Yah: Kuunga mkono CHADEMA kwa sasa

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Nilifahamu juu ya mazungumzo ya baadhi ya uongozi wa juu wa CCJ na Chadema kwa muda kidogo; Yalitokana vile vile na ushauri wa watu mbalimbali kuwa CCJ iunganishe nguvu na Chadema. Hata hivyo hadi hivi sasa kilichofanyika ni baadhi tu yaviongozi wake kujiunga na Chadema na siyo CCJ nzima. Kuna sababu.

Wapo wanaosema kwa vile hawa ndugu zetu wameingia Chadema basi CCJ na wazo la CCJ nalo limekufa kwa hiyo sote tuliounga mkono CCJ tuinamishe vichwa vyetu kwa kushindwa na kujiunga na Chadema. Hizi ni fikra potofu. Ni potofu kwa sababu zinafikiria Chama kikifa au kikishindwa ina maana mawazo yake nayo yameshindwa. Yanafikiria kuwa kama watu wakitoka kujiunga na chama kingine au kutoka katika siasa maana yake siasa za chama hicho nazo zimeshindwa.

Ukweli unabakia kuwa ukweli kwamba siasa za kutaka ushirikiano wenye lengo la kuitoa tu CCM madarakani halafu ndiyo tujue tunataka kufanya nini ni siasa ambazo katika dhamira yangu siwezi kuziunga mkono. Siasa za kutosema nini unataka kufanya, kwa vipi na kwa muda gani ukionesha ukali kuhusu ufisadi miye siziwezi kwa sababu niaamini tatizo la Tanzania ni ufisadi kuliko kitu kingine chochote kile.

Kutuambia kuwa "panya hawakamatani" lakini hutuambii wewe utawakamata vipi na kwa namna gani, haitoshi vile vile.

Chadema ni tumaini kubwa sana kwa wengi wetu na kwa muda mrefu limekuwa kwangu ni tumaini vile vile. Lakini bado haijataka kuvuta mstari ule wa kiungozi kwa miaka kadhaa sasa. Siamini kama ndani ya siku chache zilizobakia wataweza kuvuka mstari huo. Na watakapogundua kuwa walipaswa kuuvuka watajikuta wanagalagazwa kwenye uchaguzi mkuu huku wakilalamika "CCM", "Tume ya uchaguzi", "Wizi wa kura", "Vyombo vya dola".

Ninawatakia kila la kheri wale wanaojiunga na Chadema wakiamini kitabeba matarajio yao. Hiyo ni demokrasia na kwa hakika kabisa nawatakia mafanikio.

Kwangu mimini bora nirudi na kutokuwa na chama nikiendelea kusimamia fikra na itikadi na mambo ninayoyaamini kuliko kupanda treni ambalo siju linakwenda wapi na kwa nini ati kwa sababu wengine wamepanda na wanashangilia!

Kundi zima la wabunge wa CCM wanaweza kutoka baada ya bunge kuvunjwa na kujiunga na Chadema na kutoka hao akapatikana mgombea wa Urais wa Chadema kama inavyotarajiwa. Hii inaweza kuwa habari kubwa sana na mtikisiko kwa jukwaa la siasa. Kwa wengine hilo laweza kutosha kabisa kufanya waamini kuwa saa ya mabadiliko imefika. Kwangu mimi bado nitaangalia kwa macho ya shuku hadi nijue wanataka kufanya nini. Wakisema wanataka tu KUINDOA CCM MADARAKANI au KUONGEZA IDADI WA WABUNGE, nitawaangalia halafu nitacheeeeeeeka!

Chadema kinaweza kabisa kuwa chama ambacho kitachukua uongozi wa nchi mwaka huu, endapo tu KITATAKA.

MM
 
Inaelekea wewe ni CHADEMA damu damu, na una kazi maalum unafanya kwa ajili ya CHADEMA.
 
Naungana na wewe kwamba hawa CHADEMA wanalo tegemeo kubwa la kupata wanachama wa kutosha kutoka CCM baada ya bunge kuvunjwa. Kutokana na colum yako nimeelewa ni kwanini wamekuwa wazito kutangaza mgombea Urais wao. Lets hope atakuwa ni mtu makini.
Lakini ninafikiri pamoja na dhamira nyingine ambazo upinzani unaweza kuwa nazo, ya kuing'oa CCM ni lazima ipewe msisitizo. Unapokwenda vitani, dhamira ya kwanza huwa ni kumshinda adui, baada ya hapo ndo unakaa sasa kupanga mikakati ya kuijenga vita wakati umeshashinda vita. Huwezi kupanga mikakati ya kesho wakati hujui utaishindaje vita. Ila sema hofu yangu ni kwamba isije kuwa hawa viongozi wa CCJ ni viini macho tu kwa watanzania. Na si ajabu akina Mpendazoe na rafiki zake wametumwa na CCM kwenda kuisambaratisha CHADEMA (ni mtizamo tu though ninaamini una ukweli mwingi).
 
my signature means alot kuliko kusubiri. Alichokifanya Mpendazoe nilisema once he joined CCJ but kimetimia leo nampongeza. Bora kugonga mtembea kwa miguu kuliko kuangusha basi.
 
Naungana na wewe kwamba hawa CHADEMA wanalo tegemeo kubwa la kupata wanachama wa kutosha kutoka CCM baada ya bunge kuvunjwa. Kutokana na colum yako nimeelewa ni kwanini wamekuwa wazito kutangaza mgombea Urais wao. Lets hope atakuwa ni mtu makini.
Lakini ninafikiri pamoja na dhamira nyingine ambazo upinzani unaweza kuwa nazo, ya kuing'oa CCM ni lazima ipewe msisitizo. Unapokwenda vitani, dhamira ya kwanza huwa ni kumshinda adui, baada ya hapo ndo unakaa sasa kupanga mikakati ya kuijenga vita wakati umeshashinda vita. Huwezi kupanga mikakati ya kesho wakati hujui utaishindaje vita. Ila sema hofu yangu ni kwamba isije kuwa hawa viongozi wa CCJ ni viini macho tu kwa watanzania. Na si ajabu akina Mpendazoe na rafiki zake wametumwa na CCM kwenda kuisambaratisha CHADEMA (ni mtizamo tu though ninaamini una ukweli mwingi).

Bora tungetafuta dawa ya UKIMWI kabla haujaingia TZ
 
Asante mzee ila tatizo letu wabongo tulowengi hatutaki kufumbua macho ili tuone uozo wa chama cha mababu ndo maana tunabaki na mtazamo hasi na mfinyu kwa upinzani. Come oktoba fanyeni kweli!
 
Kwa upande mwingine chadema nao wawe makini wasije wakawa kama NCCR mageuzi ya wakati ule ambapo ilisambaratika baada ya uchaguzi. all in all tunawatakia kila lakheri katika michakato yao angalau wapunguze vijembe na majivuno ya CCM ambayo yanatulaza njaa kila siku.
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu wangu nimekusoma lakini nadhani umekuwa mwepesi sana wa kusahau mengi yaliyopita. Binafsi sidhani kama kuna watu waliopigana na Ufisadi kama sii wewe mwenyewe, Dr.Slaa, Zitto, Chadema kwa ujumla wake, wapiganaji wengi hapa JF pamoja na viongozi ambao wapo ktk makundi mbalimbali.. Hizi ahadi na azma ya kukomesha Ufisadi zimepigwa vita na hata JK mwenyewe tena basi naweza kusema hata mafisadi wenyewe wamelaani Ufisadi hali wao ndio vigogo. Wamesema wazi watafanya nini lakini kimetokea kitu gani? - still unataka promises!

Kwa hiyo ahadi za kukomesha Ufisadi na kipi Chadema watakifanya ni kutoamini vyombo vya sheria ambavyo pekee ndivyo vitaamua adhabu kwa wale wote watakaopatikana na hatia. Kinyume cha hapo tulichonacho ni circumstantial evidence ambazo lazima ziwe proved beyond reasonable doubt mahakamani.

Pili, nitakuwa mpuuzi kama nikianza ku question Mwanakijiji atafanya nini ikiwa atapewa nafasi ili niungane nawe wakati adui yako ndio kwanza anazidi ku gain ardhi..Hukujiunga leo itachukua another 5 years ambazo tutaendelea kupiga kelele na kupoteza usingizi hali ushindi upo within our reach..

Mkuu wangu, nitarudia kwamba fikra zimeisha orodheshwa, nia tunayo, sababu tunayo na uwezo tunao ndivyo tulivyoweza kumwondoa nduli Idd Amin kisha yaliyofuata ni historia. Walikuja kina Lule, akatoka akaja Bina Issa, Obote na leo tunaye Museveni ndio hatua za kutafuta demokrasia ya kweli lakini muhimu Waganda wameondokana na nduli Idd Amin ambaye aliufikisha uchumi wao pabaya sana. I recall 1Tsh ilikuwa sawa na Ush 1,000 mwaka 1981/82.. leo tunaenda nao sambamba kiuchumi.

Mimi nilifikiria mstari unaozungumzia ni Chadema kuweza kumchagua mgombea kiti cha Urais ambaye wewe unamkubali. Binafsi sikubaliani na fikra za kugombea Ubunge hali kiti kikubwa hakina mgombea. Nashindwa kuelewa hawa wabunge wataweza vipi kutoa ahadi zao kwa wananchi hali hawakushika mpini wa shoka. Hizi ahadi zao zitatekelezwa vipi? hao wananchi ni maskini wanaotaka kuokolewa leo wasubiri ubishi bungeni kuhusiana na katika, sheria na Muungano kwa miaka mingine mitano hali kuna uwezekano wa mtu mmoja tu - rais kutoa promise ambayo zitawezekana chini ya Utawala wake na hao wabunge wakawa nyuma ya huyo kiongozi kufikisha salaam.

Ebu nambieni, mbunge anaweza kum promise kitu gani maskini walalahoi ambao watajipanga mstari na bakuli zao mkononi..where is he gonna get the money and support! ikiwa yeye hana mamlaka yoyote zaidi ya kutunga sheria na kupitisha bajeti ambayo imeandaliwa na utawala wa JK..Kisha utekelezaji wote unategemea na rais aliyepo madarakani. Tusiwadanganye wananchi wakuu zangu..

Tumpate mgombea bora wa kiti cha Urais - sasa huyu ndiye atakayekupa salaam, huyu ndiye utajua kinachofuata ni kitu gani kwa sababu utampima ahadi zake kutokana na uwezo wa huyu nahodha..Kinyume cha hapo JK au hata RA anaweza kuzungumza yoote unayotaka ayazungumze hizo fikra, falsafa, itikadi ili mradi tu akuvute wewe..

Baada ya kifo cha mao Tse tung wale the big four ambao walikuwa wakitangaza sana fikra za Mao na kuweka sheria kali dhidi ya Ufisadi kumbe wao ndio walikuwa Mafisadi wakubwa, matajiri wasiopimika ktk mzani wa Utajiri - Mapinduzi ya China walihakikisha kwa uchafu wao wananyongwa.
 
Naungana na wewe kwamba hawa CHADEMA wanalo tegemeo kubwa la kupata wanachama wa kutosha kutoka CCM baada ya bunge kuvunjwa. Kutokana na colum yako nimeelewa ni kwanini wamekuwa wazito kutangaza mgombea Urais wao. Lets hope atakuwa ni mtu makini.
Lakini ninafikiri pamoja na dhamira nyingine ambazo upinzani unaweza kuwa nazo, ya kuing'oa CCM ni lazima ipewe msisitizo. Unapokwenda vitani, dhamira ya kwanza huwa ni kumshinda adui, baada ya hapo ndo unakaa sasa kupanga mikakati ya kuijenga vita wakati umeshashinda vita. Huwezi kupanga mikakati ya kesho wakati hujui utaishindaje vita. Ila sema hofu yangu ni kwamba isije kuwa hawa viongozi wa CCJ ni viini macho tu kwa watanzania. Na si ajabu akina Mpendazoe na rafiki zake wametumwa na CCM kwenda kuisambaratisha CHADEMA (ni mtizamo tu though ninaamini una ukweli mwingi).

hili ndilo linalowafanya Wamarekani wakome kwenda Iraq kumng'oa Saadam; mtakuja kukumbuka ninachosema.
 
Binafsi ningependa wabunge wengi zaidi wa upinzani Bungeni kwa sababu hata kama umeshinda urais halafu huna wabunge utaongozaje nchi. hapa vyote vina umuhimu wake. CHADEMA kusimamisha mgombea au kutosimamisha hakumaanishi kwamba wapinzani hawasimamishi mgombea ingawa naamini Chadema watatangaza Mgombea wao karibuni.
Naunga mkono mawazo kwamba ngonjera za nini watafanya baada ya ushindi tumezisikia sana hata kwa hao CCM lakini Je utekelezaji wake una kiwango? hapa lazima tuwe na vipa umbele, kwa sasa kipa umbele ni kumng'oa CCM madarakani, lazima hili lifanyike, bila hili mengine ni ngojera zilezile.
 
hili ndilo linalowafanya Wamarekani wakome kwenda Iraq kumng'oa Saadam; mtakuja kukumbuka ninachosema.
Mkuu wangu wewe ndio hujui dhamira ya Marekani kwenda Iraq lakini sisi tunajua na haina kificho isipokuwa wamekutana na vichaa wenye historia ya kutotawaliwa. Hawapewi pumzi ya kuyafanya waliyokusudia kuyafanya..

Hata siku moja Marekani haendi mahala pasipo malengo na wanaweza hata kutunga itikadi ili mradi malengo yao yakubalike kwa wajinga kina sisi tusioona nje ya CNN. Kumbuka mwisho wa yoote haya siku zote - TRUTH wil prevail!
 
Naunga mkono mawazo kwamba ngonjera za nini watafanya baada ya ushindi tumezisikia sana hata kwa hao CCM lakini Je utekelezaji wake una kiwango? hapa lazima tuwe na vipa umbele, kwa sasa kipa umbele ni kumng'oa CCM madarakani, lazima hili lifanyike, bila hili mengine ni ngojera zilezile.

mtapata kile kinachoitwa rude awakening... !
 
Mwanakijiji mbona hivyo mkuu? hivi wewe unadhani kushindwa mwezi =October kutatufanya tusigombee tena? Hata 2015 tutaingia kilingeni maana mapambano hayana mwisho haya. Ninao uhakika tu iko siku tutakuwa pamoja tukishuhudia mapinduzi ya kisiasa katika nchi hii.
Tushikamane twende mbele. Hakuna hata siku moja tutakuwa na matakwa sawa, lakini tukikubali kuaminiana mbele tutasogea.
 
Kwa kadiri ya kwamba lengo ni kutaka tu kuwang'oa CCM madarakani halafu ndiyo mfikirie mtafanya nini kwa taifa na kutuambia basi mtaendelea kuwa wasindikizaji kama ilivyokuwa kuanzia 1995 hadi sasa na itakavyokuwa milele na milele.

Tushikamane twende mbele. Hakuna hata siku moja tutakuwa na matakwa sawa, lakini tukikubali kuaminiana mbele tutasogea.

Bila ya shaka, lakini tushikamane kwenye kitu gani? bado naambiwa "kuing'oa CCM madarakani"; nauliza ili kiwe nini? jibu "ili itoke madarakani", nauliza halafu kifuate nini? naambiwa "hilo si la msingi kwa sasa kujua, tukishawatoa madarakani ndiyo tutawaambia"! Well.. mshikamano wa namna ndugu zangu nyie shikamaneni na ng'anganianeni kabisa na mgandane kama yule sungura alivyojagandishwa kwenye sanamu akidhania anaikomoa kule shambani.
 
of course hayuko.. Iraq ina amani zaidi kuliko wakati wa Sadaam?
Ni kweli ya wamarekani issue ya kumng'oa Saddam bila ya kufikiria mara baada ya hapo then what inawacost,lakini bado sijakubali kulinganisha na issue ya kuing'oa ccm....Hatuna matatizo kama waliyokuwa nayo Iraki,inaonekana na wewe unakubaliana na ccm kuwa wao pekee nndio wenye kuweza kukeep amani nchini kama baadhi ya watu walivyokuwa wakiamini kuwa Saddam ndiye pekee mwenye kuiweka Iraki pamoja bila ya kugawanyika,alifanya hivyo kwa njia nyingi ikiwemo kuwanyamazisha wapinzani kwa mauwaji etc....I thought the same way kuwa ni bora wakati wa Saddam,lakini sidhani kama kuna uwezekano wa kujutia na kusema ni bora wakati wa ccm....Ndoa ikikushinda ukitaka ku divorce si lazima utafute fiancee mwingine kwanza.
Kama unazungumzia itikadi,sidhani kama kutakuwepo na tatizo,kama nilivyosema hapo awali cha msingi ni kukaa chini na kufanya makubaliano kuwa whats next after joining forces....Cha muhimu ni kuing'oa ccm,hilo ni la kwanza...Sababu za kuing'oa ccm ndio zitakuwa msingi wa kuungana....Kama ni kweli sera na itikadi ya vyama hivyo viwili vinashabihiana...Then thats the begining and you can build on it.
Saddam alitolewa kwa nguvu kwa ushirikiano na serikali ya nchi nyingine,ccm watang'olewa na wapiga kura na sioni kitakachoharibika,certainly hakuna historia kama hiyo...However nakubaliana kuwa ni muhimu kujipanga ili yasitukute ya Zambia nk
Kuing'oa ccm ni ndoto na kuwa na serikali ya tofauti ni a dream come true,something most of us wishes!
ccm imegubikwa na ufisadi,kama unataka waendelee kulifisadi taifa simply kwasababu huamini kwamba wapinzania wana nia ya kufanya tofauti na ccm then hayo ni maoni yako ambayo si positive kabisa kwa mpenda mabadiliko.
 
Kwa kadiri ya kwamba lengo ni kutaka tu kuwang'oa CCM madarakani halafu ndiyo mfikirie mtafanya nini kwa taifa na kutuambia basi mtaendelea kuwa wasindikizaji kama ilivyokuwa kuanzia 1995 hadi sasa na itakavyokuwa milele na milele.

Bila ya shaka, lakini tushikamane kwenye kitu gani? bado naambiwa "kuing'oa CCM madarakani"; nauliza ili kiwe nini? jibu "ili itoke madarakani", nauliza halafu kifuate nini? naambiwa "hilo si la msingi kwa sasa kujua, tukishawatoa madarakani ndiyo tutawaambia"! Well.. mshikamano wa namna ndugu zangu nyie shikamaneni na ng'anganianeni kabisa na mgandane kama yule sungura alivyojagandishwa kwenye sanamu akidhania anaikomoa kule shambani.
Kama haya maswali waneulizwa kina Nyerere wakati wakipigania kumwondoa mkoloni ingekuwa kazi mubwa..
Hivi kweli wewe Mwanakijiji unafikiria watu wanataka kuiondoa CCM ili iwe nini?...mkuu wangu pengine sikusomi vizuri lakini mtu atataka kuondoa CCM madarakani asijue kwa nini ama kitafuata nini..sasa kwa nini wanagombea madaraka!..Bila shaka Chadema watachukua madaraka na kuhakikisha sera walizouza kwa wananchi na kukubaliwa zinafanya kazi..

Samahani lakini hivi unachotaka wewe ni madaraka yatagawanywa vipi au? maanake hata Ufisadi ni sehemu tu ya sababu za kuing'oa CCM madarakani ndani ya swala kubwa la Katiba yetu..miiko na maadili yapo ktk katiba na haya yote ni maswala yatakayopewa nafasi ktk bunge la kwanza hivyo kama wewe unalo tofali lako beba jiunge na kesho utaingia nalo bungeni kwa sababu tusifikirie kabisa kwamba Chadema wakichukua nchi basi nao watuburuze na sera ambazo wewe Mwanakijiji unazikubali..

Siku zote mhitaji ndiye husema anachokitaka na mbunge ni mwakilishi wa mawazo hayo,hivyo hata ngazi ya Kitaifa Chadema watafanya tu kile kinachohitajika na wananchi wakizingatia titikadi yao itawezesha vipi kupatikana kwake. Kila itikadi mkuu wangu ina mbinu ya kuleta kitu kile kile kinachohitajiwa Kitaifa..

LENGO ni moja isipokuwa kuna njia tofauti za kufikia lengo hilo.. Hata JK na CCM wanafikiria wanakwenda sawa kufikia maisha bora kwa kila mwananchi..Sii Chadema, CCM, NCCR TLP na wengine woote wanaamini adui yetu mkubwa ni Ujinga, Umaskini na maradhi isipokuwa tofauti zao zinakuja ktk mbinu na vipaumbele vya kutokomeza vitu hivi..

Kifupi CCM wanaamini kuvua wao kisha wape samaki maskini wasiojiweza na Chadema wanasema mfundishe maskini kuvua, kesho atakwenda mwenyewe kuvua samaki! Bado una shaka gani? mbona mimi niliwasoma mapema!
 
Pengine Mwanakijiji unatumia lugha ngumu kueleweka.Pengine tatizo liko kwangu kwamba ni mgumu kuelewa.Lakini hadi sasa nashindwa kabisa kukuelewa unapojaribu kuonyesha kuwa ufumbuzi wa matatizo yaliyopo nchini mwetu hautopatikana kwa kuing'oa CCM madarakani.

Inawezekana pia japo nilifaulu PS 101 pale Mlimani katika mwaka wangu wa kwanza,sikumwelewa Mhadhiri aliyekuwa akifundisha somo hilo (wakati huo) Dkt Max Mmuya ambaye katika mihadhara yake alikuwa akitueleza kuwa mmoja ya maelngo makuu ya kuanzisha chama cha siasa ni kukamata dola.Na hiyo,kwa namna flani,ndio inatofautisha political parties from interest and pressure groups.

Lakini hata kama wakati huo akili yangu ilikuwa changa kukamata mafundisho hao muhimu kuhusu siasa,nimetumia muda mwingine wa kutosha kusoma na kutafiti siasa kama stadi (hasa katika namna theory zinavyoendana au kukinzana na uhalisia uliopo).Na katika muda wote huo sijakutana na maandiko au njozi kwamba moja ya malengo ya msingi ya kuanzisha chama cha siasa sio kukamata dola.Umuhimu wa chama cha siasa kukamata dola unatokana na ukweli kwamba ili sera zake ziweze kufanya na/au kufanyiwa kazi ni lazima kiwe na mamlaka ya kiutawala na dola kwa umma.Na mfano mwepesi ni namna "sera za kipekee za CCJ" zitakavyoendelea kubaki "sera nzuri tu" pasipo namna ya "kulazimisha utekelezaji wake" kwa vile chama hicho hakijakamata dola.Na ni katika namna hiyohiyo,tunalazimika kukubali mabaya mengi tusiyotaka kuhusu CCM kwa vile tu chama hicho kina mamlaka ya kutekeleza matakwa yake-tupende tusipende.

Kwa vile wewe ni mchambuzi mzuri wa siasa zetu,naamini unafahamu fika kwamba kikwazo kikubwa cha maendeleo yetu ni CCM.Sasa pasipo kuondoa kikwazo hicho tutawezaje kufikia mema tunayotaka kuyafikia?Au mwenzetu utuelezeje njia mbadala ya kufikia malengo yetu wakati CCM imekumbatia dola,na kutumia vyombo vya dola kukandamiza vyama vingine vya siasa na walalahoi kwa ujumla.

Siasa na utabibu ni fani mbili tofauti lakini zinaweza kuafikiana katika namna hii:kama una matatizo ya kiafya yanayosababishwa na uvimbe unaokwaza damu kufika mahala fulani,ufumbuzi pekee ni kuundoa uvimbe huo unless kwa kuuondoa mgonjwa atakufa.Ni katika namna hiyhiyo ndio maana baadhi ya majeruhi wa ajali au vita hushauriwa kukatwa viungo vyao ili waendelee kuishi hususan kama sehemu zilizoathiiriwa zinaweza kupelekea usaha au kuoza na kuusababishia mwili madhara makubwa zaidi.Na katika siasa,ufumbuzi ni kuondoa kikwazo kinachokwaza nchi kupiga maendeleo.Na ndio maana ufumbuzi wa kadhi na uonevu wa mkoloni dhidi ya wenye nchi ulikuwa kumg'oa mkoloni.Na pia Nduli Idi Amini alipovamia Tanzania,ufumbuzi pekee tuliobakiwa nao ni kumtimua,na pel tulipoweza tukamng'ao kabisa katika utawala.

Sasa iweje kuindoa CCM madarakani kusilete ufumbuzi?Unauliza tukishaing'oa CCM itafuata nini?Kwani mwanamke anayeishi kwenye manyanyaso katika ndoa akishamtaliki mumewe mnyanyasaji kinafuata nini?Au kama gogo limeziba barabara na hivyo kukwaza magari kupita,likishaondolewa kinafuata nini?

Kuna wakati tunaoaswa kuangalia uhalisia na kukepuka matamanio ya kutaka njozi zigeuke kuwa uhalisia.Kuna wanaotaka Watanzania "waende darasani kwanza" kabla ya kuanzisha jitihada za kujikomboa.Wanachosahau ni kwamba kuna uwezekano mkubwa "tutakapohitimu somo la mbinu za kujikomboa na kujitawala" tunaweza kukuta hakuna mahala pa kufanyia kazi "kanuni tulizofundishwa darasani" kwani nchi itakuwa imeshauzwa.

Na jibu jepesi kwa swali "je CCM ikishatoka madarakani kinafuata nini" linaweza kupatikana kwenye mfano halisi wa je baada ya kumuondoa mkoloni au kumtimua nduli Idi Amin kilifuata nini.
 
Back
Top Bottom