Yale ya Man U sasa yageukia Real Madrid...

Dr. Chapa Kiuno

JF-Expert Member
Sep 11, 2009
443
18
Wadau, huko nyuma tuliona jinsi Manchester United walivyokuwa wakichemsha endapo hiyo siku Ronaldo hakucheza! Je tatizo hilo ndyo limegeukia kwa Madrid?

Kwa mfano, mechi ya juzi dhidi ya Sevilla walichapwa 2:1 kama wamesimama huku Sevilla wakitawala mchezo mzima. na hiyo yote ni kwa sababu Ronaldo ni majeruhi...

Je! watatoka maana hata Rais wa ile timu amewaambia wajifunze kucheza bila Ronaldo.
 
haya sasa! walikuwa wakidai Man U bila ronaldo haichezi game limegeukia kwa Madrid.
 
Yawezekana ni kweli mzee, unajua Ronaldo ana "style" ya uchezaji ambao hata akihamia timu yoyote, mtajikuta mkitafuta aina ya mchezo ambao utaendana na au kulazimika kumtegemea yeye. Sasa anapokuwa majeruhi ndiyo kasheshe inapoanzia hapo!
 
Mbona Man U ilikuwa inchezea kichapo hata Ronaldo akiwa ndani. Kichapo ni sehemu ya game
 
Madrid walishindwa kabisa kuutawala ule mchezo. Kuna wakati akina kaka walishindwa kabisa kuingia ndani ya 18.
 
Mbona Man U ilikuwa inchezea kichapo hata Ronaldo akiwa ndani. Kichapo ni sehemu ya game
Ndio maana yake, soka ni mchezo wa timu sio suala la indiviadual. Man walikuwa wanapigwa na hyo Ronaldo akiwa ndani ila ni kwaida ya mashabiki kutafuta sababu ya timu kufanya vibaya. Pia tusisahau Sevilla sio timu ya mchezo!
 
Sevilla siyo timu ya kubeza, imekamilika kote kote. Front two ya Kanoute & Luis Fabiano ni extremely lethal. Hata Barcelona wajiandae vizuri ....
 
Yawezekana ni kweli mzee, unajua Ronaldo ana "style" ya uchezaji ambao hata akihamia timu yoyote, mtajikuta mkitafuta aina ya mchezo ambao utaendana na au kulazimika kumtegemea yeye. Sasa anapokuwa majeruhi ndiyo kasheshe inapoanzia hapo!

Mh hata akija kwa wekundu wa msimbazi?
 
Ni wazi kuwa CR9 ni kiboko na kwamba hata nilipoingalia ile match niliona kabisa kuna pengo forwardline ya RMA bila huyo Mreno. Hata hivyo Sevilla imesukwa vizuri sana na naamini itatoa upinzani mkali kwenye La Liga. Hivi sasa ni ya tatu kwenye La liga
 
jamani mimi ni Man U damu toka kipindi cha Cantona, manU haibebwi it is a team, angalia vifaa vingapi vimehama lakini bado tuna-shine.

The only catalyst ni kocha siku akiondoka ndio tutayumba ila hatutegemei mchezaji
 
nakubaliana na wewe
 
Back
Top Bottom