Yah: Kuunga mkono CHADEMA kwa sasa

Mi nadhani tumuulize Mwanakijiji anamaanisha nini haswa anaposema "Tukishaiong'oa ccm then what?"Kikawaida,chama kinachoshinda uchaguzi ndicho kinachopewa baraka za kuunda serikali na kuongoza taifa kwa mujibu wa sera na itikadi zako walizozinadi kwa wananchi.
MKJJ ni wazi anafahamu vyema,na tumekuwa tukimpa mifano mingi tu hata ya kuhusu kumg'oa mkoloni,nduli nk.
Mwanakijiji swali kwako una maanisha nini unapouliza whats next?What exactly do you mean?Swali lako linaweza kuwa pana sana,je una maanisha mafisadi wafachukuliwe hatua gani nk?Ama unazungumzia mgawanyo wa madaraka?
Weka wazi coz lugha yetu sometimes tunaweza tukapiga kambi kwenye issue moja kisa utafsiri mbovu.

Kwa mtizamo wangu japo mimi si mwandishi wa habari wau hata mwanasiasa, na kwa uelewa wangu mdogo katika masuala ya uchambuzi, Mzee Mwanakijiji ni kuwa chama chochote kinachokuja na sera, lengo, nia na hata kutaka kutumia mali,nguvu na akili zao zote kwa ajili tu ya kuingoa CCM madarakani hakifai kwa Tanzania ya sasa. MMJ na hata mimi pia, natamani kuona chama ambacho kinakuja na sera za kumtoa mtanzania masikini hapa alipo kwenda stage nyingine japo kwa hatua moja tu. Kama nilivyosema hapo juu sijui siasa sana, lakini hata vyama vilivyopigania huru katika nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania, vyama vile vilesema vinamwondoa mkoloni ili kiwe nini kwa waliokuwa chini ya mkoloni, hili ndo MMJ analitaka lisemwe na lionekane wazi kwa wapiga kura na watanzania wengine, swala lisiwe kuitoa CCM madarakani. Hata mimi nasubiri kulisikia hilo na sio tunaingia kwenye uchaguzi kuking'oa CCM madarakani hili watanzania hawalihitaji kwa sasa.
 
Wakuu,
Mimi bado narudia pale pale na kujibu swali la MM. Kwa mfumo tulionao wa uchaguzi na wa kiutawala kuanzia executive, parliament and judiciary kuwaondoa CCM kwa sera ni far fetched idea to be honesty. Mfano si majuzi tmueona CCM walivyoishawishi mahakama kuhusu mgombea binafsi. Hivi si tunakumbuka kepten mwimbaji wa CCM alifanya vurugu uchaguzi kiteto, msajili alimfanya nini, tume ya uchaguzi ilimfanya nini!!! ingekuwa CUF au CHADEMA ungemuona msajili, na tume ikimuangukia. Mumesahau kuwa msajili wa vyama kwa kushirikiana na habari ikulu walimtetea Kikwete eti alikuwa anatania,.! Kwa mfumo uliopo sera za wapinzani hata ziandikwe na malaika kuishinda CCM na kuiondoa madarakani ni ngumu. Hawa CCM wamehodhi kila kitu.
Opportunity iliyopo ni moja, wapinzani waingize wabunge wengi hata kama hawafiki nusu, kusaidiana na akina slaa. Kwani mnadhani yale mazuri yanayotokea bungeni si nguvu za akina Dr Slaa pamoja na uchache wao. Fikiria tungekuwa na akina Slaa 45 wakajipenyeza kwenye vikamati vya bunge, isingetokea miujiza lakini tungepiga hatua sana na mabadiliko yangeanzia hapo.
Kwa sura nyingine MM, CCM waking'oka then tunakula sahani moja na waliopo! KANU walipong'oka ndipo rasimu ya katiba ilipoandikwa na ukifanikiwa kwahili ndio mwanzo wa mabadiliko. Je Kenya is better than before,? absolutely yes! ukiacha vurugu za uchaguzi zilizoanzishwa na tume ya uchaguzi [kama ya kwetu] democracy ili prevail. Kenya is better kwa sababu hata rasimu ya katiba inajadiliwa kwa uwazi na unaona kampeni za kidemokrasia kabisa, hili si mafanikio!
Zambia is better now than before! yes! kwani wamejenga mfumo wa pili [alternative way] wa kubadilisha serikali na wananchi wanajua kuwa kama serikali haileti mafanikio unaweza iondoa bila kuwa na matatizo, is this not an achievement? Sisi bado tunaamini kuwa bila CCM no Tanzania, tunajifananisha vipi na wenzetu!
Je Zambia na Kenya zimebadilika kiuchumi kwa kubadili vyama! doubtful, na nasema pengine hakuna,lakini wenzetu wana pa kuanzia si kama sisi.
So what next!!! kuvunja misingi ya kuhodhi ya CCM, ili tuwe na tume huru, msajili huru na mahakama huru, baada ya hapo ndipo ushindani wa sera utakuwa na tija. Tunavunje misingi ya CCM,? ni kuwa na opposition MP kwa kuungana pale inapobidi.
MM, usiweke mkokoteni mbele ya farasi.
Je CCJ walikuwa na vision? the answer is NO, kwani hawakujua kuwa kuanzisha chama within 8 month ilikuwa ni blunder!
Watupwe akina mpendazoe hata kama waliharibu, No ! tunaweza pata mchele ndani ya pumba japo ni punje chache lakini kwa wakti huu tunahitaji punje hata kama ni moja.
MM, ana hoja yenye mantiki, lakini tatizo ni kuwa anaamini kuwa kuku ndiye aliyetaga yai, na anaogopa nadharia ya kuwa huenda yai ndilo lilitotoa kuku. MM, I appreciate and understand your concern, but look at the issue with different perspective.

Thanks
 
Mwanakijiji

Mawazo yako ni mazuri hila kunatakiwa kuwa na approach, mtoto hawezi kuwa hajazaliwa akafikiria kukimbia, hili haliwezekani. Na hiki ndicho kilichokuwa kikwazo kwa CCJ. Huwezi kumwambia mwenye madaraka kuwa nikikutoa madarakani nitakufunga wakati unataka huruma yake ili uweze kupata madaraka hayo. Tanzania bado ina process katika kufikia hicho unacho kiongea. Huwezi kuwa na Marengo kibao kwa wakati mmoja na ukayafikia kirahisi. Hata jeshini wanakwambia mtambue adui yako kwanza. Hiyo mipango unayoisema ni katika second stage.
 
Haaa haa haaa Mzee Mwanakijiji nataka nikukumbushe yafuatayo. Katika biblia Yesu aliwaambia wanafunzi wake 'UTAFUTENI KWANZA UFALME WAKE NA HAYO YOTE MTAZIDISHIWA'. Wakati wa kupigania uhuru wa taifa la Ghana, Baba wa taifa hilo Kwame Nkrumah alitoa usemi maarufu unaofanana na ule wa Yesu, akasema 'UTAFUTENI KWANZA UHURU NA MENGINE YOTE YATAFUATA'. Hapa Nkrumah hakutaka kupoteza muda kufikiri eti baada ya uhuru atafanya nini, wala wananchi wake hawakumkataa eti kwa vile hajawaambia baada ya kupata uhuru atawafanyia nini. Sasa haya ya kutaka Chadema iseme ikiing'oa CCM kitafuata si hoja ya msingi, cha msingi saa hizi ni kuiing'oa CCM na mengine yatafuata.
 
Bila ya kuiondoa CCM madarakani au hata kuipunguzia madaraka yake katika muhimili muhimu kama Bunge swali lako Mwanakijiji halina jibu linalojitosheleza kwa sasa. Kinachotakiwa kwanza ni WATANZANIA wenyewe waiondoe CCM madarakani au Bungeni. Kenya au Zambia ni VIONGOZI waliondoana madarakani.
 
Mwanakijiji

Mawazo yako ni mazuri hila kunatakiwa kuwa na approach, mtoto hawezi kuwa hajazaliwa akafikiria kukimbia, hili haliwezekani. Na hiki ndicho kilichokuwa kikwazo kwa CCJ. Huwezi kumwambia mwenye madaraka kuwa nikikutoa madarakani nitakufunga wakati unataka huruma yake ili uweze kupata madaraka hayo. Tanzania bado ina process katika kufikia hicho unacho kiongea. Huwezi kuwa na Marengo kibao kwa wakati mmoja na ukayafikia kirahisi. Hata jeshini wanakwambia mtambue adui yako kwanza. Hiyo mipango unayoisema ni katika second stage.

pole pole karibu unanipata...

mwenzenu Obama alisema mapema kabisa kuwa akiingia madarakani atafanya nini... watu hawakuwa na kukisia kuwa sera yake ilikuwa ni kuwaondoa tu republican madarakani halafu mengine yangekuja mbele ya safari. Wapiga kura waliambiwa sera za Obama kuhusu Guantanamo, vita, uchumi n.k
 
Haaa haa haaa Mzee Mwanakijiji nataka nikukumbushe yafuatayo. Katika biblia Yesu aliwaambia wanafunzi wake 'UTAFUTENI KWANZA UFALME WAKE NA HAYO YOTE MTAZIDISHIWA'. Wakati wa kupigania uhuru wa taifa la Ghana, Baba wa taifa hilo Kwame Nkrumah alitoa usemi maarufu unaofanana na ule wa Yesu, akasema 'UTAFUTENI KWANZA UHURU NA MENGINE YOTE YATAFUATA'. Hapa Nkrumah hakutaka kupoteza muda kufikiri eti baada ya uhuru atafanya nini, wala wananchi wake hawakumkataa eti kwa vile hajawaambia baada ya kupata uhuru atawafanyia nini. Sasa haya ya kutaka Chadema iseme ikiing'oa CCM kitafuata si hoja ya msingi, cha msingi saa hizi ni kuiing'oa CCM na mengine yatafuata.

inanikumbusha kisa cha jamaa walioenda kuwaokoa watu waliokuwa katika shida; watu wale kwa vile walikuwa katika shida walikumbatia kwa haraka "waokoaji" wao hao ambao walisema wamekuja kuwatoa katika shida zao. Baada ya kutoka kwenye shida wakawauliza waokoaji wao "sasa mnatupeleka wapi"? waokoaji wakasema "msiwe na wasiwasi tutajua baada ya muda si mrefu, nyie tufuateni tu".. guess what happened?
 
Kundi zima la wabunge wa CCM wanaweza kutoka baada ya bunge kuvunjwa na kujiunga na Chadema na kutoka hao akapatikana mgombea wa Urais wa Chadema kama inavyotarajiwa. Hii inaweza kuwa habari kubwa sana na mtikisiko kwa jukwaa la siasa. Kwa wengine hilo laweza kutosha kabisa kufanya waamini kuwa saa ya mabadiliko imefika. Kwangu mimi bado nitaangalia kwa macho ya shuku hadi nijue wanataka kufanya nini. Wakisema wanataka tu KUINDOA CCM MADARAKANI au KUONGEZA IDADI WA WABUNGE, nitawaangalia halafu nitacheeeeeeeka!

Chadema kinaweza kabisa kuwa chama ambacho kitachukua uongozi wa nchi mwaka huu, endapo tu KITATAKA.

MM
Naanza kwa kukupa pole Mzee Mwanakijiji, najua you are wounded, kwa vile mimi pia naelewe what wounded means, hujakubali kuwa umejeruhiwa hali inayopelekea kujua wazi utashindwa ila inajifariji kwa maswa mengi tuu mengine ya kutokubali kutoa sababu ya kipigo. Hiyo ni despair.

Wakati ukipiga debe la CCJ, nilisema hiyo ni ngoma, ikipigwa sana, itapasuka, ngoma imepigwa, imepasuka na bado haukubali ngoma imeisha, bado unajiaminisha utaishona na itaspigwa tena.

Pia nilishauri, it is not too late to jump ship, hatimaye viongozi wenu wengine ni maboya tuu, wamesalimu amri na wamejump ship, tatizo wengine ni wepesi mno, watapeperushwa hata na upepo tuu.

Kuna baadhi ya maeneo, nakubaliana na wewe, haswa katika eneo la ushirikiano, Chadema peke yao, hawawezi, ndio maana hoja ya kuimarisha ushirikiano bado ipo. Kama Chadema itafanikiwa kuingia madarakani baada ya October, kutafuatia ombwe la uongozi kwani timu iliyopo peke yake haitoshi ndio maana wewe Mzee Mwanakijiji, mimi, yeye na yule, tunatakiwa tuunganishe nguvu against a common enemy tusonge mbele.

Kwa vile wewe ni mmoja wa ma theorist wazuri tuu, unganisha theories zako na ma practicals wazuri ili kuzigeuza into workable stragegies to bring about the change we are looking for.

Huu sasa sio wakati wa kuuliza maswali, au kutafuta majibu kwa maswali ya kificho yaliyo moyoni, huu sasa ni wakati wa kutoa ulichonacho na kushare na wengine wenye nia moja.

Vinginevyo Mzee Mwanakijiji, nitaendelea kukuweka kwenye position yako halisi, kuwa you are a man with a mission, yaani uko kazini, endelea na kazi,

Kazi Njema.

Pasco
 
Naanza kwa kukupa pole Mzee Mwanakijiji, najua you are wounded, kwa vile mimi pia naelewe what wounded means, hujakubali kuwa umejeruhiwa hali inayopelekea kujua wazi utashindwa ila inajifariji kwa maswa mengi tuu mengine ya kutokubali kutoa sababu ya kipigo. Hiyo ni despair.

very wrong.. wounded I'm not. Ila watakaokuwa wounded watakuja na kuonekana. Kama katika mapambano ingekuwa ni kila mmoja anasimama na kubembelezana na kushangiliana mapambano yasingefaa kupiganwa.
 
Tafadhali MKJJ usikwepe swali karibu watu mia kwa wewe mmoja 100/1 wanakuuliza swali lile lile 'NINI MAWAZO YAKO AU NINI KIFANYIKE KABLA YA KUING'OA CCM' hutaki kuwajibu. Tatizo ninaloliona ni inawezekana hata wewe huna jibu au hujaandaa jibu.

Haiwezekani mkusanyiko wa mawazo ya watu zaidi ya mia kutoka sehemu mbali mbali duniani na elimu mbalimbali waliyonayo kukosa kukuelewa wewe unataka nini, basi utakuwa na mawazo ya kitume maana hata Yesu na Muhamad hawakueleweka kwa wengi walichokuwa wanahubiri.

Nafikiri swali lako linajibiwa na SERA na strategies za chama (short and long term plan).

Ukiniambia chama fulani hakina sera hapo nitakuelewa, kinataka madaraka ili kiyafanyie nini. Na kama unataka sera za vyama mimi huwa na bank ya sera na ilani ya kila chama nitakubandikia, labda tuanze kuchambua udhaifu wa sera hizo na strategies za kila chama zinavyotofautiana.
 
Mwanakijiji je unayo aina ya CCM iliyongolewaa madarakani?????

ukiwa na jibu au majibu hayo basi hiyoo ndiyoo Tanzania ya kusonga mbele.. ndio maana kwa sasa ni muhimu zaidii KUINGOA CCM MADARAKANI.
 
very wrong.. wounded I'm not. Ila watakaokuwa wounded watakuja na kuonekana. Kama katika mapambano ingekuwa ni kila mmoja anasimama na kubembelezana na kushangiliana mapambano yasingefaa kupiganwa.
Mzee Mwanakijiji, war has only two sides, the winner and the looser. Katika ile vita ya usajili wa CCJ ili mshiriki uchaguzi wa October, sio lazima mkubali mmeshindwa kwa kutoa tena press release au kufanya press conference pale Maelezo, kunyamaza tuu kimya na manahodha kuhamia Chadema, ni taarifa tosha. Katika hali kama hiyo, wote walioamini on CCJ watakuwa wamejeruhiwa, hivyo Mzee Mwanakijiji, ukubali usikubali, utakuwa pia umejeruhiwa, unless ulikuwa uko kazini tuu, then ni kazi as usual, ndio maana nikaanza na pole,

Pole Mzee Mwanakijiji, Poleni CCJ wote, kujikwaa na kuanguka sio mwisho wa safari, unaamka, inajifuta vumbi, unatafuta chombo kingine cha kukufikisha mwisho wa safari yako, ndio maana baadhi wameamua kupanda jahazi la Chadema, wengine watapanda CUF, na wale wenye kazi zao, watarejea ngamani, CCM, kama mwenda tezi na homo, hurejea ngamani!.
 
well kama inakufanya ujisikie vizuri "asante"..
 
Tafadhali MKJJ usikwepe swali karibu watu mia kwa wewe mmoja 100/1 wanakuuliza swali lile lile 'NINI MAWAZO YAKO AU NINI KIFANYIKE KABLA YA KUING'OA CCM' hutaki kuwajibu. Tatizo ninaloliona ni inawezekana hata wewe huna jibu au hujaandaa jibu.

Haiwezekani mkusanyiko wa mawazo ya watu zaidi ya mia kutoka sehemu mbali mbali duniani na elimu mbalimbali waliyonayo kukosa kukuelewa wewe unataka nini, basi utakuwa na mawazo ya kitume maana hata Yesu na Muhamad hawakueleweka kwa wengi walichokuwa wanahubiri.

Nafikiri swali lako linajibiwa na SERA na strategies za chama (short and long term plan).

Ukiniambia chama fulani hakina sera hapo nitakuelewa, kinataka madaraka ili kiyafanyie nini. Na kama unataka sera za vyama mimi huwa na bank ya sera na ilani ya kila chama nitakubandikia, labda tuanze kuchambua udhaifu wa sera hizo na strategies za kila chama zinavyotofautiana.
Luteni, sio lazima kila anayeulizwa swali ajibu haswa 'men in mission', huangalia tuu kutekeleza mission, once the mission is accomplished, the rest is nothing, CCJ is over, dead and no more! unamuuliza Mzee Mwakijiji nini kifanyike ili awape njia ya kufika msikotakiwa kufika ili iweje?.
Mambo mengine ni kazi za watu, nyie endeleeni kuuliza tuu!
 
well kama inakufanya ujisikie vizuri "asante"..
Kubali tu Mwanakijiji kwamba CCJ ilianza kwa kujimaliza mapema na wewe kwa kuwa hauko Tanzania ulishauriwa vibaya kuhusu hawa jamaa haukuligundua hili. Na sio wewe tu katika hili. Hata Mpendazoe ambaye tunaye hapa nchini sielewi alipiga mahesabu gani ikiwemo kuachia milioni 43 ambazo wenzake wameanza kuzichota tangu Julai mosi. CCJ waliohamia CHADEMA jana hawana chao. Hawatapata hata Udiwani.
 
Siasa zinachosha.....:A S confused:... Ngoja nikaandae Misa ya mchana...

Kuna washiriki wangapi wa Meza ya bwana hapa?
 
Luteni, sio lazima kila anayeulizwa swali ajibu haswa 'men in mission', huangalia tuu kutekeleza mission, once the mission is accomplished, the rest is nothing, CCJ is over, dead and no more! unamuuliza Mzee Mwakijiji nini kifanyike ili awape njia ya kufika msikotakiwa kufika ili iweje?.
Mambo mengine ni kazi za watu, nyie endeleeni kuuliza tuu!

pasco pasco unataka kusema nini?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom