yahya akoswakoswa!

eRRy

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
1,125
204
1268808737_frontpageyahya.jpg


Habari zisizo na shaka zinasema kuwa mashabiki hao, wengi wao wakiwa wa Klabu ya Simba, walivamia nyumbani kwa mnajimu huyo kwa lengo la ‘kumrudi’ kutokana na kile kilichodaiwa kuwa ni kutoa utabiri feki dhidi ya klabu yao.

Siku hiyo (usiku), mashabiki wa Simba wakiwa na kiwewe cha timu yao kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2010 baada ya kuifunga Azam FC na kufikisha pointi 56 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote, waliandama hadi kwa Sheikh Yahya.
Wakiwa nyumbani kwa mtabiri huyo, mashabiki hao walikuwa wakiimba nyimbo za kumdhihaki mtabiri huyo, huku wengine wakipoteza uungwana ‘kabisa kabisa’ na kutoa matusi.

Kama hiyo haitoshi, mashabiki hao waliendelea kuporomosha maneno makali na kusisitiza kwamba ni lazima wamuone Sheikh Yahya.
Kutokana na hali hiyo, majirani wa Sheikh Yahya walitoa taarifa polisi ambapo ‘vijana wa Mwema’ walitinga eneo la tukio na kurusha risasi ambazo ziliwatawanya mashabiki hao.

Awali, ilidaiwa kuwa Sheikh Yahya alitabiri kuwa Simba ingepoteza mchezo dhidi ya Azam, hivyo isingeweza kutangaza ubingwa siku hiyo.
Hata hivyo, kabla ya timu hizo kuingia uwanjani, Sheikh Yahya alijitokeza na kukanusha habari hizo na kutoa msisitizo kwamba katika maisha yake ya utabiri hajawahi kutabiri mechi ndogo, isipokuwa hufanya hivyo kwa Simba na Yanga, tena kwa malipo.

“Ieleweke pia kuwa utabiri wa mpira niliacha tangu mwaka 1977, na nilikuwa natabiri mechi za Simba na Yanga, mimi huwa sitabiri timu ndogo. Na huwa sitabiri bure.
“Kwa sasa utabiri wa mpira wanafanya wanafunzi wangu, mimi siwezi kutabiri Simba na Azam, hata mjinga kiasi gani alikuwa akijua kuwa Simba lazima iishinde Azam, naushangaa uvumi huu,” alisema Sheikh Yahya kabla ya mechi hiyo, iliyochezwa Jumapili, Uwanja wa Uhuru, Dar.

Aliongeza: “Sijapendezwa na usumbufu kwa mashabiki wa Simba na kwa kumpakazia kitu kama hicho, inavyoonekana kuna watu wanataka kazi hii ya utabiri, lakini wanakosea sana wanaponitumia kwa kupotosha umma.
 
Natamani ningekuwepo nione jinsi huyu mzee muongo anavyotaka kutolewa uhai na wana simba
 
Magazeti ya udaku yanajua kuvuta wateja yaani ukisoma hiyo title unajua mashabiki ndio waliomimina risasi lol
 
tatizo wabongo wengi washirikina,hawapingi unajimu bali aina/matokeo ya unajimu,kikiwa cha kuwafurahisha wanakubali, cha kuwakera wanapinga, tukatae unajimu totally regardless ya matokeo
 
mi staki hata kumuona maana kanitia uwoga kuwa nikitaka kufa nimpinge kikwete na mie ndo ilikuwa mipango yangu hiyo...aaaah
 
Hakuna kitu kinaitwa utabiri1 Huwa anacheza na pyschology za watu! Huwa anajiweka kwenye position ambayo either way ataweza kutolea maelezo! Eti hatabiri mechi ndogo!
Aliwahi kutabiri kwamba mwaka 2009 Mwezi August Osama angekamatwa yako wapi? Umefika wakati tuachane kabisa na mambo ya ushirikia tumrudie Mungu wetu, maana ni kikwazo pia kwa maendeleo ya nchi yetu! Ndio maana soka letu halikui! Kazi kupasua nazi tu uwanjani! Unafikiri mchezaji atacheza kwa kujituma, mda wote anafikiri Shekhe amesema tunashinda!
 
huyo mchawi nae siku zake za kuishi si nyingi. Mungu mwenyewe atamhukumu, na kumwondosha kabisa, ni agent wa shetani, na wote mnaoenda kwake mtaanguka pamoja naye. siku hiyo imekaribia
 
Back
Top Bottom