YAH: Nyumbu - Mheshimiwa Pinda, huu sasa utani!

mi nikisikia Pinda anaongea napata kichefuchefu kabisa..sijui alitoka wapi mpaka kuwa waziri mkuu..he is useless,he knows nothing ,absolutely nothing zaidi ya kuropoka ropoka tu
 
mi nikisikia Pinda anaongea napata kichefuchefu kabisa..sijui alitoka wapi mpaka kuwa waziri mkuu..he is useless,he knows nothing ,absolutely nothing zaidi ya kuropoka ropoka tu

grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr.................
 
unajua kuna wakati mimi hua najishika mdomo ninapomsikiliza Mh PINDA , mtoto wa mkulima anapokua anatoa mahubiri yake ya kisiasa, naamini nafasi aliyonayo imemzidi uwezo, anapapara na mambo, muoga wa maamuzi mazito, au labda anakwepa lawama, msikilizeni kwa makini, mara nyingi anaongea kama mtu wa kawaida kwenye maswala mazito yanayohitaji kauli yake thabiti kama kiongozi wa juu wa KISERIKALI,
leo asubuhi nimessikia ktk kipindi cha magazeti cha radio free Afrika, kua sheria ya manunuzi imejaa matatizo, nani chanzo cha matatizo yote ktk sekta ya manunuzi, sasa waziri mkuu anamlalamikia raia wakawaida kua sheria hiyo ni mbovu ? sasa raia huyo afanyaje ? anapaswa amwagize waziri wake anaehusika aandae Muswada wa mabadiliko ya sheria hiyo....kumbuka issue za Kingunge na waraka alivyojibu..haonyeshi kama ni sehemu ya mamlaka. Kumbuka alivyolia wakati alipobanwa ktk swala la ALBINO, Kumbuka anavyoyumba katika swala la Meremeta.....na hili la Richmond ndo kabisa linamshinda.
UWAZIRI MKUU, ni mamlaka na si mambo yanayohitaji mtu lege lege...
Swala la nyumbu na matrekta ni aina ya porojo nyingine za kilimo kwanza, ni uhuni wa kisiasa.
__________________
Mwanataaluma hutarajia kukosolewa pindi anapokosea, Daima hategemei kusifiwa pale anapotimiza wajibu!
progress.gif
 
kibaya zaidi anasema wamepata mkopo kutoka serikali ya India, Hizo hela za meremeta/buhemba zilienda wapi na kwa nini hawatoi maelezo? Na wewe Pinda, usitufanye sisi ni watoto wadogo bwana tunajua.

Mlisema nia ya Buhemba mpaka mkahamisha kambi ya jeshi ni kuipatia fedha nyumbu, sasa ile hela iko wapi?? Nakuuliza wewe Pinda, Umesoma riport ya meremeta aliyoitoa Mwanakijiji?

Kama umeisoma tueleze pesa za Buhemba zilifanya nini au ndo mmegawana na Mboma??
 
Last edited:
(Note: Kwa kweli nilitaka kuandika "huu sasa uhuni"!

Kiwanda cha jeshi Nyumbu sasa kitaunda matrekta madogo
Mwandishi Maalum, Kiteto

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amesema serikali imeamua Kiwanda cha Nyumbu cha Kibaha, mkoani Pwani, kianze kuunda matrekta madogo ya mkono, wakati maandalizi ya kukiwezesha kuyatengeneza hapa nchini, yakiendelea.

Pinda amesema hatua hiyo inalenga katika kuyawezesha matrekta hayo kupatikana kwa wingi na kwa wakati mmoja, ili kufanikisha kaulimbiu ya 'Kilimo Kwanza'.

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Engusero, wilayani Kiteto juzi mara baada ya kuzindua ghala la mazao, waziri mkuu alisema serikali imeamua kuipa Nyumbu kazi hiyo, kwa sababu kimeonyesha uwezo wa kuifanya hivyo.

Alisema tayari serikali imeshapata mkopo kutoka serikali ya India, ili kuiwezesha kiwanda hicho kufanya kazi hiyo na mafunzo kwa wafanyakazi.

Akijibu maombi ya Mbunge wa Kiteto,Benedict Ole Nangoro, ambayo yaligusia tatizo la njaa, maji, umeme na minara ya simu, waziri mkuu alisema atawasiliana na Waziri wa Nishati na Madini, ili kujua hatua iliyofikiwa na mradi wa kuvuta umeme kutoka Olboloti unaofadhiliwa na MCC.

Kwa mujibu wa Pinda, mratibu huo, umekwishatengewa fedha.
“Kata hii ina wakazi zaidi ya 9,000, hiyo ni idadi tosha na kwa vile mna mazao ya kutosha ni dhahiri kuwa mtamudu gharama za kuweka umeme,” alisema.

Pia alitumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi hao kuhusu Mfuko wa Kuendeleza Umeme Vijijini (REA), ambao kazi yake kubwa ni kutafuta mbinu mbadala za kufikisha umeme vijijini, kwa kutumia vyanzo vingine kama vile jua, upepo au kinyesi cha wanyama.

Alisema yeye binafsi atasimamia ufuatiliaji wa minara ya simu ili awasaidie kuondoa adha ya kukosa mawasiliano.Kuhusu hifadhi ya mazao ghalani, Pinda alisema ataongea na viongozi wa Benki ya CRDB na wale wa Shirikisho la Vyama vidogo vya Ushirika (SCUULT) ambao wana uzoefu na uendeshaji wa AMCOS na SACCOS za mazao, ili wawasaidie wakazi hao kuziendesha vizuri zaidi.

Maswali:
a. Fedha za Meremeta/Buhemba zilienda wapi wakati tuliambiwa ni kwa ajili ya kusaidia kiwanda hicho cha Nyumbu?

b. Kama kweli wana mpango wa kuiwezesha Nyumbu kwa nini zile fedha za EPA walizopeleka TIB zisingepelekwa huko Nyumbu?

c. Kama kweli wao wanampango wa kuhakikisha Nyumbu inakuwa ni sehemu ya kuchochea haya maigizo ya "KILIMO KWANZA" (wazee kama mimi wanakumbuka "siasa ni kilimo", Azimio la Iringa, Kilimo uti wa mgongo, )kwanini wasitenge fedha za kutosha kwa hii bajeti yao iliyopita tu wiki chache zilizopita hadi waombe mkopo India?

d. Kama kweli wanataka kuinua Nyumbu kwanini wasishirikiane na makampuni ya Kijapani au Kichina ili kutengeneza zana za kilimo hapo.. na kwanini wasiamue kufufua lile lijembe juu ya jengo pale Ubungo (UFI)? Sijui bado lipo?

Hivi mtaanza kuwa serious lini?

Ndugu yangu Mwanakijiji, fedha za EPA walipeleka hewa TIB ni kwamba hiyo hela ilikwisha liwa kwa hiyo ili kuwazuga waTZ mkulu akasema anapeleka pesa TIB lakini nakuhakikishia ukiauliza baadhi ya staff TIB wanakwambia hakuna kilicholetwa ila ni siasa tu.
 
kibaya zaidi anasema wamepata mkopo kutoka serikali ya India, Hizo hela za meremeta/buhemba zilienda wapi na kwa nini hawatoi maelezo? Pumbafu tu na wewe Pinda, usitufanye sisi ni watoto wadogo bwana tunajua.

Mlisema nia ya Buhemba mpaka mkahamisha kambi ya jeshi ni kuipatia fedha nyumbu, sasa ile hela iko wapi?? Nakuuliza wewe Pinda, Umesoma riport ya meremeta aliyoitoa Mwanakijiji?

Kama umeisoma tueleze pesa za Buhemba zilifanya nini au ndo mmegawana na Mboma??

Hapo naona umeenda mbali. Pinda ni mtu na anastahili kutendewa kama mtu mwingine yeyote hata kama anafanya madudu. Hata mataahira hawawezi kufurahi kuitwa hivyo. Watafurahi ukiwambia kuwa wao ni good boys/girls vinginevyo unaamua kutowambia kitu. Sikubaliani na madudu ya serikali ila sipendi kutukana watu (personalities).
 
Hapo naona umeenda mbali. Pinda ni mtu na anastahili kutendewa kama mtu mwingine yeyote hata kama anafanya madudu. Hata mataahira hawawezi kufurahi kuitwa hivyo. Watafurahi ukiwambia kuwa wao ni good boys/girls vinginevyo unaamua kutowambia kitu. Sikubaliani na madudu ya serikali ila sipendi kutukana watu (personalities).

Samahani, ni hasira tu lakini nime-edit na kuondoa kasoro hiyo.
 
Back
Top Bottom