Kwa upande mwingine chadema nao wawe makini wasije wakawa kama NCCR mageuzi ya wakati ule ambapo ilisambaratika baada ya uchaguzi. all in all tunawatakia kila lakheri katika michakato yao angalau wapunguze vijembe na majivuno ya CCM ambayo yanatulaza njaa kila siku.
Kwa kadiri ya kwamba lengo ni kutaka tu kuwang'oa CCM madarakani halafu ndiyo mfikirie mtafanya nini kwa taifa na kutuambia basi mtaendelea kuwa wasindikizaji kama ilivyokuwa kuanzia 1995 hadi sasa na itakavyokuwa milele na milele.
Bila ya shaka, lakini tushikamane kwenye kitu gani? bado naambiwa "kuing'oa CCM madarakani"; nauliza ili kiwe nini? jibu "ili itoke madarakani", nauliza halafu kifuate nini? naambiwa "hilo si la msingi kwa sasa kujua, tukishawatoa madarakani ndiyo tutawaambia"! Well.. mshikamano wa namna ndugu zangu nyie shikamaneni na ng'anganianeni kabisa na mgandane kama yule sungura alivyojagandishwa kwenye sanamu akidhania anaikomoa kule shambani.
Please,kwa maneno mepesi kabisa tufahamishe NINI KIFANYIKE BADALA YA KUING'OA CCM MADARAKANI?
Kuindoa CCM madarakani na Kuongeza idadi ya wabunge ndicho hasa knatakiwa kufanyika.
Nadhani itabidi niende ndani zaidi kuelezea kile ninachokiita "Tatizo la Chadema". Natumaini nitaeleweka, na siyotkuwa nimechelewa. Niwatoe hofu kabisa kwangu mimi hata CCM ikiondolewa kesho madarakani sitolia!! Lakini sitorukaruka kwa furaha! Nitauliza swali hili hili ninaloliuliza sasa.. "then what"? Nakataa kabisa kuwa hatuwezi kuwa na ajenda ya uchaguzi inayosema "tuiondoe CCM kwanza"! Hii ni ajenda ya kuondoa chama kimoja na kukiweka kingine. Yatakuwa yale yale ya KANU na RAINBOW coalition! Well RAINBOW walifanikiwa kabisa kuiondoa KANU, lakini is Kenya better today than during KANU's rule? Tutapata majibu tofauti sana kwenye hilo. Je Zambia chini ya Chiluba baada ya kuiangusha ZANU je walikuwa bora zaidi kwa sababu kina Chiluba walitimiza ndoto yao ya kumuangusha Kaunda?
Hili swali hata kama mtalikwepa, mtalibeza au mtajaribu kuonesha kuwa hamlielewi mtalazimika kulijibu tu one of these days. I know you will.
Kwa vile linaonekana ni gumu mno/halielewi au halijaulizwa sawasawa itabidi nilivunje vunje katika vipande vyake vidogovidogo. CHADEMA WAKILIELEWA NA KULIJIBU KABLA YA UCHAGUZI WATASHINDA KWA KISHINDO!
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu bado unakwepa swali uloulizwa wewe. Unataka Chadema wafanye nini?.. maanake yaonyesha wewe unauliza swali ukiwa na jibu tayari kichwani. Chadema wameeleza itikadi yao sera zao ilani zao bado kitu gani haswa ambacho wewe kinakukwaza? Je hukubaliani na itikadi zao kama ndivyo nakumbuka ulishindwa kutueleza kule ktk mada iliyopita kuhusiana na sera za Chadema wapi unapingana nao pamoja na kwamba niliposoma sera za CCJ walichotofautiana zaidi ni kimaandishi tu.
Pili sidhani kama hao CCJ wengine waliojiunga na Chadema ni wajinga kiasi hicho, hawakutazama mapungufu uloyaona, wao wakaenda kukaa na viongozi wa Chadema wakjayaweza wazi maswala yao hadi imefikia wao kujiunga.Huu ndio ustraabu lakini kuja hapa JF ukaendelea kuuliza kitu ambacho hakieleweki ati Then What?
Kisha umetoa mfano wa KANU na Coalition, sijui kama unajua kwamba hata hiyo Kanu yenyewe ilikuwa coalition ya vyama vitatu kama tunavyoizungumza CCM leo hii. Kanu ilitokana na vyama vitatu - chama cha Jomo Kenyatta - KAU,Tom Mboya - NPCP na Oginga Odinga -KIM hawa ndio waliungana pamoja ku form KANU na kama unakumbuka vizuri..CCM pia haina tofauti toka TANU hadi CCM yenyewe ni coalition zilizowezesha umoja wa jumuiya zetu kutokana na WATU na MAZINGIRA tulokuwa nayo.
Huwezi kutumia mifano ya US ya kiitikadi kujenga UMOJA katika nchi ambayo wewe mwenyewe unakubali hakuna haki. Nitarudia kusema tazama South ANC na PAC hawa wote walikuwa na itikadi tofauti lakini ilipofikia swala la kumwondoa mkoloni na Apartheid that became priority number one..Tazama Zimbabwe, Zambia yenyewe wakati wa Kaunda mbinu zilizotumika ni sawa na hizi tunazotangaza hapa leo hii..
Mkuu wangu huwezi kuvuta umati wa kiafrika kwa kutumia itikadi isipokuwa kwa kumwondoa adui aliyepo madarakani na zipo nchi nyingi sana zimefanikiwa ikiwa unataka kutumia mifano kama hii.. South Afrika chini ya Mandela ni mfano mmoja mkubwa sana wa mafanikio ambao dunia nzima wanawapongeza hivyo hata hao Yankees walijiunga state hadi state kupambana na ukoloni wa Malkia wasijue itikadi gani wataitumia kutawala lakini baada ya kumwondoa Malkia ndipo fikra za itikadi zinakuja...
What next? haina mwisho mkuu wangu na kwahakika naweza kujibu kuwa -Tutahakikisha Mafisadi wanafikishwa mbele ya sheria na ukaendelea kuuliza what next?.. nikajibu Tutarudisha uhuru na haki mikononi mwa wananchi - what next? hivyo hivyo tukajaza kurasa na kurasa za maswali ya kufikirika kuandika hadithi ndefu kwa mkono wa Binadamu..
It's ONLY God knows mambo ya What next itazaa kitu gani, sisi tunapanga tunayoyaweza leo kulingana na mazingira tuliyopo. Hatuwezi panda mbegu zetu kwenye jiwe tukitegemea mavuno bora wala hatuwezi panda mahindi tukitegemea kuvuna mpunga sisi hatuko huko kabisa...isipokuwa tunachozungumza hapa ni kupata kwanza hati milki ya ardhi ambayo itatumika kwa kilimo. Kilimo ambacho kila mmoja wetu anakubali kwamba ndio uti wa mgongo wa uchumi wetu hayo ya kulima mpunga, mahindi au chochote unachofikiria wewe yatajulikana mbele ya meza kuu baada ya kupata haki miliki ya ardhi..
Hizo then what - tutalima kinachoweza kustawi - then what, then what - then what.. yoote itakuwa ktk historia ya nchi kama vile historia ya maisha yako ulitaka kuja Marekani -then what? - umefika US - then what?. haya maswali kweli tutafika!.
Leo hii hatuna hata kiwanja mkuu wangu unataka tufikirie kujenga maghorofa!
Tunakuuliza wewe utajibu vipi?.. au wataka hao Chadema wakujibu vipi.. frankly kama mimi ni kiongozi wa Chadema sintakuwa na jibu, ikiwa wewe hukupata jibu toka ktk katiba,sera, na ilani za chama - sijui unategemea jibu litoke wapi kujibu swali lisilojulikana..well, nyinyi endeleeni kulikwepa swali la "then what" na mimi nitaendelea kuliuliza. Kwa sababu naamini mabadiliko tunayoyataka lazima yajaribu kujibu swali hilo. Kwa upande wa Chadema wafanye nini well, sidhani kama wako tayari kusikia. So, nyinyi endeleeni kuwatia shime wasijaribu kujibu swali hili na mimi nitaendelea kuwauliza. Hata kama siyo popular kuuliza swali hilo ambalo si gumu kama wengi wanavyotaka liwe.
Tunakuuliza wewe utajibu vipi?.. au wataka hao Chadema wakujibu vipi.. frankly kama mimi ni kiongozi wa Chadema sintakuwa na jibu, ikiwa wewe hukupata jibu toka ktk katiba,sera, na ilani za chama - sijui unategemea jibu litoke wapi kujibu swali lisilojulikana..