Yah:wanasiasa kufanya kampeni za kuhimiza wantanzania kufanya kazi

kupelwa

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
1,087
450
Ni hivi karibuni kumekuwa na takwimu za upungufu wa chakula, kama chanzo kikubwa cha mfumuko wa bei nchini.Na kumekuwa na vijisababu vya upugufu huo.Pia kumekuwa na takwimu kubwa na vijana wengi kuhama vijini kuja mijini kutafuta maisha mazruri.na je pia huku mijini ni idadi gani imeweza kupata ajira sitahiki na maisha mazuri?kwa sasa kuna takwimu kubwa ya pengo wa vijana wengi kuwa hawana ajira;ambao ndo nguvu kazi muhimu , na rasilimali tajwa katika uzalishaji kuwa ina upungufu mkubwa wa kupata ajira.Hii ni dalili na uthibitisho tosha kuwa, ari ya kufanya kazi(working spirit) ya watanzania wengi imedorola.Hii ni rasilimali muhimu sana kwa nguvu kazi yote iwe ya mijini au ya vijijini kwenye kilimo na sekta zingine.Na kila mahali utaona jamii inalalamika maisha magumu, lakini je yatabadilika bila kufanya kazi?utaona asubuhi mpaka jioni vijana wanacheza pool hata vijijii, je ni muda gani wanaenda kufanya kazi?Lakini bila kuhoji wala kushangaa kila mara utaona wanasiasa wanafanya propaganda mfu za kuneemesha vyama vyao.Ifikie bila kusita wala kuogopa wanasiasa wetu wathubutu kuhubiri na kuhimiza wananchi wafanye kazi kwa bidii na maarifa ili kujiletea maisha bora na ustawi wa maisha yao.Ni kweli ,kuna mapungufu mengi kwenye sera zetu na program au mikakati mbalimbali yenye majina kibao, lakini kufanya kazi kwa bidii hakuna mbadala kwa hilo.Uvivu na kuacha nchi imesimama, huku nchi zingine japo ndogo kuliko hata mkoa wa mtwara zinapiga hatua ya maendeleo ni jambo la aibu.Tusiache jamii na nguvu kazi kubwa inaanza kukataa tamaa.Tuijenge , na kuijengea ari kubwa na chanya ili ifanye kazi.wanasiasa wetu tuache propanganda kwa hili, tuzunguke mijini na vijijini kufanya hilo, tutajijengea jina kubwa, kuliko mengine yasiyo na maslahi ya taifa.
 
Back
Top Bottom