Yahya Mohamed na 'Songombingo' kwa Dr Ulimboka

Salaam Wakuu,

Hatua ya kuanzisha thread si mbaya, kama mnaweza kunisifia publicly si vibaya pia kunikosoa publicly. Yalikuwa maoni binafsi na hayakulenga kumdhihaki mwanahabari yeyote, ama kuufunga mjadala juu ya Dr.Ulimboka kwani si jukumu langu wala sina dhamana hiyo.

Inawezekana kabisa kuna kupishana katika mawazo juu ya jambo fulani, hakumaanishi mtandao wala kumtumikia mtu yeyote kwa manufaa binafsi.

Napenda kutambua na kuheshimu kupishana huko katika fikra, lakini pia kuomba radhi sana kama matamshi yangu yamekwaza harakati muhimu katika sakata hili.

Maangalizo na Ushauri umezingatiwa.

Ahsanteni Wanajamvi

Yahya M

Binadamu kukosea ni kitu cha kawaida na haswa ukijua kama umekosea ndio inakuwa vizuri!
 
huyo yahya mohamed ni hopeless kabisa huwa nikimuona kwenye kipindi chochote startv huwa nahama ni mjinga mjinga fulani sijui ana elimu gani ila in short ni mtu anayejipendekeza bila kujali kama anamfurahisha huyo anayekusudia kujipendendekeza kwake. ni opportunist with very shallow analysis, i will come back wit details on my stand
Yahya Mohamed, wewe ni memba hapa JF naomba unipe jibu:

Hivi ni kweli Waandishi wa habari waache kumwandika DR Ulimboka kwa sababu wanampa kichwa na wananchi wamechoka habari zake?
Je, ni kweli madaktari wanamuona Dr Ulimboka anafanya nchi isitawalike na wanamuona ni mchochezi?
Je, uliyosema leo kwenye kipindi cha tuongee asubuhi baada ya kusoma gazeti mtaandaoni la the Citizen, wananchi wamechoka kusikia habari za Dr Ulimboka?
Je, Yahaya wewe ni mwandishi mwanaharakati unafuatilia habari mpaka upate jibu na kuwahabarisha wananchi au wewe una masilahi binafsi?
Je, Yahaya umefanya haki kuwazodoa waandishi wenzako kwamba wanamwendekeza na kumukweza Dr Ulimboka?

Leo umenisikitisha sana, I am one of you fans but I have been deeply disappointed with your today's comments. I think you used a very wrong platform.
 
huyo yahya mohamed ni hopeless kabisa huwa nikimuona kwenye kipindi chochote startv huwa nahama ni mjinga mjinga fulani sijui ana elimu gani ila in short ni mtu anayejipendekeza bila kujali kama anamfurahisha huyo anayekusudia kujipendendekeza kwake. ni opportunist with very shallow analysis, i will come back wit details on my stand

HAPO KWENYE RED - NI KWELI KABISA KWANI AMETOA KAULI HIZO AKIHISI WALIOMPIGA DR. ULIMBOKA WANAMSIKIA - NA HUENDA AKAPEWA CHEO ....................

pole zake - kwa roho hiyo - ni NGUMU KUSOGEA AU KUPANDA STEP KWENYE MAISHA

ushauri kwa Yahya Mohamed: BADILI TABIA - NA MORE OVER THINK BEFORE YOU LEAP!!!!!!:argue:

Mungu akubariki, nilianza kufikiria ile biashara ya kuamka asubuhi week end niungane na star tv inaelekea tamati.

Ni vema kutoa maoni yako kaka ila chagua maneno ya kusema, hasira na machungu ya maisha ni mengi sana watu hawachelewi kukuona km adui iwapo msimamo wako utatofautiana na maslahi ya umma.

Mungu akujaze nguvu endelea na kutumikia fani yako, ila kumbuka changamoto hazitaisha.

salaam wakuu,

hatua ya kuanzisha thread si mbaya, kama mnaweza kunisifia publicly si vibaya pia kunikosoa publicly. Yalikuwa maoni binafsi na hayakulenga kumdhihaki mwanahabari yeyote, ama kuufunga mjadala juu ya dr.ulimboka kwani si jukumu langu wala sina dhamana hiyo.

Inawezekana kabisa kuna kupishana katika mawazo juu ya jambo fulani, hakumaanishi mtandao wala kumtumikia mtu yeyote kwa manufaa binafsi.

Napenda kutambua na kuheshimu kupishana huko katika fikra, lakini pia kuomba radhi sana kama matamshi yangu yamekwaza harakati muhimu katika sakata hili.

Maangalizo na ushauri umezingatiwa.

Ahsanteni wanajamvi

yahya m
 
Salaam Wakuu,

Hatua ya kuanzisha thread si mbaya, kama mnaweza kunisifia publicly si vibaya pia kunikosoa publicly. Yalikuwa maoni binafsi na hayakulenga kumdhihaki mwanahabari yeyote, ama kuufunga mjadala juu ya Dr.Ulimboka kwani si jukumu langu wala sina dhamana hiyo.

Inawezekana kabisa kuna kupishana katika mawazo juu ya jambo fulani, hakumaanishi mtandao wala kumtumikia mtu yeyote kwa manufaa binafsi.

Napenda kutambua na kuheshimu kupishana huko katika fikra, lakini pia kuomba radhi sana kama matamshi yangu yamekwaza harakati muhimu katika sakata hili.

Maangalizo na Ushauri umezingatiwa.

Ahsanteni Wanajamvi

Yahya M

Mkuu, Respect !
 
Nadhani ungetumia PM!

huko ni kulea UJINGA ndio yaleyale ya mambo ya ufisadi kuyamaliza kwenye chama kishkaj wafanyayo ccm..
Kwanini tulee ujinga?
kwanini am'PM?
Na ambao hatukubahatka kukiona hiko kipindi tungejuaje?
MFICHA UCHI HAZAI
 
NB
Tabia ya kusema tumechoka kusikia suala fulani, (mfano EPA, Richmond, Ulimboka, NK) ndio huwajengea kiburi viongozi wetu, mpaka wanafikia kuja na misemo
"Ni Upepo, Utapita"
 
huyo yahya mohamed ni hopeless kabisa huwa nikimuona kwenye kipindi chochote startv huwa nahama ni mjinga mjinga fulani sijui ana elimu gani ila in short ni mtu anayejipendekeza bila kujali kama anamfurahisha huyo anayekusudia kujipendendekeza kwake. ni opportunist with very shallow analysis, i will come back wit details on my stand

Hatuendi hivyo maishani mtu amekiri kosa,kaomba msamaha amekuwepo hapa kabla yako why umtusi kumuita mjinga? Watu kama nyie mnakatisha tamaa na kuharibu JF hayo matusi peleka FB

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Kweli kabisa Ngonani Paul Mabuga alimwangalia Yahaya Kwa mshangao akapotezea lakini tayari tukamsoma Yahaya na bado tunajiuliza je hii ndio sura halisi ya Yahaya au amepitiwa tuu,Manake kituo chao cha Star TV kinakuja vizuri sana ,je wanataka kuingia kwenye propaganda ,manake nimeskia Faraji Mwegoha akiwa Dodoma anawasemea wananchi wa Dodoma eti ni watu wenye busara wanafikiri kabla ya kutenda hawana ushabiki na jaziba za kisiasa hawaandamani kwani maandamano ni ujinga nakadhalika nakadharika hembu tuwape wiki tuone kama hawa hawatakuwa TBCCM-B na ikiwa hivyo basi watajiungasha kama gunia

Kinachoisumbua Star TVni kwenda kasi katika mabadiliko ya kiteknolojia bila kuandaa nguvu kazi yenye weledi kiasi cha kuweza kumatch na kasi hiyo. Ni kama Boss anayejikita kufanya installations za software bila kuandaa wataalam wa kutumia hizo software.

Hiki ulichokiona kwa Mtangazaji Faraji Magonha nimekuwa pia nikikiona pia kwa muda mrefu. Kwenye kikao cha Bunge kilichoisha alionesha uwezo mdogo katika kumudu vipindi hojaji (Interview programs). Mara nyingi amekuwa akihoji maswali yaliyo nje kabisa na mada inayojadiliwa kiasi cha kupoteza maana yote ya kipindi.

Kuna kipindi kingine cha medani za Siasa kilikuwa kikirushwa kila Jumapili naona kwa sasa kimepoteza dira kabisa. Zamani kilikuwa panel discussion program lakini siku hizi anaitwa mwanasiasa mmoja na kueleza masuala yake binafsi bila kuwa na jambo msingi na lenye maslahi ya umma. Kipindi hiki sasa hakijadili masuala ila ni sehemu wa wanasiasa kutoa wasifu binafsi tu. Kilipokuwa chini ya Angelo Molekwa (Sijui siku hizi yuko wapi maana alikuwa mzuri sana katika Interviews) kilikuwa na mvuto sana lakini kwa sasa kimeporomoka mno.

To me Yahya M is a very good presenter na ni kati ya Waandishi wachache wa luninga ambao wanaendesha panel discussions vizuri sana hadi unapenda kufuatilia. Hili la leo anaweza kuwa ameghafilika tu.
 
Salaam Wakuu,

Hatua ya kuanzisha thread si mbaya, kama mnaweza kunisifia publicly si vibaya pia kunikosoa publicly. Yalikuwa maoni binafsi na hayakulenga kumdhihaki mwanahabari yeyote, ama kuufunga mjadala juu ya Dr.Ulimboka kwani si jukumu langu wala sina dhamana hiyo.

Inawezekana kabisa kuna kupishana katika mawazo juu ya jambo fulani, hakumaanishi mtandao wala kumtumikia mtu yeyote kwa manufaa binafsi.

Napenda kutambua na kuheshimu kupishana huko katika fikra, lakini pia kuomba radhi sana kama matamshi yangu yamekwaza harakati muhimu katika sakata hili.

Maangalizo na Ushauri umezingatiwa.

Ahsanteni Wanajamvi

Yahya M
Huo ndio ubinaadamu bw yahaya na ni uungwana kwani muungwana ni vitendo, Kila la kheri
 
Salaam Wakuu,

Hatua ya kuanzisha thread si mbaya, kama mnaweza kunisifia publicly si vibaya pia kunikosoa publicly. Yalikuwa maoni binafsi na hayakulenga kumdhihaki mwanahabari yeyote, ama kuufunga mjadala juu ya Dr.Ulimboka kwani si jukumu langu wala sina dhamana hiyo.

Inawezekana kabisa kuna kupishana katika mawazo juu ya jambo fulani, hakumaanishi mtandao wala kumtumikia mtu yeyote kwa manufaa binafsi.

Napenda kutambua na kuheshimu kupishana huko katika fikra, lakini pia kuomba radhi sana kama matamshi yangu yamekwaza harakati muhimu katika sakata hili.

Maangalizo na Ushauri umezingatiwa.

Ahsanteni Wanajamvi

Yahya M

Hicho kipindi cha tuongee asubuhi mbona mmekiharibu mmekalia kujiongelesha wenyewe (watangazaji) maneno kibaaaao mnapoteza muda na mnaboa sana. Ni afadhali kipindi kilivyokuwa mwanzo!
 
Niseme wazi mimi nimekuwa nikimshabikia sana ndugu yangu Mwanahabari makini Yahaya Mohamedi katika vipindi vyake vya "tuonge asubuhi" amabvyo amekuwa akiviendesha kwenye television ya Star TV. Natambua mchango wako umakini wako na busara zako lakini leo asubuhi sikufurahia mchango wako kwani kwa nyakati mbili tofauti kwanza katika maada ya taarifa ya uchunguzi ya Mwangosi na Ulimboka ulitaka kutuaminisha kwamba the public had enough of it and it needed no more na ulisisitiza waandishi wa habari kupima na kuamua kutoendelea na taarifa hizo.

Sehemu ya pili ulitaka waandishi wa habari kuamini kile ambacho afande Balo alikuwa akiwaambia waandishi wa habari, kuhusu mkasa wa afisa uhamiaji, kimsingi Yahaya The police are at cossfire because of their own make. Wamedanganya sana na sasa hata ukweli wao hakubaliki kwa waandishi wa habari au umma.

Hivi yayahaya unatulazimisha vipi kuamini polisi wanasema ukweli kama huku nyuma ukweli wao umedhihirika kuwa uwongo. Polisi wameingia kwenye mtego ambao itawagharimu kwani sasa kila mtu anawaona ni watu ambao wako mbali na ukweli. Sikiliza maelezo ya awali ya tukio la Nyololo, sikiliza maelezo kuhusu kifo cha muuza magezeti Morogoro. Ukweli ukifichwa akili ya mwanadamu haikubali utupu/vacuum inatafuta taarifa kuondoa utupu sasa kazi kwa wasema uongo kuondoa ukweli unaokizana na ukweli wao.

Nina hakika na nakubali Yahaya kuwa na msimamo wa kuwa tuwaache polisi wafanya kazi yao ya weledi, lakini polisi hao walituhusisha wakati wa kuanda na kuusadikisha uongo huo. Sasa wanayokazi kutusadikisha ukweli wao.

Ndugu yangu Yahaya mwandishi yeyote duniani na hasa anaeandika habari za kitafiti au kiuchunguzi lazima awe na base ya certain opinion na kwamba ule mwanga alionao unaweza kuimarishwa au kuondolewa na taarifa anazo pata wakati wa uchunguzi, vinginevyo kama huna mwanga, biase au uelewa wa aina yoyote usifanye taarifa za uchunguzi maana huna unachokichunguza, kwa kuuliza maswali magumu ambayo wakati mwingine yanaonyesha kuwa unamwelekeza mtoa habari ni katika kutafuta taarifa zaidi ili unachokifahamu kijitenge na taarifa halisi au ukweli.

Kimsingi waandishi wanaodadidisi wasitupiwe madogo kama alivyotaka kutuaminisha Yahaya. Uandishi bora na uchambuzi unaokubalika si kusimika maoni yako kama ulivyotaka kufanya leo asubuhi. Ukiendesha kipindi kama kile asubuhi be neutral otherwise unakichafua ki[pindi. Niwie radhi Yahaya kwa hilo.

Tunatafuta uhuru ili ukweli utawale kwa watu wote na watawala, utuwekee mwanga wa uadilifu, ukapingane na nguvu ya ufisadi, uongo uzandki na umangi meza, demokrasia ya kweli na kurejesha nguvu ya utawala na uwajibikaji kwa waliowengi. Tanzania hiii haiwezi kuja kiurahisi, kama ilivyongumu kumtoa kupe anayenyonya damu na ukabaki salama lazima uyasikie maumizi makubwa lakini yatakuwa ya muda mfupi. Wako watu wananufaika na mfumo huu na wameapa kuulinda daima milele, nani anasema katika hali hii tutafika salama kamwe tusijidanganye

Tunamwombe Mungu awangazie nuru ya imani wasikie kilio cha watu wengi ili wakishindwa waende salama mapumzikoni wakisubiri kauli ya mwisho ya umma juu ya dhuluma waliotufanyia.

Tanzania hii yaja lakini hatutaipata kirahisi, wako watu mitaani leo wanasema bila uoga tuanyo CHADEMA leo kama cha siasa kwa sababu ya kazi takatifu iliyofanywa na waandishi wa habari vinginevyo kifo cha Mwangosi ilikuwa ni single ticketi ya kuelekea kuzimu kwa CHADEMA. Maneno ya awali ya kusema amepigwa na kitu kilichotupwa kutoka kwa wananchi, taarifa ya waziri wa mambo ya ndani juu ya sms ya Dr slaa ilikuwa ni kuanza mchakato rasmi wa kuandaa umma jua ya kufutwa kwa CHADEMA. Mimi siamini haya na wala sitaki kuamini haya lakini hii ni siasa ambayo watuhumiwa lazima waje na ukweli ili waaminike vinginevyo kila nafsi itaonja mauti

wasalimieni wote ambao kwao ukweli ni mwiko bila kuona masilahi yao na wale wanaowatumia kufikia matakwa yao. The ultimate power of his almighty God is soon going to be let out for a final blow out of the enemy of his children.
 
Niseme wazi mimi nimekuwa nikimshabikia sana ndugu yangu Mwanahabari makini Yahaya Mohamedi katika vipindi vyake vya "tuonge asubuhi" amabvyo amekuwa akiviendesha kwenye television ya Star TV. Natambua mchango wako umakini wako na busara zako lakini leo asubuhi sikufurahia mchango wako kwani kwa nyakati mbili tofauti kwanza katika maada ya taarifa ya uchunguzi ya Mwangosi na Ulimboka ulitaka kutuaminisha kwamba the public had enough of it and it needed no more na ulisisitiza waandishi wa habari kupima na kuamua kutoendelea na taarifa hizo.

Sehemu ya pili ulitaka waandishi wa habari kuamini kile ambacho afande Balo alikuwa akiwaambia waandishi wa habari, kuhusu mkasa wa afisa uhamiaji, kimsingi Yahaya The police there at cossfire because of their own make. Wamedanganya sana na sasa hata ukweli wao hakubaliki kwa waandishi wa habari au umma.

Hivi yayahaya unatulazimisha vipi kuamini polisi wanasema ukweli kama huku nyuma ukweli wao umedhihirika kuwa uwongo. Polisi wameingia kwenye mtego ambao itawagharimu kwani sasa kila mtu anawaona ni watu ambao wako mbali na ukweli. Sikiliza maelezo ya awali ya tukio la Nyololo, sikiliza maelezo kuhusu kifo cha muuza magezeti Morogoro. Ukweli ukifichwa akili ya mwanadamu haikubali utupu/vacuum inatafuta taarifa kuondoa utupu sasa kazi kwa wasema uongo kuondoa ukweli unaokizana na ukweli wao.

Nina hakika na nakubali Yahaya kuwa na msimamo wa kuwa tuwaache polisi wafanya kazi yao ya weledi, lakini polisi hao walituhusisha wakati wa kuanda na kuusadikisha uongo huo. Sasa wanayokazi kutusadikisha ukweli wao.

Ndugu yangu Yahaya mwandishi yeyote duniani na hasa anaeandika habari za kitafiti au kiuchunguzi lazima awe na base ya certain opinion na kwamba ule mwanga alionao unaweza kuimarishwa au kuondolewa na taarifa anazo pata wakati wa uchunguzi, vinginevyo kama huna mwanga, biase au uelewa wa aina yoyote usifanye taarifa za uchunguzi maana huna unachokichunguza, kwa kuuliza maswali magumu ambayo wakati mwingine yanaonyesha kuwa unamwelekeza mtoa habari ni katika kutafuta taarifa zaidi ili unachokifahamu kijitenge na taarifa halisi au ukweli.

Kimsingi waandishi wanaodadidisi wasitupiwe madogo kama alivyotaka kutuaminisha Yahaya. Uandishi bora na uchambuzi unaokubalika si kusimika maoni yako kama ulivyotaka kufanya leo asubuhi. Ukiendesha kipindi kama kile asubuhi be neutral otherwise unakichafua ki[pindi. Niwie radhi Yahaya kwa hilo.

Tunatafuta uhuru ili ukweli utawale kwa watu wote na watawala, utuwekee mwanga wa uadilifu, ukapingane na nguvu ya ufisadi, uongo uzandki na umangi meza, demokrasia ya kweli na kurejesha nguvu ya utawala na uwajibikaji kwa waliowengi. Tanzania hiii haiwezi kuja kiurahisi, kama ilivyongumu kumtoa kupe anayenyonya damu na ukabaki salama lazima uyasikie maumizi makubwa lakini yatakuwa ya muda mfupi. Wako watu wananufaika na mfumo huu na wameapa kuulinda daima milele, nani anasema katika hali hii tutafika salama kamwe tusijidanganye

Tunamwombe Mungu awangazie nuru ya imani wasikie kilio cha watu wengi ili wakishindwa waende salama mapumzikoni wakisubiri kauli ya mwisho ya umma juu ya dhuluma waliotufanyia.

Tanzania hii yaja lakini hatutaipata kirahisi, wako watu mitaani leo wanasema bila uoga tuanyo CHADEMA leo kama cha siasa kwa sababu ya kazi takatifu iliyofanywa na waandishi wa habari vinginevyo kifo cha Mwangosi ilikuwa ni single ticketi ya kuelekea kuzimu kwa CHADEMA. Maneno ya awali ya kusema amepigwa na kitu kilichotupwa kutoka kwa wananchi, taarifa ya waziri wa mambo ya ndani juu ya sms ya Dr slaa ilikuwa ni kuanza mchakato rasmi wa kuandaa umma jua ya kufutwa kwa CHADEMA. Mimi siamini haya na wala sitaki kuamini haya lakini hii ni siasa ambayo watuhumiwa lazima waje na ukweli ili waaminike vinginevyo kila nafsi itaonja mauti

wasalimieni wote ambao kwao ukweli ni mwiko bila kuona masilahi yao na wale wanaowatumia kufikia matakwa yao. The ultimate power of his almighty God is soon going to be let out for a final blow out of the enemy of his children.

Hakuna siku niliyowahi kukasirika kama leo nilipokuwa namuona mtu niliyemheshim na kufuatilia vipindi vyake kama Yahya akiongea pumba tena macho makavu as if kapewa kitu fulani na watu fulani ili awasafishe. Ukweli nilishindwa kuamini kama kweli huyu ni yule Yahya niliyemuamini sana kwa busara na uweledi mzuri wa taaluma ya uandishi wa habari. Naomba niwe muwazi huyu bwana kama hajapewa kitu kidogo kuisafisha serikali basi atakuwa katishwa na yeye kafyata otherwise ameanza kampeni za kutafuta ukuu wa wilaya kama Kibonde a.ka Zuzu. Maana alikuwa anaongea kama mtu aliye na hakika na kile akiongeacho! Itanichukua muda sana kumuamini tena huyu bwana kama ilivyokuwa awali na nitakuwa na kigugumizi kuukatisha usingizi wangu ili niangalie vipindi vyake star Tv. Eti anasema hivi 'IMEFIKIA WAKATI KWA WAANDISHI WA HABARI KUACHANA NA HABARI ZA DR. ULIMBOKA KWA SABABU HABARI HIZO ZINAFANYA NCHI ISITAWALIKE" KWA MANENO MENGINE TUKUBALI KUONEWA NA WATAWALA ILI NCHI ITAWALIKE. TATHMINI YA LEO: IKIWA TUTAKUBALI KUONEWA NA KUNYAMAZA KIMYA PASIPO KUITAFUTA HAKI ILI NCHI ITAWALIKE NA KAMA TUTAONEWA WOTE NA KUNYAMAZA KIMYA HAO WATAWALA WATAWALA AKINA NA NANI?
 
Kweli kabisa,hawa watangazaji wa runinga na radio na baadhi ya waandishi wa habari wa magazeti wanapenda sana kulazimisha jamii ichukue misimamo yao na iwe ya jamii nzima.wanalazimisha wanajamii waamini na kufuata imani zao na misimamo yao.hii kwa kweli ni trend mbaya sana kwa wanahabari wetu.wabadilike haraka[/QUOTE
Ni kweli mkuu, labda ni katika makala ama maoni mwandishi anaweza kuingiza maoni yake lakini katika hard news ama Sports news kwa kweli wanaharibu sana wanapoingiza maoni yao, wanataka kuifanya hiyo habari iwagawe wasikilizaji ama watazamaji, ama waanze kuipinga na kuhama katika kusikiliza ama kutazama, sijajua kama kipindi alichoongoza Yahaya alikuwa anahojiwa kutoa maoni yake ama alikuwa anaongoza kipindi. Any way, ni mfumo mbaya.
 
kweli JF ni ule ulimwengu ulionenwa kuwa "asiyefunzwa na mamaye..........."
 
Salaam Wakuu,

Hatua ya kuanzisha thread si mbaya, kama mnaweza kunisifia publicly si vibaya pia kunikosoa publicly. Yalikuwa maoni binafsi na hayakulenga kumdhihaki mwanahabari yeyote, ama kuufunga mjadala juu ya Dr.Ulimboka kwani si jukumu langu wala sina dhamana hiyo.

Inawezekana kabisa kuna kupishana katika mawazo juu ya jambo fulani, hakumaanishi mtandao wala kumtumikia mtu yeyote kwa manufaa binafsi.

Napenda kutambua na kuheshimu kupishana huko katika fikra, lakini pia kuomba radhi sana kama matamshi yangu yamekwaza harakati muhimu katika sakata hili.

Maangalizo na Ushauri umezingatiwa.

Ahsanteni Wanajamvi

Yahya M
yahya mkuu umenikuna sana big up kwa ungwana wako.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom