Yajue yafuatayo kuhusu ubongo wa mwanadamu

Nimependa namba 11,tumewazidi ukubwa wa ubongo kwa 10% ila bado kila siku utasikia thread zinaanzishwa wametuliza na kulalamika vile wanavyotuendesha,pia kutafuta namna ya kuishi nao na kuwajua!!
 
Mkuu, asante kwa elimu, swali langu ni; nini kinasababisha mtu kusahau vitu au kupoteza kumbukumbu na wakati hajawahi kuanguka au kupata ajali na kujigonga kichwani?.
 
Nimeipata Elimu Mkuu.Kuna project wameanzisha Marekani na ulaya kuhusu GENOM wanataka wapate jibu who exactly we are. Nadhani wakiimaliza Mambo mengi kuhusu ubongo yatajulikana.Kuna mtu aliniambia Mtoto akizaliwa huwa hana ubongo ila huwa kadiri anavyokuwa mkubwa na ubongo unagrow na kuongezeka sambamba na ukuaji wa mtoto.Hili unalijuaje?
 
Mkuu Fion,kupoteza kumbukumbu kunaweza sababishwa na vitu vifuatavyo ukitoa ulivyovisema wewe;

-utumiaji wa baadhi ya madawa ya viwandani kwa mda mrefu hasa antidepressants,anti anxiety na baadhi ya muscle relaxants.

-kutopata usingizi wa kutosha na bora.

-msongo wa mawazo kw mda mrefu

-uvutaji wa sigara, tumbaku,kokeni na heroini

-unywaji wa pombe

-kujichua(kupiga nyeto) kwa mda mrefu pia huathiri uwezo wa ubongo kukumbuka.
 
Hapana mtoto anapozaliwa anakuwa tayari ana ubongo na anapofikisha miaka 2 ukubwa wa ubongo wake uwa ni 80% sawa na ukubwa wa ubongo wa mtu mzima.

mtoto akifikisha miaka mitano ubongo husimama kukua na uendelea kudevelop mpaka mtu afikishe miaka 40 napo utasimama.
 
Mkuu Fion,kupoteza kumbukumbu kunaweza sababishwa na vitu vifuatavyo ukitoa ulivyovisema wewe;

-utumiaji wa baadhi ya madawa ya viwandani kwa mda mrefu hasa antidepressants,anti anxiety na baadhi ya muscle relaxants.

-kutopata usingizi wa kutosha na bora.

-msongo wa mawazo kw mda mrefu

-uvutaji wa sigara, tumbaku,kokeni na heroini

-unywaji wa pombe

-kujichua(kupiga nyeto) kwa mda mrefu pia huathiri uwezo wa ubongo kukumbuka.

Mkuu asante sana kwa elimu.
 
kupatia utajiri. Ukitumia chini ya hapo wewe andika fukara Wa milele
Binadamu tunatumia asilimia 100 ya ubongo wetu.

Habari ya mwanadamu kutumia asilimia 10 ya ubongo wake ni ya uongo isiyokuwa na uthibitisho wowote wa kisayansi.
 
Si kweli kwamba tunatumia 10% tu ya ubongo wetu na mpaka sasa hakuna ushaidi wa kisayansi uliotolewa na mwanasanyansi yoyote kuonyesha kwamba tunatumia 10% tu ya ubongo wetu.

uongo huu wa kwamba tunatumia 10% tu ya ubongo wetu ulianzishwa na watu waliowanukuu na kuelewa vibaya kwenye mojawapo za nukuu za Albert Einstein na Piere Flourens(1800).

wengine pia walimnukuu na kumwelewa vibaya William James(1908) aliyesema, "We are making use only a small part of our possible mental na physical resources"

pia kuna mwanabaiolojia,Lashleyalishikilia bango uongo wa 10% ya matumizi ya ubongo, yeye alikata kipande kidogo cha ubongo wa panya kutoka kwenye frontal cortex ya cerebral hemisphere, na kugundua kwamba baadhi ya matendo yanayoongozwa na kipande cha ubongo kilichokatwa yameweza kuonenaka tena kwa panya kupitia kujifunza hivyo akaja na hitimisho la 10% kwa mwanadamu kitu ambacho si kweli.
lete ukweli
 
lete ukweli
Ukweli ni kwamba, kila eneo la ubongo wa mwanadamu lina kazi hivyo kuufanya ubongo kutumika kwa asilimia 100.

Kuondoa kwa kukata au kuharibu sehemu yoyote ya ubongo kutakufanya ushindwe kufanya baadhi ya matendo.

Mfano,kuharibika kwa sehemu ya ubongo wa nyuma(cerebellum) kutakufanya ushindwe kutembea,kukimbia na hata kuendesha baiskeli ama gari.

Na sehemu zote za ubongo zilizobaki zitasababisha matokeo fulani ikiwa zitaharibiwa,hivyo basi ubongo wetu unatumika kwa 100% ndani ya mwili na si 10%.
 
Back
Top Bottom