Licha ya Waziri wa Ujenzi Mhe John Pombe Magufuli kujigamba kuwa ni muumini mzuri wa utawala wa sheria, na ameapa kulinda sheria kwa kutamka "Mungu Nisaidie" hivyo hawezi kusita kutekeleza sheria. Imebainika kuwa katika hoja ya hifadhi ya barabara Ubungo anatumia sheria feki.
Ibara ya 2 ya Kanuni za Sheia ya barabara-Tangazo la Serikali namba 161 la Tar 05/05 1967 inatamka kuwa upana wa hifadhi ya barabara zote kuu hapa nchini (Trunk Roads) utakuwa ni Futi 75 kila upande. Na Ibara ya 4 ikaweka upana maalmu kwa barabara ya Morogoro kuwa ni kati ya Futi 300 hadi 400 kati ya Ubungo hadi Kibaha.
Mara baada ya kukamilika barabara iliyokusudiwa na ibara ya 4 hapo juu mwanzoni mwa 1970s, Serikali ya awamu ya kwanza ilianzisha vijiji vya ujamaa na kuwagawia ardhi katika vijiji vya Kimara, Mbezi, Kibamba na Kiruvia.
Kifungu cha 15 cha Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya ya 1999 inatamka kuwa "Ugawaji wa ardhi uliofanywa kwa mtu au kundi la watu waishio au waliotakiwa kuhamia na kuishi katika kijiji wakati wowote kati ya tarehe 01 Januari 1970 na tarehe 31 Desemba 1977, kama ugawaji huo ulifanywa kwa mujibu wa sheria au kinyume cha sheria au bila kuzingatia sheria yoyote, sasa inathibitishwa kuwa ugawaji huo ni halali na kwamba daima ni wenye nguvu ya kutoa haki na wajibu kwa kisheria kwa kundi la watu waliogawiwa ardhi hiyo......
Kifungu cha 16 cha Sheria ya Ardhi ya Vijiji ya 1999 kinatamka kuwa"Kwa madhumuni ya kuepusha mashaka na ili kuwezesha kuwapo kwa usalama wa miliki ya ardhi na hivyo kuchangia maendeleo ya ardhi ya kijiji, masharti ya Kifungu cha 15 yatatumika kila mara ugawaji wa ardhi ya kijiji ulipofanywa na Halmashauri ya Kijiji au mamlaka nyingine yoyote mnamo na baada ya tarehe 01 Januari 1978 hadi tarehe ya kuanza kutumika kwa sheria hii na kwamba badala ya tarehe zilizotajwa katika kifungu cha 15, kumewekwa tarehe kati ya tarehe 01 Januari 1978 na tarehe ya sheria hii kuanza kutumika".
Vijiji vyote 52 vya Mkoa wa Dar es Salaam vilifutiwa hadhi ya vijiji mwaka 1985 kutokana na mahitaji makubwa ya ardhi kwa ajili ya upangaji wa Jiji hivyo kuingizwa katika Mipango Miji. Hivyo Mtu au watu waliogawiwa ardhi katika vijiji vya Kimara, Mbezi, Kibamba na Kiruvia kufikia mwaka 1985 wananufaika na vifungu 15 na 16 vya Sheria ya Ardhi ya Vijiji ya 1999 ambayo iliwekwa sahihi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Benajmin Mkapa tarehe 15 Mei 1999 ili kuanza kutumika kama sheria.
Kutokana na uwezo mdogo wa kiuchumi Serikali ya Tanzania huchukua muda mrefu kuchapisha, kusambaza na kutoa elimu ya sheria mbali mbali kwa wananchi zinazopitishwa na Bunge . Hivyo Mhe John Magufuli aliposhika wadhifa wa Waziri wa Ujenzi kwa mara ya kwanza mwaka 2000, akatumia mapungufu hayo ya serikali kusigina haki za wananchi waliokuwa wakiishi katika vijiji vilivyotajwa hapo juu kwa kuagiza kupandwa kwa mawe na mabango yanayoonyesha mwisho wa hifadhi ya barabara Mita 120 ndani ya ardhi na makazi ya wananchi hao bila ya uchambuzi wowote kufanyika kubaini ni akina nai wanapaswa kunufaika na Sheria ya Ardhi ya Vijiji.
Kuanzia tarehe 15 Mei 1999 Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya ya 1999 ilipoanza kutumiaka kama Sheria (Lwa) Ibara ya 4 Kanuni za Sheria ya Barabara za 1967 ilyoweka upana wa kati ya Futi 300 hadi 400 katika eneo kati ya Ubungo hadi Kibaha ilipoteza uhai kwa watu wote waliokuwa wakiishi katika vijiji hadi mwaka 1985. Hivyo Kanuni ya hifadhi ya Barabara iliyobaki na uhai na ibara ya 2 inayotamka kuwa Hifadhi ya barabara zote kuu hap nchini ni Futi 75 kila upande. Hata Master Plan ya Jiji la Dar es Salaam ndiyo iliadopt ibara hiyo wakati inatengenezwa mwaka 1979.
Kwa mantiki hiyo lilikuwa kosa kubwa kwa Mhe John Magufuli kuagiza mawe na mabango yanayoonyesha mwisho wa hifadhi ya barabara kupandwa Mita 120 ndani ya ardhi na makazi ya wananchi kati ya Ubungo hadi Kiruvia kiholela pasipo kufanyika uchambuzi wa ain ayoyote kuwatamnbua wale wanaopaswa kunufaika na sheria ya 1999.
Kwa kuwa Mhe John Magufuli alikuwa mbunge wakati Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 inapitishwa na Bunge mwaka 1999, ni dhahiri alikuwa akitambua maudhui ya vifungu 15 na 16 kuwa vinawapa haki wananchi waliokuwa wakiishi katika vijiji vya Kimara, Mbezi, Kibamba na Kiruvia n.k ndio maana akakwepa kushirikisha ngazi za Mkoa, Wilaya, Manispaa, Tarafa, Kata na Seriklai za Mitaa katika zoezi hilo la kikandamizaji. Vile vile amekataa majadiliano ya aina yoyote kuhusu suala hilo mapaka sasa na anaendeleza ukandamizaji kwa kutumia ulaghai kuhus msongamano wa magari na mradi wa mabasi yaendayo kasi.
Ni kwa kuzingatia ukwei huu, ukarabati wa barabara ya Morogoro kati ya Dar-Mandizi uliofanyika mwaka 2001 uliwagusa tu wale waliojenga ndani ya hifadhi ya barabara ya Futi 75 kila upande, hata hivyo busara kubwa ilitumika kwa zile nyumba zilizoko katika eneo lililohitajikwa kwa upanuzi wa barabara wakati huo ndizo tu zilizobomolewa, zipo zilizobomolewa zote, nusu, robo zingine uzio tu n.k.
Ibara ya 29 (1a, b) ya Kanuni za Sheria mpya ya Barabara namba 13 ya 2007-Tangazo la Serikali Na 21 la Tar 23 Januari 2009, inatamka kuwa upana wa hifadhi ya barabara kwa barabara zote kuu hapa nchini (Trunk Roads) ziwe za njia moja (single carriageway), au njia mbili (dual carriage ways) utakuwa ni Mita 60 tu, yaani Mita 30 kila upande wa barabara. Ikizingatiwa kuwa hata sheria ya zamani ilitamka kuwa upana wa hifadhi ya barabara kwa barabara zote kuu ya nchini (Trunk Roads) ni Futi 75 kila upande. Na kwa kuzingatia kuwa Ibara ya 27 Kanuni ya mpya inatamka kuwa upana wa chini kabisa wa njia moja ya barabara (lane) katika barabara kuu (Trunk Roads) utakuwa si chini ya Mita 3.25.
Hivyo upana wa hifadhi ya barabara uliowekwa na Kanuni za sheria mpya ya barabara ya 2007 wa Mita 60 unao uwezo wa kuzalisha njia za 18 (lanes) yaani 9 za kuelekea Kibaha na njia 9 (lanes) za kuja Dar. Hivyo madai ya Mhe John Magufuli kuwa msongamano wa magari katika barabara ya Morogoro unasababishwa na watu waliojenga nje ya Mita 60 ndio maana akaagiza nyumba hizo kuwekewa alama ya X hayama ukweli wowote. Aidha hana uhalalai wowote wa kisheria kushinikiza nyumba zilizoko nje ya Mita 30 kila upande wa barabara kati ya Ubungo hadi Kiruvia kubomolewa kwa kuwa hazina uhusiano wowote na msongamano wa magari na hazizuii kwa namna yoyote ile upanuzi wa barabara hiyo.
Kutokana na matendo yasiyo halali ya Mhe John Magufuli, mwaka 2009 wakati Wizara ya Ujenzi inatengenza Kanuni za Sheria mpya ya barabara ilijichanganya pale Waziri mwenye dhamana ya barabara aliponakiri Ibara ya 4 ya Kanuni za Sheria ya barabara-Tangazo la Serikali namba 161 la Tar 05/05 1967, kama ilivyokuwa ikisomeka mwaka 1967 (miaka 43 iliyopita) na hivyo kufanya ibara 29 (2) kuendelea kusomeka kuwa "upana wa hifadhi ya barabara kati ya Ubungo hadi Kiruvia ni Mita 120 sawa na Futi 300 hadi 400"; na hivyo kuwepo mgongano kati ya Ibara hiyo ya Kanuni (Regulation) na maudhui ya vifungu 15 na 16 vya Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya 1999 (Law enacted by the Parliament) katika maeneo yaliyokuwa yakiitwa vijiji vya Kimara, Mbezi, Kibamba na Kiruvia.
Licha ya mgonagno huo kati ya Kanuni na Sheria Ibara ya 29 (2) inapingana na Ibara 29 (1 a,b) inayosemeka kuwa upana wa hifadhi ya barabara kwa barabara zote kuu hapa nchini (Trunk roads) ziwe za njia moja (single carriageway), au njia mbili (dual carriage ways) utakuwa ni Mita 60 tu, yaani Mita 30 kila upande wa barabara.
MY TAKE: WAZIRI MKUU MIZENO PINDA BEING A LAWYER BY PROFESSION AMESHAGUNDUA MGONGANO ULIOPO AMBAO UMESABABISHWA NA UBABE WA MHE JOHN MAGUFULI WA MWAKA 2001 ALIPOVAMIA SECRETLY ARDHI NA MAKAZI YA WANANCHI NA HIVI SASA CLANDESTINELY KUTAKA KOBOMOA NYUMBA ZA WANANCHI KWA KUTUMIA KWA TATIZO LA MSONGOMANO WA MAGARI NA UJENZI WA BARABARA ZA MRADI WA MABASI YAENDAYO KASI AMBAYO HAYANA UHUSIANO WOWOTE NA NYUMBA ZILIZOKO NJE YA MITA 30 KILA UANDE WA BARABARA.
kWA KUWA MWAKA 2008 MRADI WA MABASI YAENDAYO KASI (DART) ULIWALIPA FIDIA HANDSOMELY WAATHRIKA WOTE WA MRADI HUO BILA YA KUJALI POROJO ZA KUWEPO KATIKA HIFADHI YA BARABARA. HIVYO MAGUFULI ANADANGANYA UMMA ANAPODAI KUWA ANATAKA KUBOMOA NYUMBA ZA WATU 120 METRES FROM THE ROAD KWA AJILI YA MRADI HUO.
ILI KUMALIZA MGOGORO HUU ULIOZAA BOMOA BOMOA HOLELA IITWAYO MAGUFULI, AMBAO PIA ULISABABISHA CCM KUPOTEZA JIMBO LA UBUNGO NA VITI KADHAA VYA UDIWANI, KATIKA UCHAGUZI MKUU WA 2010. WAZIRI MKUU PINDA ANATAKIWA KUMWAGIZA MAGUFULI KUONDOA (TO OFFCIALLY DELETE) IBARA YA 29 (2) YA KANUNI MPYA ZA SHERIA YA BARABARA ILIYONAKILIWA KAMA ILIVYO KUTOKA KANUNI ZA 1967 BILA KUZINGATIA MAUDHUI YA VIFUNGU 15 NA 16 VYA SHERIA YA ARDHI YA VIJIJI NAMBA 5 YA 1999.
HIYO ITAONDOA MGONGANO ULIOPO KATI YA KANUNI ZILIZOTUNGWA NA WAZIRI MWENYE DHAMANA (REGULATIONS) NA SHERIA ZILIZOTUNGWA NA BUNGE (LAWS ENACTED BY THE PARLIAMENT); THEREFORE SECTION 29 (1) OF THE REGULATIONS WILL PREVAIL WHICH REAFFIRMS THAT THE ROAD RESERVE IN ALL TRUNK ROADS EITHER SINGLE AND DUAL CARRIAGE WAYS IN TANZANIA IS ONLY 60 METRES.
KATIKA HILI HAMNA HAJA YA KUSUMBUA BARAZA LA MAWAZIRI FOR SUCH MINOR ISSUES OF FEW PEOPLE LOOKING FOR CHEAP POPULARITY THROUGH THE SUFFERINGS OF OTHERS, IT IS JUST KNOWING HOW TO TAME THE ERRANT HORSE.