Yajue Madhara ya Vipodozi vyenye Kemikali na Vipodozi Vilivyopigwa Marufuku

Tathmini kuhusu usalama wa vipodozi kwa bahati mbaya hufanyika wakati tayari vipodozi viko sokoni na vinatumiwa na binadamu.

Nchini Marekani Mamlaka ya Udhibiti wa Vyakula na Dawa (The U.S Food and Drug Administration - FDA) hufanya majaribio ya kimaabara kwa vipodozi ambavyo vimelalamikiwa na wateja na kufunguliwa shauri la kisheria. Kinyume na hapo hakuna!

Aidha, inachukua miaka mingi mpaka kufikia huo mchakato kwa mamlaka hiyo kuzishauri mamlaka za kisheria kutoa idhini ya kuanza kufanyika majaribio hadi kuyapiga marufuku makampuni yanayozalisha vipodozi vinavyolalamikiwa. Hivyo kutokana na kadhia hiyo FDA mara nyingi hufanya mashauriano na makampuni hayo ili ama yasitishe kuzalisha vipodozi hivyo au yabadiri formula inayotumiwa kuzalisha vipodozi hivyo. Hii yote ni kukwepa mlolongo mrefu wa kisheria.

FDA imekadiria kwamba ni asilimia 3 tu ya wasambazaji wakubwa wa vipodozi wapatao 4,000 na 5,000 ndo wamewahi kutoa taarifa kuhusu madhara ya baadhi ya vipodozi vilivyolalamikiwa na watumiaji. Yaani asilimia 97 wala hawatoi taarifa na wanasambaza vipodozi vingine vikiwa na sumu. Sasa kama US hali iko hivyo hapa Tanzania si tuna hali mbaya sana!

Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Tanzania (TFDA) kimsingi huwa inafuatilia ripoti za WHO na nchi zilizoendelea kuhusu vipodozi vilivyopigwa marufuku. Ndio maana wakipata ripoti ndio wanahangaika na operesheni za kushtukiza za kukagua maduka ya vipodozi. Usalama wetu uko wapi?

Nisiwaache bila kuwapa habari kuhusu madhara ya kemikali mbili japo zipo nyingi zenye madhara kwa binadamu. Kemikali hizo ni 1,4-Dioxane na Phthalates. Ukiangalia label kwenye chupa ya vipodozi iwe ni toner, shampoo, cleanser, conditioner, mafuta ya nywele, baby lotion, soaps, etc hutoona imeandikwa 1,4-Dioxane kama kiambata (ingredient).

Ni kwamba sumu hiyo ipo katika vipodozi vingi. Ukiona kwenye lebel kuna viambata vyenye majina yenye herufi..eth…ujue kiambata hicho kinatengeneza sumu ya 1,4-Dioxane kwenye vipodozi hivyo ulivyonavyo. Mathalani Sodiumm laureth, Polyethyleneglycol, Oleth, Myreth, Ceteareth, nk.1,4-Dioxane inaitwa ‘Silent Killer' na husababisha saratani (Cancer). Sasa chunguza labels za vipodozi ulivyonavyo je kuna ambavyo vina viambata vyenye majina yenye eth?

Nakuja kwenye sumu ya pili – Phthalates. Asilimia 80 ya vipodozi kufuatia utafiti uliofanywa na Women's Environmental Network, Swedish Society for Nature Conservation and Health Care Without Harm, vina sumu aina ya Phthalates.

Unataka kujua harufu ya hiyo sumu? Egesha gari lako juani kwa masaa kadhaa ukiwa umefunga milango na vioo vyote. Then nenda kafungue mlango, harufu utakayosikia ndio hiyo sumu! Hiyo sumu inatoka kwenye dashboard na viti vya gari yako (plastics). Hii ndio maana baadhi ya madaktari wanashauri wanawake wajawazito ama wasinunue magari mapya au wasipande magari hayo hususan katika kipindi cha wiki chache za kwanza za ujauzito. Kwa nini…nitaeleza!

Mwaka 2000 University of Puerto Rico katika utafiti wake ilihusisha sumu ya Phthalates katika vipodozi na kuwahi kubalehe kwa mabinti. Usishangae siku hizi vibinti vinabalehe vikiwa katika umri mdogo sana. Sasa akina mama wajawazito mnaotumia vipodozi vyenye hiyo sumu jueni mnahatarisha afya za watoto wenu wa kiume ambao bado hawajazaliwa (unborn baby boys).

Sumu hiyo inahatarisha ukuaji kamilifu wa pumbu za watoto wa kiume, madhara yake ni low sperm count, upungufu wa nguvu za kiume (sexual dysfunction) na hormonal imbalance! Unakuta katoto ka kiume kanajisikia zaidi kuwa ka kike kuliko ka kiume!!! Ushoga ndo namaanisha!

Siku hizi pia tatizo la nguvu za kiume linazidi kila siku ienda! Kijana wa miaka 20 tu anaanza kutafuta madawa ya kuongeza nguvu za kiume…je akifikisha 40? Halafu matatizo haya yanashika kasi mijini kuliko vijijini…Hatujiulizi why?! Matatizo ndo kama haya ya vipodozi na aina ya vyakula plus our life style!

Mwaka 2007 University of Rochester School of Medicine, New York ilifanya utafiti kuhusu sumu hiyo na kugundua kuwa inaleta adnominal obesity kwa wanawake!

Hatushangai siku hizi lipo ongezeko la wanawake wenye vitambi na ndevu? Hiyo ni afya au matatizi! Na sisi wanaume hatuko salama na hiyo sumu maana tunatumia pia vipodozi vyenye hiyo sumu.

Halafu hata hizi MP3 player earphones zina hiyo sumu. Siku hizi ni fasheni kutembea na nazo muda wote. Pamoja na kwamba zinaleta tatizo la usikivu baada ya matumizi ya muda mrefu pia check nguvu za kiume… wanaume tunahitaji kufunga magoli na ufundi haswa.

Ngoja niwambie jambo la mwisho kwa leo.

Vipodozi vinavyouzwa katika nchi za Ulaya havina sumu hizo kwa kiwango kama vile vinavyouzwa nchi za Afrika! Aina ni ile ile ya vipodozi lakini kwao mambo safi kwetu tunatupiwa uchafu wa vipodozi. Why? Kwa sababu sheria na kanuni zinazosimamia vipodozi zimekaza…sisi kwetu legelege! Kama sio legelege…fake fake kwa kila bidhaa huku kwetu yatoka wapi?

Next time nitaongelea madhara ya hizo mnazopaka kwenye makwapa ili kukata jasho. Hatutaki kunuka vikwapa je hizo antiperspirants ni salama kwa afya zetu? Mind you sipingani na biashara za watu za hivyo vipodozi bali tunaelemishana tu.


Use At Your Own Risk!

 
Kamanda Kazi, sijui kinadada nani kawaroga... Wamekuwa wateja, wanazi na waathirika wakubwa wa bidhaa za viwandani ambazo licha ya kuwaharibu afya ya ndani na nje, bado haviwafanyi kuwa warembo kama wanavyodhani.

Tunahitaji harakati aisee!
 
Last edited by a moderator:
Ili niishi salama naanza kurudi Edeni kwa asiri yangu,naanza kura vya asiri wazungu wabaki na vya kwao,kama kufa ntakufa kama walivyokuufa wazazi wetu ila kujiua kwa sumu hizi sitoweza ...God bless me!
 
Mimi nilikuwa natumia deodorant ya nivea. Nilipata majipu ya kwapa tokea niache kutumia sijapata tena jipu.
 
Podochi zote dhimepigwa marukufuka sasa dada zetu mrudie enzi zile za kupakaa maparachichi na mawese..
 
Nimeangalia ingredients kwenye body lotion ya johnson na hand lotion ya johnson ina viambatanisho hivyo vya "eth" itanibidi niachane navyo tu haina jinsi
 
Haya ni madhara ya kutumia vipodozi ni hatari sana, hasa (loshen, krim,na nyinginezo) matatizo huharibu mimba, kuozesha ngozi napia, kuhisi maumivu ya ngozi.
 
ni kweli ila sio vyote.. jaribu ku-google hasa kwa kiingereza utapata majibu mengi kwa urefu.
 
4f4c9168f36abd9ea4474f841a929f09.jpg
 
Back
Top Bottom