Yakitokea ya udsm na st john chuo cha udom nani alaumiwe?

Kaka mwisho

JF-Expert Member
Dec 19, 2011
402
165
Sababu kuu ya migomo vyuoni kwasasa ni kucheleweshewa kupatiwa fedha zao ambazo kwasasa zinatolewa na vyuo husika, mpaka sasa udom baadhi bado hawajapata hata la kwanza na la pili muda wake umefika nalo bado hawajapewa. Maisha dom kla kitu kinahitaji pesa. Uongozi upo kimya hata tukihoji hatupewi jibu la msingi. Je udom yakitokea kama udsm na st john nani alaumiwe?
 
Poleni sana wana-UDOM. Ili mwanafunzi aweze ku-concentrate kwenye masomo kwa 100% ni lazima, kwanza ale chakula,ikifuatiwa na mahitaji mengine. Wakati mwingine ninafikiria labda mihula ya masomo kati ya masiki wanaotegea fedha za HESLB kuendesha maisha yao ya vyuoni, na wenye uwezo wasiotegea mikopo iwe tofauti!? Kwa masikini wanaotegemea mikopo, mhula wao uwe wakati HESLB wanakua na fedha!? Inasikitisha sana. Pia tuwape pole Tumaini-Iringa ambao wamekwenda likizo hata majina hayajaja, st. John na wengine.
 
Tatizo mnaendekeza sana starehe. Endelea kutumia pesa ya stationary bumu likiingia utajazia.

Tatizo mnaishi bila bajeti. Mnajifanya familia bora wakati watoto wa Mkulima.
 
hasara ya roho, pesa makaratasi.
Hela yenyewe hata kiwanja hainunui...
 
poleni sana najua nashangaa sana wabunge walidai waongezwe posho kwa kudai kuwa dodoma maisha yamepanda sasa hayo maisha yamepanda kwa wabunge tuu,mbona wanachuo awapatiwi pesa kwa wakati je wataishije
 
Tatizo mnaendekeza sana starehe. Endelea kutumia pesa ya stationary bumu likiingia utajazia.

Tatizo mnaishi bila bajeti. Mnajifanya familia bora wakati watoto wa Mkulima.

Mfumuko wa bei ya vyakula umefikia 17% na thamani ya shilingi imeendelea kuporoka kwa kasi. Mkopo ni 7500/-kwa ajili ya chai,chakula mchana na jioni, na malazi kwa siku moja. Fedha ya stationary ni sh. 100,000/- semista. Kutokana upungufu wa vitabu tulazimika kutoa photocopy. Mimi huwa natoa copy kwa wastani wa sh.20000/= kwa kitabu,bado handouts n.k. Hiyo budget unayosema ndugu yangu ni ya namna gani? Tuwekee mfano wa mchanganuo hapa tujifunze. Kumbuka pia bei za vyakula kuzunguka vyuo zilipanda mara tu baada fedha kuongezwa kutoka 5000/- HADI 7500/-, je ongezeko lina maana gani?
 
unachosema ni tofauti na mwenzako anachodai. Jarbu kumsoma vizuri.
 
Kama kwa sisi tusiofanya starehe huwa tunajikuta tunaingiza fedha za stationary kwenye matumizi ya chakula na malazi pamoja kujitahidi kufanya budgeting, sijui kwa wanaofanya starehe watakuwa na hali gani!! Ninafikiri ninaweza kuwa nimekusoma vizuri!?
 
Tatizo mnaendekeza sana starehe. Endelea kutumia pesa ya stationary bumu likiingia utajazia.

Tatizo mnaishi bila bajeti. Mnajifanya familia bora wakati watoto wa Mkulima.
Ushaanza ujinga wako mzee
 
Kama kwa sisi tusiofanya starehe huwa tunajikuta tunaingiza fedha za stationary kwenye matumizi ya chakula na malazi pamoja kujitahidi kufanya budgeting, sijui kwa wanaofanya starehe watakuwa na hali gani!! Ninafikiri ninaweza kuwa nimekusoma vizuri!?

ni hivi hajasema kuwa pesa haitoshi ila anadai pesa wamechelewa kuwekea hela.

Unachosema kipo sahihi. 7500/= ni pesa ndogo sana kwa maisha ya mwanachuo, wengine wanatumia hiyo hiyo kujilipia ada. Nadhani kuna haja ya serikali kulifikiria hili, sio wabunge wajiongezee tu posho.
 
Back
Top Bottom