Je ni vema watu wa bara kuhusika moja kwa moja kuchagua mgombea wa urais wa zanzibar kama CCM wanavyofanya? au wawaachie wenyewe mahamuzi yote?
lakini mkuu sasa huoni ni wakati wa kukuza demokrasia ndani na nje ya vyama kwa mfano rais aliyepita alikuwa anakubalika kwa asilimia 30 tuu ya wajumbe wa zanzibar lakini huku bara ndio tukalazimisha wazanzibar awe mgombea wao hatuoni tunawanyang'anya uhuru wao, au tunafanya znz kama kamkoa ka kisiasa?Mkuu Godwine, jambo hilo limekaa kiutaratibu wa chama zaidi na kamati zake.
Kama sehemu ya muungano zanzibar inapaswa kuwashirikisha Watanzania (wote) kwenye suala la kumpata kiongozi wake, otherwise wanaweza kujisahau wakamchagua mtu mwnye negative effect kwa muungano...
Yup..Zenji inATUMIKA tu na bara kwa maslahi ya kisiasa(remotely controlled)!...Ndio maana hata Muungano unang'ang'aniwa zaidi na watu wa Bara wakati wazenji hawana mpango nao!...Ni ushenzi wa toka zamani ambapo hata mikataba ya Muungano haijulikani iko wapi, na hata ridhaa yenyewe ya Muungano haikutafutwa!
Kama wabara hawatakubali wawe radhi kurudi visiwani na Aro Shirazi yao!!
Point. wazanzibar ni watu wa ajabu. wanalalamika kama vile hawana njia mbadala.Zanzibar si nchi. nchi ni Tanzania, kama kwa hiyari yao waliamua kuungana na Tanganyika ni dhahiri walikuwa tayari kwa maamuzi ya kichama kufanyika na chama. Kwani walipo shindwa chaguzi zote visiwani (tokea 1995 mpaka 2005) walikuwa wanatangazwa washindi kwa maelezo ya watu toka Bara kwani ndiyo walioshika vyombo vya dola. Nina uhakika kama bara wataachia wanzanzibar wenyewe watauana kama senene. Ila bado wana-nafasi ya kujikwamua kama wote wataamua kutomchagua mgombea wa CCM atakayewekwa na bara na kumchagua Maalim Seif kwa 100% na kudemand atangazwe, baada ya hapo CCM bara watajifunza kuwa wanzibar wakichaguliwa mtu na wabara hawampigii kura.
lakini lengo la muungano si kuitawala zanzibar bali kushirikiana katika mambo muhimu kwa hiyo kitendo cha kuwatawala kwa mambo yao ya ndani ni aina ya ukandamizajiwazenji n i kama watoto wetu kwa hiyo c busara luwaachia kujiamulia mambo yao wenyewe ni lazima na muhimu sana kwa cc wabara kuingilia mambo ya kule la sivyo0 kitakuwa kisiwa cha kuzaliasha magaidi.....
Unajua vitu vingine unaongea halafu unakuja kufikiria baadaye badala ya kufikiria kwanza ndio uongee! Ok, tuambie kama wakirudisha Afro-Shiraz ndio itajenga barabara, italeta maji safi ya kunywa, itajenga shule, nk? Au kwa kuwa unadhani kwamba jina linatamkika vizuri vinywani mwa watu ndio maendeleo?
Je ni vema watu wa bara kuhusika moja kwa moja kuchagua mgombea wa urais wa zanzibar kama CCM wanavyofanya? au wawaachie wenyewe mahamuzi yote?