Yahaya Hussein amtabiria rais mwenye jina K....

Pamoja na kwamba hatuamini katika unajimu, wala hatutoi usikivu wetu kwenye hizi ndumba hatari inayoikabili jamii ya watz ni kwamba huyu sheikh Yahya anayatumia majini katika kazi yake. Sasa katika kuhakikisha hizi mindsetting zake zinatimia atayatuma kwa mtu mwenye jina linaloanzia na herufi alizozitaja kutimiza azma yake. Mtu anaweza kufa kwa ajali, ugonjwa wa moyo, pumu nk na sayansi inathibitisha hivyo. Ila chanzo cha hayo magongwa ni maruhani katika ulimwengu wa kiroho ambapo science haipati kitu hapo. WANAJIMU WAMEKUWA WASEMAJI WA MASWALA YA KITAIFA TUSIPO JISAHIHISHA TUSIJESHANGAA NCHI YETU KUYAPATA YA HAITI.
 
hawa ndio wenye S
Salim
Slaa
Selelii
Sitta
Simba

hawa ndio wa H
Hosea
Husein (Mwinyi)
Harrison (Mwakyembe)

hawa ndio wenye K
Kingunge
Kikwete
Kabwe
Karamagi
Karume

kaaaaaaaazi kwelikweli

Kasema Jina linaanza na S na kufuatiwa na H.

Hivyo yaweza kuwa kwa mfano (Sio majina halisia, ila nimejaribu kuowanisha majina yenye S na H):

Said Haruna
Samweli Homel
Seif Hamadi
Saibog Huruma; na yanayofanana na hayo!
 
Jana jumatatu 01/02/2010,Nilikuwa naangalia TV ya channel 10 kipindi cha nyota zenu na sheikh Yahaya, nilishtushwa na utabiri wake ambao kimsingi alisema "Mwaka huu kutatokea kifo cha kiongozi maarufu ambaye jina lake linaanzia na S ikifuatiwa na H, vilevile mwenye jina linaloanzia na K.

Hapo kwenye bold ya red ni Seif Hamad-tuendelee na uganga!
 
Wizi mtupu... mi mwenyewe kanitabiria kwamba nitaolewa na jamaa mwenye initials JK.... Teh teh teh...
 
inabidi huyu Mnajimu awekewe mipaka ya kuongea ongea...Hivi channel 10 mmekosa vipindi vyenye kuburudisha na kuelimisha Jamii??

mi ningemshauri atabiri kipidi cha mamilioni ya African Cup of Nations avute mamililioni yote...
 
Back
Top Bottom