Yale mafuriko yalinitisha sana

ladyfurahia

JF-Expert Member
May 10, 2011
14,699
9,461
Mwenzenu nilikuwa silali wa sitambai kwani yale mafuriko yalikuwa si mchezo ilikuwa ni balaa tupu maana sijawahi kuona
kaitika macho yangu ndugu zetu kufa kiasi kile na serikali inatudanganya kuwa wamekufa wachache kumbe lukuki yaani mwenzenu nililia kiasi cha kuona uchungu wa kuploteza ndugu zangu na wengine kukosa makazi, ilinitia uchungu sana wewe ushazoea mahali fulani pa kukupatia riziki unaambiwa uende magwepande je utaishije huko je huduma zile za kijamiii utazipataje nua je shughuli zako au biashara zako utazifanyeje wakati mahali ulipozoea ni hapo ndugu zangu waungwana ingelikuwa ni wewe ungefanyaje?
 
Dar es salaam mvua inaweza kunyesha wiki nzima lakini haijawahi kuleta mafuriko kama yale na kuua watu embu fikiria ile mvua ilinyesha usiku tu halafu asubuhi ikaendelea lakini siyo yakuleta mafuriko kama yale halafu ilikatika ghafla yaani sijui kuna nini kimejificha hapa?
 
mwenzangu hata nami sielewi kwanini mafuriko yale yameleta maangamizi makubwa uenda Mungu ameamua kutupiga kwa dhambi tuzifanyazo mmhmm!
 
Back
Top Bottom