walishindwa kuzuia mwili wake kupelekwa uwanjani kwa kuhofia kudhuriwa na wafuasi wa CHADEMA waliokuwa wamefurika hospitalini hapo.
Juma alisema aliwapigia simu viongozi wa CHADEMA na baada ya mazungumzo alikubali kuupeleka mwili wa mwanawe uwanjani ili apate msaada wa chama hicho kwa ajili ya maziko. “Tulilazimika kuwapigia simu ili kupata msaada kutokana na vifo kutokea kwenye mkutano wao nasi hatuna uwezo. Tulipeleka mwili uwanjani kutokana na hali ilivyokuwa, kwani vinginevyo tungeweza kupigwa hata mawe na wafuasi wao,” alisema. Omar alisema shinikizo hilo liliwakwaza baada ya waumini wa Kiislamu kuchukizwa na kitendo hicho, ambapo walinyimwa jeneza la kubebea mwili wa Ismail, jambo lililowafanya kuhangaika kwenye misikiti mitatu na kuambulia patupu.
Alisema familia ililazimika kwenda kuchukua jeneza kwenye msikiti uliopo Hospitali ya Mount Meru kwa gharama ya sh. 5,000, ambazo hadi jana zilikuwa hazijalipwa. Omar aliwaomba viongozi na Waislamu wote kuisamehe familia yake kwa kuwa haikuwa dhamira yao kukiuka maamrisho ya dini, bali hilo lilitokea kutokana na shinikizo la viongozi wa CHADEMA.
Mwenyekiti wa wenyeviti wa baraza la wazee wa CHADEMA mkoa wa Arusha, Haruna Fundikira, alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema aliungana na familia ya Omar kupinga mwili wa Ismail kupelekwa uwanjani kuagwa. Alisema walichokubaliana ni kupata picha ya marehemu Ismail ili ipelekwe uwanjani na baadae mwili uchukuliwe na kupelekwa Usa River kwa maziko. Kwa mujibu wa Fundikira, alishangazwa baada ya kupata taarifa kuwa mwili wa marehemu Ismail ulipelekwa uwanjani. Fundikira alisema Jumanne alikwenda kwa familia ya Omar ili kuweka mikakati ya maziko na walikubaliana kuhusu taratibu hizo na aliahidi kutoa sanda.
Hata hivyo, alisema alilazimika kuahirisha kutoa sanda hiyo kama alivyoahidi baada ya taratibu walizokubaliana kukiukwa. “Sikwenda uwanjani kwa kuwa nilikuwa na mgeni nyumbani kwangu, lakini nilichosikia ni kwamba walipeleka mwili uwanjani tofauti na nilivyokubaliana nao,” alisema. Fundikira alidai baada ya kuahirisha kutoa sanda, alipigiwa simu na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, akimweleza wamekubaliana na familia kuhusu taratibu za maziko, hivyo asihangaike kutoa sanda kwani itatolewa na chama. Kwa upande wake, Sheikh wa Msikiti wa Bondeni, Shaaban Juma, alidai familia ya Omar imekiuka maamrisho ya dini na kwamba, ilipoona inazidiwa ingewasiliana na viongozi wa dini. Juzi CHADEMA iliendesha ibada maalumu ya kuwaombea na kuwaaga marehemu Ismail na Denis Shirima wa Rombo, mkoani Kilimanjaro, ambao walipoteza maisha kwenye maandamano yaliyoandaliwa na chama hicho na kusababisha uvunjivu wa amani.

Mazishi ya waliouawa Arusha Mazito yaibuka

Kafukueni maiti ili mfuate taratibu mnazozitaka.
 
Juma alisema aliwapigia simu viongozi wa CHADEMA na baada ya mazungumzo alikubali kuupeleka mwili wa mwanawe uwanjani ili apate msaada wa chama hicho kwa ajili ya maziko. “Tulilazimika kuwapigia simu ili kupata msaada kutokana na vifo kutokea kwenye mkutano wao nasi hatuna uwezo. Tulipeleka mwili uwanjani kutokana na hali ilivyokuwa, kwani vinginevyo tungeweza kupigwa hata mawe na wafuasi wao,” alisema.

Ina maana kama marehemu angekufa kwa ugonjwa wasingeweza kumzika?
 
Akionekana kuumia na kitendo cha Kijana Denis Shirima Kuuawa Padre alieeongoza misa ya mazishi Wilayani Rombo amewataka vijana wajirinde na makundi wasiyo yajua! Kwa tafsiri Padre huyu ameona vijana wasijiingize kwenye makundi yatakayo hatarisha maisha yao na kumbe Chadema sio Chma cha Siasa ni kikundi tu ambacho vijana wawe macho kutambua makundi ya aina hiyo na kujilinda na maisha yao!
Kauli hii aliitoa Mbele ya Mh Mbowe,Mh Ndesamburo na Mh Mnyika! Viongozi hao tofauti na walivyofikiri kama kutakua na hamasa kama za Arusha lakini Rombo kwenye mazishi hayo kuliibuka kauli mbalimbali zilizoonesha kuwalaumu na hata baadhi ya wazee wengine waliona ni kama wanafanyiwa unafiki na Viongozi wa Chama cha Chadema! Ulinzi uliimarishwa kwa viongozi hao ambao waliamua kuondoka haraka baada ya mazishi hayo kwani walihisi walikua hawatakiwi na jamaa wa Denis na majirani kwa kuwaona wao ni sehemu ya Tatizo!

source Taarifa ya habari

huyu padre hana hisia ya taifa, kayumba. Pengo kakosea?
 
Wadau, tufungue album ya yaliyojiri Arusha siku ya mazishi ya wahanga wa Maandamano tarehe 05 Januari 2011 Arusha.

Picha hizi nilizipiga kuanzia saa 5 hadi saa 7 mchana kabla majeneza hayafika Uwanja wa NMC.
 

Attachments

  • DSC01295.JPG
    DSC01295.JPG
    48.6 KB · Views: 34
  • DSC01250.JPG
    DSC01250.JPG
    44.1 KB · Views: 31
  • DSC01260.JPG
    DSC01260.JPG
    51.5 KB · Views: 31
  • DSC01239.JPG
    DSC01239.JPG
    41 KB · Views: 27
  • DSC01302.JPG
    DSC01302.JPG
    74 KB · Views: 31
  • DSC01280.JPG
    DSC01280.JPG
    54.5 KB · Views: 28
  • DSC01240.JPG
    DSC01240.JPG
    42.1 KB · Views: 27
  • DSC01268.JPG
    DSC01268.JPG
    43.9 KB · Views: 28
  • DSC01314.JPG
    DSC01314.JPG
    32.5 KB · Views: 27
  • DSC01322.JPG
    DSC01322.JPG
    65.1 KB · Views: 28
  • DSC01261.JPG
    DSC01261.JPG
    66.6 KB · Views: 31
  • DSC01228.JPG
    DSC01228.JPG
    57.1 KB · Views: 25
  • DSC01301.JPG
    DSC01301.JPG
    44.6 KB · Views: 25
  • DSC01281.JPG
    DSC01281.JPG
    63.3 KB · Views: 25
  • DSC01269.JPG
    DSC01269.JPG
    65.7 KB · Views: 26
  • DSC01262.JPG
    DSC01262.JPG
    67.3 KB · Views: 25
  • DSC01303.JPG
    DSC01303.JPG
    69.7 KB · Views: 24
  • DSC01241.JPG
    DSC01241.JPG
    46 KB · Views: 30
  • DSC01325.JPG
    DSC01325.JPG
    47.7 KB · Views: 25
  • DSC01252.JPG
    DSC01252.JPG
    45.8 KB · Views: 28
  • DSC01229.JPG
    DSC01229.JPG
    41.7 KB · Views: 25
  • DSC01282.JPG
    DSC01282.JPG
    50.9 KB · Views: 24
  • DSC01270.JPG
    DSC01270.JPG
    41.2 KB · Views: 27
  • DSC01263.JPG
    DSC01263.JPG
    53.4 KB · Views: 23
Huyo padri ana akili nyingi sana,,anastahili tuzo iliyotukuka
j.tatu tukirudi maofisini lazma tuangalie namna ya kumtuza,,ni ukweli vijana wanatumika,uchaguzi umepita,jakaya kikwete ndio rais till 2015 kama hutaki hama nchi....ha ha ha ha ha,,njaa kitu kibaya sana mpaka inakufanya mtu uanzishe majungu yasiyo na msingi
 
Kama ni hivyo,basi mpango wa mapinduzi kupitia maandamano wanaoutamani chadema kama kule Tunisia una walakini.
Mipango ya Chadema itakuwa kama ya Red shirts wa Thailand,itasambaratika yenyewe.Watunis wameunganishwa na kitu kimoja tu-mkate.Lakini Chadema haiwezi kuwaunganisha watanzania kuleta mapinduzi kutokana na ubaguzi wao na udini wa kuwachukia waislamu walio madarakani.
 
Alichosema Padre kwa kutumia mfano wa wachaga wa Rombo "huwezi kuona maiti ya Nyani" Akimaanisha kwamba Nyani ni muoga na huwa mwepesi sana kukimbia akiona hatari hata kama ni jani limejigusa. Aliwataka vijana kutojiingiza katika mabishano akisema kwamba mabishano si mazuri. Akaendelea kusema "ukiona maji mengi kaa pembeni". Hakuna mahali alipotaja CDM au kutumia neno 'kikundi'.

Mbunge wa Arusha Mjini, Mh. Godbless Lema, aliposimama aliwaambia wananchi "nawaambia jipeni moyo, hata yesu hakuwahi kuwaambia watu poleni". aliendelea kuelezea kilichotokea arusha na kuwaambia vijana wasirudi nyuma kudai haki. Aliwaeleza kwamba woga ni kitu kibaya kwani hata mtu muoga hawezi kutubu dhambi zake kwa sababu ya woga.

Hakuna kiongozi wa CDM aliyeondoka kwa haraka na wananchi walikuwepo kwa wingi kwenye mazishi. Huwezi kutegemea idadi kama ya arusha Rombo hata siku moja. Arusha inabaki kuwa Arusha na Rombo itabaki kuwa Rombo.

Usipotoshe ukweli. Simamia kweli na haki itapatikana. Ujumbe wako ungefika kama ungesema ukweli bila kupindisha maneno!!
 
Akionekana kuumia na kitendo cha Kijana Denis Shirima Kuuawa Padre alieeongoza misa ya mazishi Wilayani Rombo amewataka vijana wajirinde na kujiepusha kujiingiza kwenye makundi wasiyo yajua! Kwa tafsiri Padre huyu ameona vijana wasijiingize kwenye makundi yatakayo hatarisha maisha yao na kumbe Chadema sio Chma cha Siasa ni kikundi tu ambacho vijana wawe macho kutambua makundi ya aina hiyo na kujilinda na maisha yao!
Kauli hii aliitoa Mbele ya Mh Mbowe,Mh Ndesamburo na Mh Mnyika! Viongozi hao tofauti na walivyofikiri kama kutakua na hamasa kama za Arusha lakini Rombo kwenye mazishi hayo kuliibuka kauli mbalimbali zilizoonesha kuwalaumu na hata baadhi ya wazee wengine waliona ni kama wanafanyiwa unafiki na Viongozi wa Chama cha Chadema! Ulinzi uliimarishwa kwa viongozi hao ambao waliamua kuondoka haraka baada ya mazishi hayo kwani walihisi walikua hawatakiwi na jamaa wa Denis na majirani kwa kuwaona wao ni sehemu ya Tatizo!

source Taarifa ya habari ITV saa 2 Usiku

Mara nyingi maudhui ya viongozi wa kiroho wa kikatoliki ni ya kutafakari kwa kina kabla ya kufikia hitimisho huyo padre alikuwa na maana nzuri tu na wala hajamaanisha kuwa CDM ni chama cha kihuni au kikundi tu.
Tafakari
 
Back
Top Bottom